Ubaguzi wa rangi nchini Marekani na matumizi ya nguvu ya polisi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
2F20DE9C-F7BB-407C-80D7-57BDCF7D5CB4.jpeg

George Floyd
Mauaji ya Mmarekani mwenye asili ya Afrika GeorgeFloyd yamesababisha wimbi kubwa la maandamanondani nan je ya Marekani, watu wa rangi tofautiwakiungaika pamoja kupigania haki zao. Kifo hichopia kimeibua maswali mengi kwa watu wa ngazimbalimbali, kuangalia kwa makini maisha yao namustakabali wao na kizazi chao katika siku za baadaye. George Floyd alifariki baada ya polisi mzungukumkandamiza kwa goti shingoni, akiwa amelala chinihuku amefungwa pingu, kwa zaidi ya dakika nane.

Lakini historia inaonyesha kuwa mauaji ya George Floyd, Mmarekani mwenye asili ya Afrika si yakwanza kutokea nchini Marekani. Mwanaharakatimaarufu wa nchini humo Hayati Martin Luther King, Jr , pia aliuawa katika harakati zake za kupigania hakiza watu weusi, ama wakati huo wakijulikana kamaWanegro. Martin Luther King Jr aliwaongoza Waamerika Weusi kupinga ubaguzi wa rangiuliokuwepo nchini Marekani mpaka miaka ya 1960. Katika mapambano hayo alieleza ya kuwa kila mtuamepewa heshima yake na Mungu, hivyo sheria zanchi na serikali zinazovunja heshima hiyo si za haki. Aliongoza maandamano kadhaa lakini yaliyofanyikakwa njia za amani, ingawa waandamanaji walipigwa nakukamatwa, lakini hawakufanya vurugu. Waliingiakwenye maeneo ambayo awali yalikuwa yametengwakwa ajili ya watu weuoe tu, ikiwemo shule, vyombovya usafiri na hata hoteli, wakasubiri mpaka polisiwalipoitwa na kuja kuwakamata. Baada ya miakakadhaa mapambano hayo dhidi ya ubaguzi wa rangiyaliyofanyika kwa amani yalishinda, na ubaguzi warangi ukapigwa marufuku mwaka 1964. Hata hivyo, Martin Luther King Jr aliuawa mwaka 1968 kwakupigwa risasi na mtu aliyetetea ubaguzi wa rangi.

Mwaka 2014, aliuawa Mmarekani mweusi Michael Brown katika kitongoji cha St. Louis huko Ferguson, Missouri. Mauaji yake yalizua maandamanoyaliyopewa jina la ‘Black Lives Matter’ ama ‘Maishaya Weusi Yanastahili’. Mwaka 2015, maandamanoyalitokea tena nchini Marekani kutokana na mauaji yaMmarekani mwenye asili ya Afrika, ambaye alikutwana mauti alipokuwa amezuiliwa na polisi katika mji waBaltimore, jimbo la Maryland.

A3846E57-1652-448A-978E-1DF39B455705.jpeg

Freddie Gary
Kijana huyo, Freddie Gray, mwenye umri wa miaka 25, alifariki kutokana nakujeruhiwa kwenye uti wa mgongo wakati akiwa chiniya uangalizi wa polisi.

Itakumbukwa kuwa, miaka sita iliyopita, Mmarekanimwingine mweusi kwa jina la Eric Garner alipotezamaisha mikononi mwa polisi mjini New York kwa njiaya kukosa pumzi na kubanwa kifua huku akipiga keleleakisema "siwezi kupumua." Aidha miaka kadhaailiyopita, Michael Brown, Walter Scott, Tamir Rice naWamarekani wengi weusi pia walipoteza maishakutokana na vitendo vya ukatili wa polisi wa Marekani.

Mauaji ya George Floyd yameibua wimbi la maandamano, Wamarekani weusi kwa weupe, nawenye asili za nchi mbalimbali wameungana kwapamoja kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi na piaukatili dhidi ya polisi.

Polisi, ambao tunatarajia kuwa wangekuwa msari wambele kulinda na kutetea uhai wa binadamu, ndiowanahusika kwa sehemu kubwa kwa matumizi yanguvu na mauaji ya Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Haya yote yanapotokea, watu wanajiuliza, serikali yaMarekani inachukua hatua gani? Baada ya vurugukutokea kufuatia mauaji ya George Floyd, rais waMarekani Donald Trump aliwaita waandamanaji kuwani genge la wahuni, na kutishia kupeleka maelfu yawanajeshi kuwadhibiti waandamanaji katika mijimbalimbali nchini humo. Hatua hiyo ilikosolewa vikalina jamii ya kimataifa, huku mgombea urais katikauchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu Joe Biden, akisema Trump anatumia jeshi la Marekani, risasi zamipira na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya watuwake, na kwamba ni lazima adhibitiwe.

Umefika wakati sasa wa jamii ya kimataifa kuunganakatika kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi, si nchiniMarekani tu, bali katika nchi zote. Ni wakati sasa wakuacha kuangalia rangi ya ngozi ya mtu, na badalayake kutanguliza utu, na pia ni wakati sasa wakukumbuka kuwa, sisi sote ni binadamu, haijalishirangi, dini ama kabila.
 
Back
Top Bottom