Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Uchafu mitaani Dar: Nani alaumiwe?

Tatizo tukiangalia wale wazee eti ni madiwani wote ni vihiyo tu na wengi ni waswahili wa pwani ambao uchafu ni jadi yao. Ukiangalia meya wa jiji au mameya wa manispaa za ilala, temeke na kinondoni wote ni bure tu ila kwa sababu tu wanaitukuza CCM basi ndo hivyo tena.
 
Tunasema uchafu au usafi ni jadi ya watu. Lakini Usafi ni Sanaa, au Tathnia kamili inayojitegemea, na inahitaji wataalamu waliobobea kwenye fani na wenye uwezo wa kupanga mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu ya Usafi wa miji.

Ukiongelea usafi Bongo maana yake ni Akina mama wale waliovaa Reflector jackets wakiwa barabrani wanafagia na kumeza viroba tele vya vumbi.

We need changes...Elimu iingie na kutumika kwenye mambo haya.
 
Ni jambo la kushangaza kuwa katika mji wa moshi ukitupa hata ganda la pipi faini ni tsh. 50,000/= na ndilo haswa linaloufanya mji ule uwe msafi kuliko miji yote hapa tanzania. Sasa jambo la kuniishangaza ni kuwa hivi hawa wahusika wa jiji hawawezi kwenda kujifunza hapo moshi au wanasubiri kupelekwa nje ya nchi?
 
Kwa kweli hata mimi suala la uchafu dsm linaniudhi mpaka natamani ningepewa ukuu wa mkoa niforce usafi wa lazima. Lakini pia ukiangalia uchafu uliopo tunauleta wenyewe. Mtu kanununua vocha akishaweka anatupa popote. Kanunua ndizi sijui maji au embe au mahindi anakula akimaliza anatupa popote. awe kwenye daladala gari binafsi anatembea its all the same. wakati mtu huyo huyo angeweza kuifadhi huo uchafu wake akifika kwake atupe au akifika palipo na pipa la taka atupe. uchafu hautajaa uishe kwa jinsi hii.

Am so proud of my small town MOSHI. kuja nakuishi dar ni kwa sababu ila si kwa kupenda.
 
NI AIBU iliyoje kwamba jiji hili pamoja na viongozi wetu kuwa wanakwenda nje kila siku na kuona jinsi miji ya wenzetu ilivyo mizuri na misafi ndilo linaloongoza kwa uchafu. Japo bahari ni pua na mdomo, lakini eti maji yanasimama na kutuama Magogoni karibu na ofisi yao.
Hivi, wenzangu Watanzania mna habari kuwa serikali nzima ya Tanzania iko katika kata moja tu hapa nchini ? Kweli si uzushi, Magogoni, Kivukoni!
Wakati wengine wanazungumzia kila mkoa uwe na makao makuu ya angalau wizara moja ....sisi jamaa wanatupa shida ya foleni na uchovu usiokwisha wa kuweka serikali nzima katika kata moja!
Na jamaa ndio weshashinda kura tena basi tungoje maumivu zaidi na shida tupu kila kukichwa. Naona kama tunarudi nyuma au ni basi la dunia na majirani wanaotupita ndilo linalofanya nione kama twarudi nyuma vile.
Hivi maendeleo kweli yataweza kupatikana chini ya utawala wa chama kimoja? Ndio chama kimoja kwani wewe unaona kuna vyama vingi. Mimi sividioni. Tazama kura ya bajeti ilivyotembezwa kibabe bungeni. Kwenye bajeti inayofuata mfumo uliopitwa na wakati, ya mazoea, na ambayo inachangia asilimia -0.001 ya maendeleo ya mwananchi wa kawaida kijijini.
 
Hygiene refers to keeping things clean in order to fight against illness and disease.

