Ubani una uhusiano gani na mambo ya roho/imani?

Ubani una uhusiano gani na mambo ya roho/imani?

Kaunga

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Posts
12,529
Reaction score
13,502
Kufukiza ubani.

Kwa wakatoliki, sijui kuhusu makanisa mengine; ubani ni sehemu muhimu katika ibada ya misa.

Nimeona na kusikia pia, ubani hutumika katika kuyaita/kuyapunga majini.

Sasa swali langu hasa kwa wajuvi, ubani una issue gani na spirits? Iwe Holy Spirit au evil spirit?

Pasco
upo?
 
Kufukiza ubani.
Kwa wakatoliki, sijui kuhusu makanisa mengine; ubani ni sehemu muhimu ktk ibada ya misa.
Nimeona na kusikia pia, ubani hutumika ktk kuyaita/kuyapunga majini.
Sasa swali langu hasa kwa wajuvi, ubani una issue gani na spirits? Iwe Holy Spirit au evil spirit?
Pasco upo?
Mkuu Kaunga, mimi nipo sana tuu!. Graphology inanieleza hili swali umeliletwa kwa nia ya uchokozi fulaani hivi!, any way, mimi ni Mkatoliki niliyeisoma Biblia kivyangu vyangu, kuna mambo mengi dini zinayafanya ambayo sio, hili likiwa miongoni mwake!.

Sisi binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, yaani Mungu ndiye yumo ndani yatu kwa ile omnipresence yake, ila pia ametupa utashi kujua kuwa shetani pia yupo na tuko huru kumkaribisha!, ukimkaribisha shetani, Mungu anakuacha!. Nyumba za ibada, ni mahala patakatifu penye Mungu hivyo shetani hawezi kuwepo, lengo la ubani ni kumfukuza shetani na watumishi wake ambao ni mapepo!.

Shetani huyu na mapepo haya huletwa kwenye nyumba za ibada na waumini wenye nayo!.

Pasco.
 
Asante Pasco, sasa kama ubani hutumika kumfukuza shetani kwanini waganga na waita majini nao hutumia ubani?

Sijafanya uchokozi, ninajaribu tu kuielewa hii ritual yetu (mimi pia mkatoliki) na nilifukiri jamvini pia mapadre wapo wangetusaidia kuput more light to this.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kaunga, nipo sana tuu!. Graphology inanieleza hili swali umeliletwa kwa nia ya uchokozi fulaani hivi!, any way, mimi ni Mkatoliki niliyeisoma Biblia kivyangu vyangu, kuna mambo mengi dini zinayafanya ambayo sio, hili likiwa miongoni mwake!. Sisi binadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, yaani Mungu ndiye yumo ndani yatu kwa ile omnipresence yake, ila pia ametupa utashi kujua kuwa shetani yupo na tuko huru kumkaribisha!, ukimkaribisha shetani, Mungu anakuacha!. Nyumba za ibada, ni mahala patakatifu penye Mungu hivyo shetani hawezi kuwepo, lengo la ubani ni kumfukuza shetani na watumishi wake ambao ni mapepo!. Shetani huyu na mapepo haya huletwa na waumini wenye nayo!.
Pasco.

Pasco,

Kumbe weye ni Mkatoliko? Tuyaache hayo ya kwako ila nikuulize swali la kizushi tu, Umesema ati ubani unafukuza mapepo na mijishetwani inayoletwa/inayokuja na waumini, sasa mbona kulee kwa wenzetu nao huutumia ubani huo huo kuwavuta hao jamaa waje?

Mi nilikuwa muumini mkubwa wa mnajimu fulani maarufu sana ambaye keshatangulia mbele ya haki. Aliniuzia mpaka chombo maalumu cha kuufukizia huo ubani ili hao jamaa (Mapepo/majini) wanijie na kunifanyia kazi nilio taka. Weye unalijua hilo?

Pia, mbona kama Wakatoliki na hao rafiki zetu mnafanya mambo yakufanana saana kiimani? Mfano; Wote mna tAsbiHi, chetezo etc. Sisemi kama kuleta zogo lakini jibu lako la kufukiza ili kumvuta Roho Mtakatifu si kweli labda roho mtakavitu ndiye huja. Fikiri tena jibu jingine Pasco.
 
kaka ubani wengi huzani si utaratibu mzuri lakini si kweli,kiuhalisia ni kuwa kanisa katoliki hufuata mafundisho katika maandiko na mapokeo matakatifu.

