Wamarekani wenye asili ya Afrika bado wakabiliwa na ubaguzi wa rangi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1683793705140.png
Hivi karibuni kijana mmoja Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliuawa na kijana mzungu kwenye treni ya chini ya ardhi mjini New York, Marekani, lakini mhusika wa mauaji hayo aliachiliwa huru baada ya kuhojiwa na polisi kwa muda mfupi tu. Ikiwa ni miaka mitatu tangu George Floyd auawe kwa kukosa pumzi baada ya kukandamizwa kwa magoti na polisi mzungu, wito wa “Black Lives Matter” umekuwa dhaifu, na watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani bado wanakabiliwa na ubaguzi mbaya wa rangi.

Kijana aliyeuawa hivi karibuni anaitwa Jordan Neely, ni mtu asiye na makazi ambaye alikuwa anajikimu kimaisha kwa kumuiga Michael Jackson mitaani. Kwa mujibu wa mashuhuda katika eneo la tukio, mara tu Neely alipoingia kwenye subway, alianza kupiga kelele, “Inatosha, nina njaa!”, mpaka akakabwa shingoni na Daniel Penney, aliyekuwa askri wa jeshi la Marekani. Baada Penney kuachiliwa, watu wengi walikusanyika na kuandamana, wakitaka “muuaji akamatwe” na “haki itendeke”.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Viongozi wa Haki za Kiraia na Haki za Binadamu wa Marekani Maya Wiley, ambaye pia ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika, alisema kwenye mitandao ya kijamii: “Neely angekuwa hai, Neely angekuwa na nyumba, Neely angekuwa na chakula cha kutosha, Neely angekuwa na kile anachohitaji!”

“Siwezi kupumua!” Mwandamanaji mmoja aliyekimbilia kwenye kituo cha treni ya chini ya ardhi na kusimamisha treni alipiga kelele kwa polisi. Kauli hiyo ilitokana na tukio la kuuawa kwa Floyd, ambalo lilisababisha maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi kote nchini Marekani. Hata hivyo, sasa miaka mitatu imepita, matukio kama hayo hayajatoweka, lakini yameongezeka zaidi. Sababu ni kwamba dhuluma dhidi ya Waafrika katika nyanja mbalimbali nchini Marekani imefanya ubaguzi wa rangi kuwa tatizo lisilotatuliwa.

Katika sehemu ya mashariki mjini Detroit, Marekani, kufuatia picha za satelaiti, unaweza kuona ukuta unaopita kaskazini mpaka kusini, ambao unatenganisha eneo la “watu weupe” na “watu weusi”. Ripoti ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu ya Wamarekani wenye asili ya Afrika iliyotolewa hivi karibuni na Shirikisho la Miji la Marekani ilieleza kwamba, Wamarekani wenye asili ya Afrika wana “asilimia 73.9 tu ya fursa za wazungu”, na hawana haki sawa na watu weupe katika kupata utajiri, afya, elimu na mambo ya kisiasa. Data za uchunguzi kuhusu hali ya kifedha ya watumiaji nchini Marekani zinaonyesha kuwa, wastani wa mali za familia ya Wamarekani weupe ni mara nane kuliko familia ya Wamarekani weusi. Wastani wa mali za familia ya watu weupe ni dola 983,400 za kimarekani, huku wastani wa mali za familia ya watu weusi ukiwa dola 142,500 tu za kimarekani.

Suala la ardhi ni chanzo kingine muhimu cha umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Ripoti iliyotolewa tarehe 3 Mei na Shirika la Habari la Uingereza Reuters inasema, wakulima wenye asili ya Afrika nchini Marekani walipoteza takriban ardhi yenye thamani ya dola bilioni 326 za kimarekani katika karne ya 20 kutokana na sera za ubaguzi wa rangi. Kuanzia mwaka 1922 hadi 1997, mashamba ya kilimo ya wakulima weusi katika majimbo 17 nchini Marekani yalipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na “vitendo vya kimabavu vilivyoungwa mkono na serikali”, pamoja na sera ya ubaguzi wa rangi katika utoaji wa mikopo, na hatua ya kuwalazimisha watu weusi kuuza mashamba yao.