Wa-tanzania wengi wamezaliwa wagonjwa - so they can not notice the difference between the two
 
Ni kweli. Viongozi wetu wengi wakiongozwa na rais ni wabutu wa kutambua hilo. Wameridhika na hali walizo nazo. Hizo kero unazosema haziwakumbi wao. Wanaishi kama wako ulaya kwa mazingira waliyojijengea. Hakuna kiongozi wa juu anaejua adha ya foleni wala dhiki za kawaida
 
UCHAFU katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam ni moja ya matatizo makubwa ambayo dhahiri uongozi wa jiji hilo umeonekana kushindwa kuyapatia ufumbuzi. Ni aibu kubwa kwa jiji hili ambalo linapaswa kuwa kioo cha taifa letu kwa usafi, kukithiri kwa uchafu katika maeneo yake mbalimbali, pamoja na wanayofikia wageni kutoka nje.

Nionavyo ni kama viongozi wetu wanazidi kufumbia macho tatizo hilo, licha ya kupata nafasi ya kutembelea nchi nyingi duniani ambazo mimi naamini wamepata fursa ya kujifunza.

Naamini wamejifunza mambo mengi, lakini pia hili la usafi wakafahamu wenzetu wanafanyaje hata miji yao ikawa katika viwango vya usafi vya hali ya juu.

Iwapo wameshindwa kufanya wao waende kwingine kujifunza hasa katika Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro au katika Manispaa ya Iringa. Ni hakika kuwa miji hii imepiga hatua kubwa inayofaa kupigiwa mfano kwa usafi na ziara za watendaji wa Dar es Salaam zinaweza kusaidia kutimiza azma hiyo.

Lakini, sioni kwa nini Moshi au Iringa waweze na Dar es Salaam ambako ni makao makuu ya shughuli karibu zote za nchi, washindwe. Naamini hapa kuna tatizo tena tatizo linalofaa kutazamwa kwa jicho kali kama la fundi saa anapomhudumia mteja wake.
Ni wazi kuwa katika Jiji la Dar es Salaam kuna upungufu mkubwa wa vifaa vya kuwekea takataka hasa katika vituo vya mabasi ya abiria (daladala), viwanja vya mpira na maeneo ya kazi.

Ni kutokana na hali hiyo ni vigumu kumshawishi mtu kwa kumbebesha taka kuanzia eneo la kazi au kituoni na kwenda nao hadi nyumbani kwake kwenye kifaa cha kuhifadhia taka kabla ya kuzitupa.

Hali hiyo inawashawishi watu kutupa takataka ovyo, hasa chupa za maji na mifuko ya plastiki.Ni wazi kuwa uchafu husababisha magonjwa ya milipuko hususan kuhara na kipindupindu.

Ni bora kuepuka hali ya uchafu badala ya kuiachia na likitokea tatizo ndio kuanza kukimbizana nalo bila mpango na kuingia gharama kubwa za matibabu kwa magonjwa ya kuambukiza. Tukumbuke kuwa kuzuia ni bora kuliko kutibu na hili ndilo linaloweza kuisaidia Dar es Salaam.

Sioni sababu za magonjwa ya mlipuko kuendelea kuisumbua Dar es Salaam na wakazi wake hasa wakatio huu wa mvua za masika. Nakubali kuwa mvua hizo zinaongeza changamoto na hatari ya magonjwa ya mlipuko kwani wapo wanaozitumia vibaya kwa kufungulia mifereji ya maji machachu na kinyesi.

Inashangaza upitapo maeneo mbalimbali ya jiji hili kama Kariakoo, Manzese, Tandale na kukutana na baadhi ya watu katika maeneo tofauti wakiwa wameyafungulia mabomba yao yanayotoka vyooni na kumwaga uchafu huo nje, tena katikati ya jiji.

Tatizo lililopo ni kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za jijini Dar es Salaam kuzoea kufanya kazi kwa mazoea, wamekariri utendaji baada ya mambo kadhaa kufanyika.

Nikumbushe siku moja nikiwa katika moja ya ofisi za jiji hilo nilimsikia mmoja wa mabosi akitamba, "Bwana, sisi tunashukuru kwa kipindi hiki tumepiga hatua sana katika maeneo yetu hakuna mtu aliyeugua wala kubainika kuwa na magonjwa ya milipuko’ (kipindupindu)."