Ukisoma biblia(sikumbuki ni kitabu gani) Mungi mwenyewe anauruhusu matumizi ya ubani ili kufukuza pepo, kama ilivyo alipoamuru watoto walambishwe chumvi iliuondoa uozo, utundika nyoka wa shaba enzi za musa nk .

Lakini hayo yote katoliki huchukulia kama ni mapokeo matakatifu na haioni ubaya katika kuyafuata, na ndio maana si kila misa hutumia bali ni kwa siku maalumu tu.
 
Asante Pasco, sasa kama ubani hutumika kumfukuza shetani kwanini waganga na waita majini nao hutumia ubani?

Sijafanya uchokozi, ninajaribu tu kuielewa hii ritual yetu (mimi pia mkatoliki) na nilifukiri jamvini pia mapadre wapo wangetusaidia kuput more light to this.

Kinachomater ni unanuizia nini wakati wa kufukiza huo ubani!. Ukifukuza wanakimbia, ukiita wanakuja!. Wanawake warembo wa ukanda wa pwani, hufukiza udi kwa lengo fulani, ukinuizia hilo lengo, linatimia!. Kwenye kufukiza, sio ubani tuu, hata bangi, ukinuizia uvute upate raha, ukivuta unapata raha kweli!, ukinuizia uvute usome kwa bidii, ukivuta, kitabu kinapanda kweli kweli!. Ukinuizia uvute ili kupandishia fulani, kupigana, kutolala, inakutuma vivyo hivyo!, au wale dada zetu wala kungu, hunuizia mambo fulani, na wanayafanya kweli kweli!.

Application ya ubani ni kama ilivyo sadaka yoyote, iwe ya kutoa, ya kuchinja au ya kuteketeza, ukitoa sadaka with well wishes, unapata ulichotaka, ila na wale wanaotumia sadaka kulaani wenzao, "albadir" hutumia hizo hizo sadaka au kisomo kumtuma shetani kufanya maangamizi!.

Akijiaminisha wewe ni wa Mungu, Mungu atakutumia kufanya yale yaliyo ya Kimungu, akijitoa kuwa wewe ni wa Kaisari, Kaisari atakutumia kufanya yaliyo ya Kaisari!, na ukijiaminisha wewe ni shetani, shetani atakutumia kufanya yaliyo ya kishetani!.
Pasco.
 
ibada zote zinazoshirikisha,uban,malashi,sanamu,kafara ya damu, ni chukizo mbele za MUNGU,kwa maana yeye ni roho wamwabuduo imewapasa kumwabudu ktk roho na kweli,si kwa kuona

Really?
Umesoma bíblia yako vizuri? Una maanisha agano la kale lote ni chukizo? Sadaka ya Abeli ilikuwa ni chukizo?
Soma pia kuhusu ubani ktk
Kutoka 30:1-9
Hesabu 7:13-17
Luka 1: 8-11
Matayo 2:11
Ufunuo 8:3-4
 
Kinachomater ni unanuizia nini wakati wa kufukiza huo ubani!. Ukifukuza wanakimbia, ukiita wanakuja!.
Pasco.

Luka 1:9,11
Zakaria (baba yake yohana mbatizaji) alichaguliwa kwa kura kama ilivyo desturi, kuingia hekaluni ili akafukize ubani. Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani.

Umeona kwa aya hizo, Angel (spirit) alikuja baada ya ubani kuchomwa. Na upande wa pili wa darkness pia ubani hutumika. Nafikiri ni sahihi kusema ubani ni mvuto wa spirits, iwe light au dark spirits.

Cc MziziMkavu
 
Kaunga uko deep!.
Dini zilitakiwa kuwasisitizia waumini wake kuyasoma wenyewe maandiko matakatifu, watafunuliwa na kuijua kweli, hivyo wataweza kuepuka, kwenda kwenye upotevu!.

Light spirits ndio viumbe gani hao, Kaunga?
 
Ni kweli usemayo biblia imeongelea sana matumizi ya ubani.
Yaweza kuwa sahihi kuwa ni mvuto ws spirits iwe nzuri au mbaya
 
Last edited by a moderator:
Kaunga uko deep!.
Dini zilitakiwa kuwasisitizia waumini wake kuyasoma wenyewe maandiko matakatifu, watafunuliwa na kuijua kweli, hivyo wataweza kuepuka, kwenda kwenye upotevu!.

Pasco

Pasco kwanini umesema Kaunga yupo deep sana, kwani kuna kitu ambacho hakitakiw sisi kukijua??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom