Changamoto ni burudani katika maisha, burudika nazo badala ya kulialia ovyo

Feb 4, 2024
67
206
Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema ukitaka ufurahie adhabu basi ukipewa usiione kwa sura ya adhabu bali ona kama ni sehemu kama wajibu wako, kwa mfano ukipewa adhabu ya kumwagilia maua wewe ona ni wajibu wako kufanya hiyo ili maua yakue na kustawi.

Changamoto ni burudani kama zilivyo burudani ni ngumu kuburudika bila kuvuja jasho, kwenye suala la burudani kuna upande utavuja jasho na kuna upande utaburudika ila inaitwa burudani na watu hufurahi kwa sababu wameamua kumakinika na upande wa furaha kuliko upande waliovuja jasho.

Maisha ya kukosa kazi kwa muda, kuachwa kwenye mahusiano na mengine mengi yenye sura ya changamoto ni sehemu tu moja wapo ya burudani ambayo ndio ya kuvuja jasho na kama ukiendelea kukaza utafikia ule upande wa pili wa burudani ambao ni wa kufurahia.

Kwenye hii burudani ya maisha hakuna mtu asiyepitia upande wa kuvuja jasho ambao ndio changamoto na burudani haina maana kama itakuwa na upande mmoja tu wa furaha, ukiona watu kwenye viti virefu au kokote wapo wanajipongeza basi jua wana upande mwingine waliopitia ambao ndio uliwapa hizo pesa.

Ikitokea unafukuzwa ama kukataliwa usione kwa sura ya kukomolewa au kama vile umeadhibiwa bali ona hiyo ni sehemu tu ya burudani ambapo unaandaliwa kwenda kukubalika kwingine tena panaweza kuwa pazuri zaidi ya ulipofukuzwa.

Tatizo ni pale ambapo utaiona hiyo changamoto kwa sura ya kukomeshwa hapo utajikuta kwenye maumivu, kulia na kulalamika hovyo kitu ambacho hakitakupa unafuu bali kukuumiza na mbaya zaidi kukufanya uje ukosee tena kwa sababu utafanya maamuzi bila utulivu.

Maisha yana changamoto nyingi sana na nzito ila ukisema kila moja uione kwa sura yake basi kila siku utakuwa mtu wa kulia hovyo badala ya kujifunza kupitia changamoto hizo.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Back
Top Bottom