Ubani una uhusiano gani na mambo ya roho/imani?

Ubani una uhusiano gani na mambo ya roho/imani?

he he he wajihoji kimoyomoyo kila siku? mkuu unaacha miaka inapita, miezi inapita huulizi wanokuongoza kulikon?


umeleta swali zuri sana
mkuu,mara nyingi hata mimi nikiingiaga kanisani tu lazima nihoji
kimoyomoyo swali hili,ngoja mapandri waje watufumbue fumbi hili
 
Una mke? Picha yake hujaiweka ofisini au sebuleni kwako au pengine kwenye wallet? Ni ya kazi gani? Hujawahi ibusu?

Sijaona picha, sanamu ya Mungu kanisani. Nimeona sanamu na picha ya Ubinadamu wa Yesu Kristu ambaye aliishi kati ya watu na watu hawakufa (maana tunaambiwa ukimuona Mungu unakufa).

Sina tatizo kabisa na picha ya Yesu na kiukweli imenisaidia kuanzia nilivyokuwa mdogo kupata picha ya mateso na nini Yesu alikipitia ili kutukomboa, na sijawahi kufikiri ile picha ni Mungu na hivyo kuchukua nafasi ya Mungu. Sana imenisaidia kuujua Upendo wa Mungu kwa wanadamu hadi kuruhusu Mwanawe to go all thru that for unworthy creature like me.

Kumbe!
 
Kufukiza ubani.
Kwa wakatoliki, sijui kuhusu makanisa mengine; ubani ni sehemu muhimu ktk ibada ya misa.
Nimeona na kusikia pia, ubani hutumika ktk kuyaita/kuyapunga majini.
Sasa swali langu hasa kwa wajuvi, ubani una issue gani na spirits? Iwe Holy Spirit au evil spirit?
Pasco upo?
Nijuavyo Mimi Ubani unatumika kwa njia mbili 2 nji ya kwanza ni njia nzuri ya kumuomba Mungu huku ukifukiza ubani. Na njia ya pili ubani unatumika kufanya maombi ya mabaya kwa mfano kuroga na mambo mengine ya uchawi. Sasa inategemea yule Mtumiaji wa huo Ubani anatumia kwa njia gani? nzuri au mbaya. Kazi kwako bibie Kaunga
 
Last edited by a moderator:
About 33AD, wakati wa Pentekoste. Na hata Popes can be traced kuanzia Apostle Peter.




Yesu alipoondoka hakuacha kanisa lililoitwa Roman Catholic.

Na Petro alikataliwa na hao warumi na kumuua kwa hofu ya kuenea kwa ukristo wa kweli kwenye himaya na falme za Kirumi ndipo Mfalme Constantine alipoanzisha Ukristo Chotara Unaitwa Romani Catholiki ,ukiwa ni zao la nusu ukristo na nusu upagani wa Kirumi .Wakiunganisha ibada za miungu ya kirumi na taratibu zake za kishetani kama kubadili sanamu za miungu ya kirumi na kuzipa majina mapya kama bikira maria,mtoto yesu n.k.

Tusipokee dini kama bahari invyopokea maji masafi na machafu.
Yesu aliachana na taratibu za kimila zilizokuwa zinatumiwa na wayahudi kama tatatibu zao za kumuita Mungu bila kujua kuwa Mungu yupo ndani ya mioyo ya watu wema na haji ili anuse ubani kama Wayahudi walivyokuwa wanfikiri.
Imani hizi potofu zilikuwa zikifanywa na wanadamu wote na bila kujali ni Mungu yupi waliyemwamini. Waisrael walipotoka Misri na Babeli walirudi wakiwa na imani iliyochanganyika na imani za dini za miungu ya mataifa hayo waliacha imani ya kweli ya Ibrahim na Isaka na Yakobo.

Yesu alikuja kuvunja na kuharibu kazi za shetani na kuwarudisha watu kwenye Imani ya rohoni ili wahesabiwe haki.

Shetani kupitia utawala wa kidunia naye akauchakachua ukristo kupitia Upapa uliogawana madaraka na Himaya ya Kirumi kwa kumkataba wa kulinda ufalme,mila na dini za warumi,ndipo ilpozaliwa Kanisa la kirumi.

