Ubungo kariakoo

Ubungo kariakoo

Mkuu hakuna kitu, yani kipnd hcho ndo kidogoo mlikua mna jitahidi ukakamavu,sikuizi mnakula mpaka vumbi la ikwiriri
Mkuu,tuheshimiane tafadhali. Huko nimehama baada ya vita vya kagera. Bahari ilikuwa na samaki wakutosha kabisa,mpunga tunalima sinza.
 
Hiyo Ilikuwa bonde la msimbazi, naona Kajima wanajenga barabara kuna taxi Peugeot 404 nakumbuka mbali sana.

Enzi hizokulikuwa na"Simba Ruala" M'Nyamala Kariakoo, "Jadide" Ubungo Posta


Mkuu EWGM's ,

Umenikumbusha mbali sana mitaa ya Mwananyamala A enzi hizo..
 
Enzi hizo kila mkoa kuna kampuni ya mabasi ya serikali, Morogoro tulikuwa tunatumia MORETCO!

Nakumbuka tulikuwa tunasafirishwa jkwenda mashuleni (Sekondari) bure kwa nauli za serikali. Shule zikifungwa tunarudishwa kwa treni au bus.
 
Alafu inawezekana ubungo kwenda kariakoo ilikuwa mbali sana wakati huo naona na barabara ilikuwa ya moramu.Kweli mlifaidi sana enzi hizo so natural,chai ya maziwa ikiwa inatoka kwenye mabomba UDSM na Nyama za makopo za Tanganyika Perkers.

kuna basi lilikua linaenda posta liliitwa dau la mnyonge
 
Kipindi hicho hata trafic police kumuona barabarani ilikuwa ni bahati mbaya. Taxi peugeot 304 milango yake ilifunguka kutokea mbele kuelekea nyuma na hakukuwa na dereva kijana.
 
Back
Top Bottom