Sikuamini kuwa kauli ile ilikuwa ya bosi huyo aliyekuwa akitamka hayo, kisa eti hajatokea mtu mwenye maradhi hayo mwaka huu, lakini wakati anaongea hayo maeneo yanayozingira ofisi zake ni machafu mno kiasi cha kutoelezeka.

Ni jambo la msingi na ni wakati muafaka kwa watendaji wa jiji la Dar es Salaam sasa waende wakajifunze kwa wenzao wa Moshi na Iringa waliweza kufanya nini katika kuimarisha usafi.Wanachotakiwa kufanya ni kujifunza na kuchota mafanikio ya miji hiyo na kuondoa changamoto hizo za usafi kwa jiji la Dar es Salaam.

Binafsi nafikiri kuna kila sababu kwa Dar es Salaam kuwa safi tena kwa wakati wote.

Natambua kuwa manispaa za jiji hilo zimejiwekea sheria ndogo ya kuwakamata na kuwatoza faini wanaotupa ovyo taka, hilo sipingani nalo na ninaliunga mkono.

Lakini, hili la kujikusanyia mamilioni ya faini hakutasaidia chochote, ikiwa hakuna mabadiliko ya kusambaza vifaa vya kutosha kukusanyia taka.Nashauri kwamba pamoja na kujifunza kutoka Iringa na Moshi, elimu kwa umma kuhusu usafi wa manispaa na Jiji kwa ujumla yake inahitajika.

Ni muhimu pia kwa jiji na manispaa zake zote tatu kuweka mfumo wa mafunzo kwa wakazi wake badala ya kuishia kufukuzana na wamachinga na kujikusanyia faini kutoka kwa watu wanaotupa ovyo taka.Elimu hii inayohusu usafi wa mazingira yafaa iwashirikishe watendaji wote kuanzia ngazi za chini katika serikali za mitaa, kata hata tarafa.

Kwa kutenda hayo yote kuwe na mashindano ya usafi yatakayoanza kwa kushindanisha ngazi ya mtaa kwa mtaa hadi kufikia hatua ya mwisho ya kushindanisha manispaa kwa manispaa na washindi kupewa zawadi kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya usafi mara kwa mara.

Nionavyo, bila darasa la kutosha kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira itakuwa ni ndoto Dar es Salaam kuwa safi na ni kazi bure isiyokuwa na tija kuendelea kuwakamata na kuwatoza faini watu wanaotupa ovyo taka.

Niashauri kuwa kuweka mazingira katika hali ya usafi siyo mpaka yatokee magonjwa ya mlipuko na ndiyo maana tunatakiwa sote kujua mapema maana halisi ya usafi wa mazingira kama wenzetu wa Moshi na Iringa walivyofanya na kufanikiwa.

Pamoja na darasa la usafi yapo mambo mengi yanayotakiwa kurekebishwa moja likiwa magari ya kubebea uchafu.

Haiwezekani magari hayo yakawa ni ya kuhesabika wakati matumizi yake ni makubwa.

Hapa nashauri pia serikali ikopeshe gari la taka kwa kila kata kama inavyofanya kuwakopesha wabunge magari ili iweze kusaidia kupunguza uhaba wa magari ya taka ikiwa ni pamoja na vitendea kazi vingine.
 
Moshi watu wanajituma, sio lazima serikali iwaambie waweke maeneo safi, wanaweka maana ni kitu cha msingi...
 
UCHAFU katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam ni moja ya matatizo makubwa ambayo dhahiri uongozi wa jiji hilo umeonekana kushindwa kuyapatia ufumbuzi. Ni aibu kubwa kwa jiji hili ambalo linapaswa kuwa kioo cha taifa letu kwa usafi, kukithiri kwa uchafu katika maeneo yake mbalimbali, pamoja na wanayofikia wageni kutoka nje.

Nionavyo ni kama viongozi wetu wanazidi kufumbia macho tatizo hilo, licha ya kupata nafasi ya kutembelea nchi nyingi duniani ambazo mimi naamini wamepata fursa ya kujifunza.