Yesu aliliona hili tangu mwanzo na akasema ''Yaacheni magugu yakue na ngano mpaka siku ya mavuno ndipo magugu yatakapotupwa motoni na ngano kuwekwa ghalani''
 
Nijuavyo Mimi Ubani unatumika kwa njia mbili 2 nji ya kwanza ni njia nzuri ya kumuomba Mungu huku ukifukiza ubani. Na njia ya pili ubani unatumika kufanya maombi ya mabaya kwa mfano kuroga na mambo mengine ya uchawi. Sasa inategemea yule Mtumiaji wa huo Ubani anatumia kwa njia gani? nzuri au mbaya. Kazi kwako bibie Kaunga

Ongezea na udi....au it is the same?
 
Sidhani kama unategemea sura, muundo na mfumo wa kanisa la mwanzo liwe sawa hata baada ya miaka 1900.

Labda ni Jina Katoliki ndio lenye shida hapo, kwamba kikitakiwa kuappear in early church. Lkn kama unazungumzia kanisa na ukristu, (again inategemea unamaanisha nini kwa Ukristu) tunaamini kuwa asili yake ni Kristu, alipomwambia Perto ni nwamba na juu yake ataanzisha kanisa lake. Na assignment ya kuihubiri injili (kazi kuu ya kanisa) ilutolewa siku ya pentecoste baada ya kupata nguvu ya Roho Mtakatifu.

Back to Popes, sidhani pia utalinganisha papacy ya sasa baada ya mfumo na utaratibu kuwepo na kipindi cha Clemency (4th pope) aliye fariki 101ad; na huenda hata cheo hakikutumia Jina hilo lkn functions zinaonesha some sort orders na authorities (refer barua za maelekezo n.k)

Au niambie basi kanisa lililojengwa na Kristu kama alivyoahidi ni lipi?

Kanisa limejengwa ktk mwili wa kristo, Petro hakufa msalabani kwa ajili ya wenye dhambi. Yesu alisema juu ya nafsi yake.kwa kuwa Petro alimtambua Kristo kuwa ni Ndiye aliyetarajiwa.

Kama Petro angekuwa ameshuka kuzimu akamnyang'anya shetani funguo za mauti na kuzimu basi yamkini maneno ya Mungu pale bustanini Adeni kwama uzao wa mwanamke utamponda shetani kichwa.Tungeweza sema kweli ktk petro misingi ya kanisa itajengwa.

Mt.Paulo je naye ameihubiri injili ambayo misingi yake iko katika Petro? La hasha,Paulo ameihubiri injili ambayo misingi yake ni ktk Yeye aliyemzao wa mwanamke na ambaye alishuka kuzimu akashinda, yeye Kristo Yesu ndiye ambaye milango ya kuzimu haitamuweza. Na wale walio wakwake amewapa uwezo wa kuzikanyaga nguvu na malango ya kuzimu. Leo hii wameonesha kile ambacho kilifanywa nyakati za mitume.Wanakemea pepo, wanapoza wagonjwa, wananena kwa lugha mpya. Marko 16:16-18
 
Pole mkuu naona ulikuwa mbio sana... Haya ngoja nikusaidie kumuita Rakims

Nashukuru Kuitwa Hapa.. Mengi Yameongelewa Lakini Ni Kiushabiki Fulani...
Ipo Hivi..

UBANI:
Kwanza Kuna Aina Zaidi Ya Saba Za Ubani...
1: Ubani Makka
2: Ubani Zukura
3: Ubani Somalia
4: Ubani Zuriki
5: Ubani Mweupe
6: Ubani Mweusi
7: Ubani Mtama
8: Ubani Zakari

Nyingine Nimezisahau Kwa Jibu Lisilo Chosha Ubani Unategemea Umechoma Upi Na Kwa Kazi Ipi Usiuhukumu Moja Kwa Moja Kwamba Ni Sheria Au Sio Sheria..

Ubani Ni Fusho Linalosimamiwa Na Malaika,pamoja Na Majini Hujipenyeza Hapo Wale Walioamini Kinachofanywa Pale Kwa Kutumia Ubani Huo..

Ni Fusho Linalotoa Majibu Hapo Hapo Au Baadae.. Kwa Wale Wanaoutumia Huweka Nia Kwamba Nachoma Huu Kwa Sababu Gani Hiyo Ndio Hufanya Kazi Ya Ile Nia.. Zile Mnazoita Spirits Nyingi Huja Zingine Hufata Kula Ule Moshi...

Zinapofika Pale Huja Mbaya Na Nzuri.. Maombi Yako Ndio Hufanya Zijigawe Kwa

Huyu Kafanya Hii Kuomba Mungu,..
Huyu Kafanya Hii Kututuma,

Huyu Kafanya Hii Kutufukuza,

Huyu Kafanya Hii Tumsaidie Kuomba Kwa Mungu..

