Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Mh. Major

Nafasi za uteuzi aufanyao Mh. Rais katika ngazi yoyote haziombwi kihivyo! Lakini pia ujue kuna watanzania kibao kama wewe wanaishi nchini Tanzania. Elimu, uzoefu, uwezo na utendaji wao wa kazi unajulikana vema. Kama kweli, uko serious rudi nchini, shirikiana na watanzania wenzako katika shida na raha na wakujue pia upate muda wa kuwajua vizuri ikiwa ni pamoja na shida zao. Wananchi wakishakujua dhamira na uwezo wako, ni wao watakupatia uongozi aidha wa kuchaguliwa au wa kuteuliwa na Mh. Rais. Uteuzi hauji by chance, mara nyingi ni thru vetting na vetting ni watu wanaulizwa juu ya uwezo na utendaji wako wa kazi. Lakini pia ni lazima wajue itikadi yako, maana nafasi ya DC na RC ni kumwakilisha Mh. Rais....ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama husika ya 2005-2010 na 2010-2015.

Wenzako tayari wanajipitisha pitisha katika lango kuu la Ikulu Dar wakisubiria uteuzi. Mwenzangu ninadhani uko mbali.....du...Fimbo ya mbali haiui nyoka! Rudi tu nafasi ni nyingi na si lazima kipindi hiki! Samahani kama sijakusaidia...........pengine wengine watakupa moyo.

Mkuu mbona umekurupuka kujibu wazo la kijana mwenzetu?

Amekwishasema kwamba anataka kutatua tatizo la barabara za jiji la Dar-Es-Salaam na pia kuhakikisha jiji linakuwa safi.

Mimi nafikiri anafaa kuteuliwa awe mbunge wa kuteuliwa na baadae mkuu wa mkoa. Raisi kama anapitaa humu aangalie hii.

Du!
 
Nchini Kenya kuna wizara kamili kwa ajili ya kuendeleza jiji la Nairobi, vilevile nadhani hata Uganda wanayo. Nionavyo ni wakati muafaka tukapata hii wizara tuachane na mambo ya mkuu wa mkoa. Dar has different challenges compared to other regions, i.e. Katavi, Mtwara, Kilimanjaro etc.
Just thinking loudly.
Bob
 
Cafeteria, Ma-hall eg hall 2 and 5 yanakera kwa uchafu na harufu
 
Cafeteria, Ma-hall eg hall 2 and 5 yanakera kwa uchafu na harufu
 
Ndugu zangu,

Kama kuna jambo linalotia kinyaa katika Jiji la Dar es Salaam ni uchafu uliozagaa kila kona ya Jiji. Kwa mgeni anayefika Jiji la Dar kwa njia ya barabara lazima atakaribishwa na mlundikano wa uchafu kuanzia Ubungo hadi ndani ya Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani. Halikadhalika, kwa wanaofika kwa njia ndege, meli na treni hali ni ileile. Lazima watapokelewa na takataka. Kila kona utakayozunguka Dar, lazima ukutane na uchafu.

Jambo nalojiuliza ni je, hivi viongozi wetu hawaoni huo uchafu wanapopita!? Je, Rais wetu ambaye bila shaka ndiye kinara wa marais wote duniani kwa kutembelea nchi za watu, haoni aibu anapoona miji ya wenzie inapendeza!? Je, ni mbinu gani au mfumo gani tunaweza kuutumia kuboresha hali ya mazingira katika Jiji la Dar es Salaam. Karibuni wakuu.
 
Magogoni na harufu ya ferri ndio majanga zaidi..
 
Ni aibu kwa wananchi wote wa dar ambao wamezoea uchafu

kiongozi,
kama wamezoea ni wazi hawawezi kuona aibu tena. ila sisi wapenda usafi ndo tuwahurumie. tanzani lile soko la samaki magogoni , JICA walitujengea na wakakabidhi likiwa safi, tena karibu na ngome yetu. lakini leo hii amini nakwambia ukitaka kuacha kula samaki nenda kwa lile soko itakuwa ni dawa raisi kabisa ya kukukatisha kula samaki. aidha ngome yetu imezungukwa na harufu ambayo ni nzito hata nyoya la ndege lina elea kwa harufu ile
 
nilitembea toka mkapa hause hadi stesheni sikukuta hata dustbin hamadi nikakuta moja stesheni pale na yenyewe imetoboka... Wtf na hawa viongozi.
No dhahiri nchi wameishindwa
 
Poor planning! Akili mbovu ya Magamba. Huwezi weka kila kitu Dar. Threshold level imevukwa
 
Nenda Moshi ukitaka kujuwa usafi ni nini,ccm imeshapigwa chini kitambo tu na mji msafi kwa sana tu,watu ni waelewa na wastaarabu!Hakuna uchafu kama Dar.
Mt.+Kilimanjaro+from+Moshi.jpg
 
Nipo dar kwa siku yatano sasa nilichogundua hapa ni
1)Uchafu kuna uchafu wa kutisha lakini cha ajabu wakazi wake hawaushangai manake kama ni sehemu ya maisha yao. usishangae dar ukaona sufuria la supu katikati ya maji machafu ila watu wanakunywa na hawahofu.
2) Tatizo la usafiri hadi inakera hili lipo na litaendelea kuwepo.
3)Joto kama kawa.
 
Ulichokiona Dar kiache hapo hapo.lol!
umekuja kutembea na uishie matembezi!
Haya mambo mengine tuachievwenyewe, mvua ikinyesha ukiwa mitaa hii ya kwetu hutaitamani DAr Milele!
 
Ulichokiona Dar kiache hapo hapo.lol!
umekuja kutembea na uishie matembezi!
Haya mambo mengine tuachievwenyewe, mvua ikinyesha ukiwa mitaa hii ya kwetu hutaitamani DAr Milele!

Sawa mkuu ila!!!!
 
Nipo dar kwa siku yatano sasa nilichogundua hapa ni
1)Uchafu kuna uchafu wa kutisha lakini cha ajabu wakazi wake hawaushangai manake kama ni sehemu ya maisha yao. usishangae dar ukaona sufuria la supu katikati ya maji machafu ila watu wanakunywa na hawahofu.
2) Tatizo la usafiri hadi inakera hili lipo na litaendelea kuwepo.
3)Joto kama kawa.

Kuna watu wanalipwa kila mwezi, sijui wanafanya nini kwenye hayo maofisi, Kituo kikuu cha mabasi Ubungo kilivyo oza na kunuka utafikiri nchi iko vitani kwamaana hakuna anaewajibika.
 
Nipo dar kwa siku yatano sasa nilichogundua hapa ni
1)Uchafu kuna uchafu wa kutisha lakini cha ajabu wakazi wake hawaushangai manake kama ni sehemu ya maisha yao. usishangae dar ukaona sufuria la supu katikati ya maji machafu ila watu wanakunywa na hawahofu.
2) Tatizo la usafiri hadi inakera hili lipo na litaendelea kuwepo.
3)Joto kama kawa.
Mkuu hujakamilisha orodha yako....jiji LINANUKA. Ukipita mitaani unasikia harufu ya inya, kwa kweli ni aibu kubwa.
 
Back
Top Bottom