Naamini wamejifunza mambo mengi, lakini pia hili la usafi wakafahamu wenzetu wanafanyaje hata miji yao ikawa katika viwango vya usafi vya hali ya juu.

Iwapo wameshindwa kufanya wao waende kwingine kujifunza hasa katika Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro au katika Manispaa ya Iringa. Ni hakika kuwa miji hii imepiga hatua kubwa inayofaa kupigiwa mfano kwa usafi na ziara za watendaji wa Dar es Salaam zinaweza kusaidia kutimiza azma hiyo.

Lakini, sioni kwa nini Moshi au Iringa waweze na Dar es Salaam ambako ni makao makuu ya shughuli karibu zote za nchi, washindwe. Naamini hapa kuna tatizo tena tatizo linalofaa kutazamwa kwa jicho kali kama la fundi saa anapomhudumia mteja wake.
Ni wazi kuwa katika Jiji la Dar es Salaam kuna upungufu mkubwa wa vifaa vya kuwekea takataka hasa katika vituo vya mabasi ya abiria (daladala), viwanja vya mpira na maeneo ya kazi.

Ni kutokana na hali hiyo ni vigumu kumshawishi mtu kwa kumbebesha taka kuanzia eneo la kazi au kituoni na kwenda nao hadi nyumbani kwake kwenye kifaa cha kuhifadhia taka kabla ya kuzitupa.

Hali hiyo inawashawishi watu kutupa takataka ovyo, hasa chupa za maji na mifuko ya plastiki.Ni wazi kuwa uchafu husababisha magonjwa ya milipuko hususan kuhara na kipindupindu.

Ni bora kuepuka hali ya uchafu badala ya kuiachia na likitokea tatizo ndio kuanza kukimbizana nalo bila mpango na kuingia gharama kubwa za matibabu kwa magonjwa ya kuambukiza. Tukumbuke kuwa kuzuia ni bora kuliko kutibu na hili ndilo linaloweza kuisaidia Dar es Salaam.

Sioni sababu za magonjwa ya mlipuko kuendelea kuisumbua Dar es Salaam na wakazi wake hasa wakatio huu wa mvua za masika. Nakubali kuwa mvua hizo zinaongeza changamoto na hatari ya magonjwa ya mlipuko kwani wapo wanaozitumia vibaya kwa kufungulia mifereji ya maji machachu na kinyesi.

Inashangaza upitapo maeneo mbalimbali ya jiji hili kama Kariakoo, Manzese, Tandale na kukutana na baadhi ya watu katika maeneo tofauti wakiwa wameyafungulia mabomba yao yanayotoka vyooni na kumwaga uchafu huo nje, tena katikati ya jiji.

Tatizo lililopo ni kwa viongozi wa ngazi mbalimbali za jijini Dar es Salaam kuzoea kufanya kazi kwa mazoea, wamekariri utendaji baada ya mambo kadhaa kufanyika.

Nikumbushe siku moja nikiwa katika moja ya ofisi za jiji hilo nilimsikia mmoja wa mabosi akitamba, "Bwana, sisi tunashukuru kwa kipindi hiki tumepiga hatua sana katika maeneo yetu hakuna mtu aliyeugua wala kubainika kuwa na magonjwa ya milipuko’ (kipindupindu)."

Sikuamini kuwa kauli ile ilikuwa ya bosi huyo aliyekuwa akitamka hayo, kisa eti hajatokea mtu mwenye maradhi hayo mwaka huu, lakini wakati anaongea hayo maeneo yanayozingira ofisi zake ni machafu mno kiasi cha kutoelezeka.

Ni jambo la msingi na ni wakati muafaka kwa watendaji wa jiji la Dar es Salaam sasa waende wakajifunze kwa wenzao wa Moshi na Iringa waliweza kufanya nini katika kuimarisha usafi.Wanachotakiwa kufanya ni kujifunza na kuchota mafanikio ya miji hiyo na kuondoa changamoto hizo za usafi kwa jiji la Dar es Salaam.

