Ubakaji unaongezeka kwasababu ya umasikini. Watu wanatafuta urahisi

G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
2,077
5,269
Wabakaji wa siku hizi siyo kwamba wanasukumwa na hamu ya mapenzi. Hapana.

Sababu kubwa ni kutafuta utajiri kwa njia ya mkato. "Kutembea" na bikra ni moja ya masharti yanayotolewa na waganga wa kienyeji. Ndiyo maana wanaobakwa ni watoto wadogo wa miaka chini ya 10.

Badala ya kuendelea kutengeneza sheria kali za kuwahasi wabakaji, kuwaua ama kuwafunga miaka mingi, ni vema kudhibiti chanzo cha unyama huu kwa kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania.
 
Tatizo siyo umaskini bali tatizo ni imani potofu. Siku hizi ''wajanja'' wanaotumia propaganda za uchawi, miujiza na uganga wameachiwa wawalaghai wananchi kwa kuwalisha imani za uongo. Ukiingia YouTube kuna hizi online TV zinazofundisha imani potofu na serikali inawaachia tu.
 
Kweli kabisa tatizo kuu ni watu kukosa maarifa
 
Back
Top Bottom