Huyu Kafanya Hii Tutoe Harufu,

Huyu Kafanya Hii Kutuzawadia, n.k...
Nia Yako Ndio Hufanya Hiyo Kitu Kufanya Kazi....

N.B:
Kwa Wale Ambao Hufanya Kuumiza Au Kuangamiza Kama Imetiki Utaona Moshi Unapanda Juu,
Kama Imegoma Basi Moshi Haupandi Juu Huzagaa Hapo Hapo Chini....

Kwa Wale Wanaotumia Hii Kitu Waweza Kupima Imekubali Ombi Lako Au Imefail Kwa Kupima Hivyo.....

Wengine Wawe Wanapita Tu Kuliko Kushauri Wasioyajua...


#Rakims
 
Last edited by a moderator:
Luka 1:9,11
Zakaria (baba yake yohana mbatizaji) alichaguliwa kwa kura kama ilivyo desturi, kuingia hekaluni ili akafukize ubani. Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.

Umeona kwa aya hizo, Angel (spirit) alikuja baada ya ubani kuchomwa. Na upande wa pili wa darkness pia ubani hutumika. Nafikiri ni sahihi kusema ubani ni mvuto wa spirits, iwe light au dark spirits.

Cc


Luka 1:9,11
Zakaria (baba yake yohana mbatizaji) alichaguliwa kwa kura kama ilivyo desturi, kuingia hekaluni ili akafukize ubani. Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.

Umeona kwa aya hizo, Angel (spirit) alikuja baada ya ubani kuchomwa. Na upande wa pili wa darkness pia ubani hutumika. Nafikiri ni sahihi kusema ubani ni mvuto wa spirits, iwe light au dark spirits.

Cc MziziMkavu


Ok nimekuekewa
 
Last edited by a moderator:
Rakims

Nakuheshimu sana lkn naomba unifafanulie hivi hizi aina za ubani hata huko marekani na ulaya wanatumia majina haya yenye uhusiano (influence) na uislam? kama ubani Makka, Somalia. Au hakuna ubani vatican etc... napata wasiwasi kuwa hapa uislam unanasibishwa na ubani wakati sijawahi kusoma ndani ya qur an au hadithi za mtume zinazoonyesha uhusino huu, zaidi ya baadhi ya mashekhe hasa waliopata elimu kutoka Lamu. Nimepata kusikia kuwa mashekhe hawa walipohitimu dini walishauriwa kuwa wasomee taaluma hii ya ziada ili nao waweze kujiajiri.
 
Rakims

Nakuheshimu sana lkn naomba unifafanulie hivi hizi aina za ubani hata huko marekani na ulaya wanatumia majina haya yenye uhusiano (influence) na uislam? kama ubani Makka, Somalia. Au hakuna ubani vatican etc... napata wasiwasi kuwa hapa uislam unanasibishwa na ubani wakati sijawahi kusoma ndani ya qur an au hadithi za mtume zinazoonyesha uhusino huu, zaidi ya baadhi ya mashekhe hasa waliopata elimu kutoka Lamu. Nimepata kusikia kuwa mashekhe hawa walipohitimu dini walishauriwa kuwa wasomee taaluma hii ya ziada ili nao waweze kujiajiri.

Sijaingiza Dini Hapo Mkuu.. Aina Ya Ubani Inategemea Umechanganywa Vipi Ndio Unapata Kazi Yake Na Umetoka Wapi Ndio Tunapata Jina Lake.. Wao Pia Wanaubani Unaotoka Kwao Na Kwa Majina Yao Lakini Ubani Makka Wenye Ranga Kama Ya Chai Ya Maziwa Hutumika Sana Katika Maombi Mbali Mbali Ya Kumuomba Mungu Tu... Na Ukisema Hujauona Ubani Kwenye Kitabu, Mimi Pia Sijaiona Suruali Kwenye Kitabu... Ikiwa Hivyo Kitabu Kingeandikwa Na Kuchambuliwa Kitu Kimoja Kimoja Basi Hakuna Ambae Angekimaliza Lakini Vipo Katika Group Au Kauli Moja.......
Mf: Mungu Anaposema Nendeni Mkatafute Rizki Kwenye Mgongo Wa Ardhi.... Wewe Unataka Angesema:
Nendeni Mkalime,mkapande,mkavune,mmwagilie,mvune msage,mkaushe mpike Mfungue Maduka, mjiajiri n.k mnh! Hicho kitabu sijui kingekuwa kikubwa kwa kitu gani..

#Rakims
 
Back
Top Bottom