Binafsi nafikiri kuna kila sababu kwa Dar es Salaam kuwa safi tena kwa wakati wote.

Natambua kuwa manispaa za jiji hilo zimejiwekea sheria ndogo ya kuwakamata na kuwatoza faini wanaotupa ovyo taka, hilo sipingani nalo na ninaliunga mkono.

Lakini, hili la kujikusanyia mamilioni ya faini hakutasaidia chochote, ikiwa hakuna mabadiliko ya kusambaza vifaa vya kutosha kukusanyia taka.Nashauri kwamba pamoja na kujifunza kutoka Iringa na Moshi, elimu kwa umma kuhusu usafi wa manispaa na Jiji kwa ujumla yake inahitajika.

Ni muhimu pia kwa jiji na manispaa zake zote tatu kuweka mfumo wa mafunzo kwa wakazi wake badala ya kuishia kufukuzana na wamachinga na kujikusanyia faini kutoka kwa watu wanaotupa ovyo taka.Elimu hii inayohusu usafi wa mazingira yafaa iwashirikishe watendaji wote kuanzia ngazi za chini katika serikali za mitaa, kata hata tarafa.

Kwa kutenda hayo yote kuwe na mashindano ya usafi yatakayoanza kwa kushindanisha ngazi ya mtaa kwa mtaa hadi kufikia hatua ya mwisho ya kushindanisha manispaa kwa manispaa na washindi kupewa zawadi kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya usafi mara kwa mara.

Nionavyo, bila darasa la kutosha kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira itakuwa ni ndoto Dar es Salaam kuwa safi na ni kazi bure isiyokuwa na tija kuendelea kuwakamata na kuwatoza faini watu wanaotupa ovyo taka.

UNAONAJE KAMA UKIWAALIKA WATENDAJI WA JIJI WAKAJA KUJIFUNZA NYUMBANI KWAKO KBLA YA MS/IR
 
Watendaji ni wavivu wanaendekeza njaa,waroho hovyo ndio wanaopindisha sheria ndogondogo ,hawafai wote mameya wabunge madiwani wa Dar es Salaam wana akili kama wanautapiamlo hawafai kuwa viongozi jiji la Dar es Salaam ni chafu kuliko majiji yote duniani
 
lakini kwanini wananchi wanawachagua?kweli ibaboha sana
Watendaji ni wavivu wanaendekeza njaa,waroho hovyo ndio wanaopindisha sheria ndogondogo ,hawafai wote mameya wabunge madiwani wa Dar es Salaam wana akili kama wanautapiamlo hawafai kuwa viongozi jiji la Dar es Salaam ni chafu kuliko majiji yote duniani
 
Usafi moshi ni tabia yao nakumbuka niliwahi jaribu kujisaidia maeneo ya mashujaa nilikimbizwa kule kwenye makaburi nlipodakwa faini .pia miinuko ya moshi na iringa inasadia mijikuwa safi ndomaana ukienda njoro moshi au mlandege iringa ni kuchafu
 
Kilimasera+froida: hoja zenu haziwezi kuisaidia jamii ya wana Dsm hata kidogo. Hivi unahitaji nguvu ya watendaji ili usitupe chupa ya maji barabarani?. Nashauri muwaalike watendaji wa jiji waje kutazama hali ya usafi mitaani kwenu ili wajifunze kabla ya kwenda moshi na iringa.
 
Watanzania wenzangu, nimesikia tetesi kuwa Raisi anawateua wakuu wa mikoa sasa.Mimi naomba kupitia mtandao huu wa jamii na kwa nia njema kabisa na dhamira ya kweli, mniombee kwa Jk anipe nafasi ya ukuu wa mkoa wa DAR.

Dhamira yangu ya kwanza ni kuhakikisha foleni inakuwa ni hadithi DAR, na kazi yangu ya pili ni kuhakikisha DAR, Inakuwa ni sehemu safi na yenye hadhi ya jiji kama yalivyo majiji mengine Duniani.

