Ubinafsi ni changamoto katika mirathi

Muuza Viat

JF-Expert Member
Dec 23, 2022
2,824
7,350
Mzee alikuwa mfanyakazi wa bandari ya Dar kama zimamoto geti no.7/8 mpaka alipostaafi.

Kilichomgharimu huyu Mzee ni kama wazee wengine tu alijenga kijijini kwake akiamini baada ya kustaafu angerudi huko lkn mwishowe alibadili gia angani na kulazimika pesa ya kustaafu ndio aitumie kujenga jengo la makazi.

Alifanikiwa kupata nyumba kubwa ya vyumba sita ambayo alipangisha na banda la ubavuni ambalo lina vyumba viwil na sebule ambako ndipo alipokuwa anakaa.

Mkewe wa mwanzo alizaa nae wanne, Mungu akampenda zaidi baadae akamtia mimba mtumishi mwenzie na kufanikiwa kupata mtoto mmoja lkn hakumuoa hatimaye akapata mke kutoka kwao huko na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Baada ya miezi kadhaa Mzee alifariki.

Baada ya mazishi wanandugu walikaa kikao cha familia ili waweze fungua mirathi.

Baada ya majadiliano mafupi ikakubalika watoto wa mke wa mwanzo na wa mwisho kila mmoja atachukua chumba kimoja na mke atamiliki alipokuwa anakaa pamoja na marehemu, changamoto ikawa huyu mtoto mmoja yeye atarithi nini?

Mjumbe mmoja akatoa wazo huku anacheka kuonesha kuwa hakuwa sirias "kwa vile mpaka sasa kimebaki choo tu ndio hakijapata mtu kama vipi arithishwe huyo aliyebaki" watu wakaanza kucheka kama utani lkn cha kushangaza yule mrithi alitoa kauli kuwa yeye yupo tayari kupokea choo kama urithi wake.

Kabla mwanasheria hajaanza kuandika muhtasari wa kile kikao akatoa msisitizo kuwa je kila mmoja ameafiki kile kilichokubaliwa pale majibu, yakawa ndio na wakasisitiza kuwa wapo tayari kusaini maazimio ya kikao.

Ukaandaliwa muhtasari wa kikao kile pamoja na maazimio ya kikao na kila mmoja akasaini.

Baada ya wiki kadhaa kesi ya mirathi ikaisha.

Yule aliyerithi choo akafanya marekebisho makubwa ktk kile choo mpaka wenzake wakaingiwa na hofu.

Choo kimewekwa tiles mpya, milango yote ya vyoo kaweka vitasa funguo kaweka mfukoni.

Na baada ya yale marekebisho akaweka tangazo la gharama kwa ajili ya huduma na hapo zogo likaanza.

Watoto wa wale wake wawili wanaendelea na vikao ili wajibu mapigo.
 
Waliorith vyumba waweke vyoo kwenye vyumba vyao, na aliyerithi choo aweke chumba kwenye choo chake
😂😂😂😂
 
Kivip ndugu tupe ufumbuzi kuhusu ubinafs uliopo
Kila mtu anataka apate kingi kuliko mwenzake

Lkn km kila mmoja atazingatia mwenzake apate ilikua rahisi tu

Nyumba inapangishwa na mnagawana pesa sawasawa kwa kila mmoja
 
Jamaa nimempenda, yeye alikua na kosa gani mpaka wampe choo wakati baba yake na mama yeke wanapiga starehee yeye hata hakuwepo
 
Back
Top Bottom