mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,212
- 6,409
Kocha Nabi namsifia sana kutokana kuitengeneza Yanga kucheza kitimu zaidi na mbinu zake katika kuzikabili mechi kubwa
Tukiachana na usajili wa wachezaji wazuri, tuhuma za kuhonga na mbinu nyingine nje ya uwanja ni kwamba huyu kocha ni chachu kubwa sana ya mafanikio ya timu ya Yanga uwanjani
Ukiwaangalia Yanga kikosi kizima ni wacheza wawili tu ndio wenye uhakika wa kuanza kila mechi, mtaani tunasema ' panga pangua' ni Golikipa Diarra na Mshambuliaji Mayele, na ni kwa vile tu viwango vyao ni vikubwa sana. Waliobakia wote hakuna mwenye uhakika wa kuanza, hii ni kwa sababu Yanga inacheza kitimu zaidi kuliko kutegemea mchezaji mmoja mmoja.
Mfano mzuri angalia mechi kubwa za Yanga, dhidhi ya Simba na dhidi ya Rivers United ( ya marudiano). Kikosi chao kilibadilika kwa kiasi kikubwa sana, tofauti na Simba ambao mechi yao dhidi ya Yanga na Wydad kikosi kilikuwa almost ni kilekile. Msimu mzima Nabi amekuwa hivyo.
Simba inajulikana kabisa Kulia Shomari, kushoto Hussein, kati Onyago na Inonga, kati na kuendelea ni hivyo hivyo labda mtu aumie.
Ubora huu wa Nabi naamini utawapa mafanikio makubwa mashindano ya kimataifa na wana nafasi kubwa kuchukua kombe la shirikisho hata mwakani au miaka michache inayo wananafasi kufika mbali ligi ya Mabingwa hata fainali au kuchukua. Sasa hivi gape baina ya timu zetu za Tanzania na Afrika Kaskazini na Magharibi limepungua. Simba imefika mara kadhaa Robo na kote kutolewa kwa tofauti ndogo sana hivyo naamini haya makombe kwa miaka hii kuna nafasi ya kuyabeba. Nakumbuka Simba kutolewa na Kaizer Chiefs na Orlando kwa tofauti ndogo sana.
Kama mshabiki wa Simba naukubali uwezo wa Kocha Nabi Nasreddeen na naamini watatamba zaidi ya Simba kimataifa