MASHARTI YANGU;
Naomba nipewe mkataba wa miaka 10
Naomba nipewe uhuru wa kufanya maamuzi
Serikali inihakikishie kutokatika kwa umeme kwa kipindi chote cha miaka 10.
Sintohitaji ruzuku yoyote toka serikali kuu

MWISHO;
Kama serikali itakubaliana na mimi basi nitakuwa tayari kufanya nao mkataba huru na nitarudi nyumbani Tanzani kwa ajili ya kazi hiyo maalumu. kwa mawasiliano ya mwanzo wanaweza kunipata kupitia mtandao huu wa JF, wakishakuwa sawa nitawapa anuani kamili, niko serius.
 
Mh. Major

Nafasi za uteuzi aufanyao Mh. Rais katika ngazi yoyote haziombwi kihivyo! Lakini pia ujue kuna watanzania kibao kama wewe wanaishi nchini Tanzania. Elimu, uzoefu, uwezo na utendaji wao wa kazi unajulikana vema. Kama kweli, uko serious rudi nchini, shirikiana na watanzania wenzako katika shida na raha na wakujue pia upate muda wa kuwajua vizuri ikiwa ni pamoja na shida zao. Wananchi wakishakujua dhamira na uwezo wako, ni wao watakupatia uongozi aidha wa kuchaguliwa au wa kuteuliwa na Mh. Rais. Uteuzi hauji by chance, mara nyingi ni thru vetting na vetting ni watu wanaulizwa juu ya uwezo na utendaji wako wa kazi. Lakini pia ni lazima wajue itikadi yako, maana nafasi ya DC na RC ni kumwakilisha Mh. Rais....ikiwa ni pamoja na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama husika ya 2005-2010 na 2010-2015.

Wenzako tayari wanajipitisha pitisha katika lango kuu la Ikulu Dar wakisubiria uteuzi. Mwenzangu ninadhani uko mbali.....du...Fimbo ya mbali haiui nyoka! Rudi tu nafasi ni nyingi na si lazima kipindi hiki! Samahani kama sijakusaidia...........pengine wengine watakupa moyo.
 
Watanzania wenzangu, nimesikia tetesi kuwa Raisi anawateua wakuu wa mikoa sasa.Mimi naomba kupitia mtandao huu wa jamii na kwa nia njema kabisa na dhamira ya kweli, mniombee kwa Jk anipe nafasi ya ukuu wa mkoa wa DAR.

Dhamira yangu ya kwanza ni kuhakikisha foleni inakuwa ni hadithi DAR, na kazi yangu ya pili ni kuhakikisha DAR, Inakuwa ni sehemu safi na yenye hadhi ya jiji kama yalivyo majiji mengine Duniani.

MASHARTI YANGU;
Naomba nipewe mkataba wa miaka 10
Naomba nipewe uhuru wa kufanya maamuzi
Serikali inihakikishie kutokatika kwa umeme kwa kipindi chote cha miaka 10.
Sintohitaji ruzuku yoyote toka serikali kuu

MWISHO;
Kama serikali itakubaliana na mimi basi nitakuwa tayari kufanya nao mkataba huru na nitarudi nyumbani Tanzani kwa ajili ya kazi hiyo maalumu. kwa mawasiliano ya mwanzo wanaweza kunipata kupitia mtandao huu wa JF, wakishakuwa sawa nitawapa anuani kamili, niko serius.

Ebu fafanua utafanya niniau maamuzi gan ili hiyo foleni ipungune ?
 
Kweli una nia nzuri na inaonekana umezamilia pengine ukipewa nafasi unaweza ukafanya kweli; ila we ni mwana-magamba? kama jibu ni Ndiyo, mtafute riz1 akupigie debe ndo kazi yake hiyo kama alivyofanya kwa kijana wakisuma(Marsha) aliyetoka ughaibuni akanyakua Ubunge na hatimaye Uwaziri fastafasta.
 
Dar ni moja ya majiji yaliyokithiri kwa uchafu duniani. Wiki chache zilizopita ilianzishwa kampeni ya usafi nchi nzima, lakini sasa haisikiki tena!
 
Back
Top Bottom