Takwimu za Sensa iliyofanywa na Wizara ya Kilimo ya Marekani zinaonesha kuwa, mwaka 1910, wakulima wenye asili ya Afrika nchini humo walikuwa wanamiliki mashamba zaidi ya ekari milioni 16, ikiwa ni asilimia 14 ya mashamba yote ya kilimo nchini Marekani. Lakini hadi kufikia mwaka 2017, wakulima weusi walikuwa wanamiliki mashamba ekari milioni 4.7 tu. Hivi leo ni asilimia 1 tu ya watu weusi wanaomiliki mashamba nchini Marekani, ambao wanamiliki asilimia 0.1 tu ya mashamba ya kilimo ya nchi hiyo.

Ubaguzi wa rangi nchini Marekani umekuwa tatizo sugu lisilotatuliwa, na kuifanya Marekani ambayo inajifanya kuhimiza haki na usawa duniani, kuonekana inafanya mzaha.
 
... wamarekani weusi wamejaa kote serikalini huko Marekani hadi makamu wa rais mweusi yupo including majenerali waliojazana Pentagon na kwingineko! Nitajie mweusi japo mmoja tu aliyewahi kuwa japo rais wa DARUSO ya huko China!
 
Hawa jamaa ni wachina na wanafanya kazi under CCP kueneza propaganda za CCP.

Kazi yao kubwa ni kuipamba China na kuichafua Marekani.

Wapo wawili TTP na Huyu Idleo.

Majuzi tu hapa Chinese diplomat amekumbwa na kashfa ya Rushwa huko Canada ya kumtaget law maker na familia yake ili Waunde sheria inayowafeva CCP wakastukiwa na kuwa expelled from Canada.

Lakini hii habari hauwezi kuisikia japo na ukubwa wake wote japokuwa inahusu taifa Lao la China
 
H
Hivi karibuni kijana mmoja Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliuawa na kijana mzungu kwenye treni ya chini ya ardhi mjini New York, Marekani, lakini mhusika wa mauaji hayo aliachiliwa huru baada ya kuhojiwa na polisi kwa muda mfupi tu. Ikiwa ni miaka mitatu tangu George Floyd auawe kwa kukosa pumzi baada ya kukandamizwa kwa magoti na polisi mzungu, wito wa “Black Lives Matter” umekuwa dhaifu, na watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani bado wanakabiliwa na ubaguzi mbaya wa rangi.

Kijana aliyeuawa hivi karibuni anaitwa Jordan Neely, ni mtu asiye na makazi ambaye alikuwa anajikimu kimaisha kwa kumuiga Michael Jackson mitaani. Kwa mujibu wa mashuhuda katika eneo la tukio, mara tu Neely alipoingia kwenye subway, alianza kupiga kelele, “Inatosha, nina njaa!”, mpaka akakabwa shingoni na Daniel Penney, aliyekuwa askri wa jeshi la Marekani. Baada Penney kuachiliwa, watu wengi walikusanyika na kuandamana, wakitaka “muuaji akamatwe” na “haki itendeke”.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Viongozi wa Haki za Kiraia na Haki za Binadamu wa Marekani Maya Wiley, ambaye pia ni Mmarekani mwenye asili ya Afrika, alisema kwenye mitandao ya kijamii: “Neely angekuwa hai, Neely angekuwa na nyumba, Neely angekuwa na chakula cha kutosha, Neely angekuwa na kile anachohitaji!”

“Siwezi kupumua!” Mwandamanaji mmoja aliyekimbilia kwenye kituo cha treni ya chini ya ardhi na kusimamisha treni alipiga kelele kwa polisi. Kauli hiyo ilitokana na tukio la kuuawa kwa Floyd, ambalo lilisababisha maandamano makubwa dhidi ya ubaguzi wa rangi kote nchini Marekani. Hata hivyo, sasa miaka mitatu imepita, matukio kama hayo hayajatoweka, lakini yameongezeka zaidi. Sababu ni kwamba dhuluma dhidi ya Waafrika katika nyanja mbalimbali nchini Marekani imefanya ubaguzi wa rangi kuwa tatizo lisilotatuliwa.

Katika sehemu ya mashariki mjini Detroit, Marekani, kufuatia picha za satelaiti, unaweza kuona ukuta unaopita kaskazini mpaka kusini, ambao unatenganisha eneo la “watu weupe” na “watu weusi”. Ripoti ya kila mwaka kuhusu hali ya haki za binadamu ya Wamarekani wenye asili ya Afrika iliyotolewa hivi karibuni na Shirikisho la Miji la Marekani ilieleza kwamba, Wamarekani wenye asili ya Afrika wana “asilimia 73.9 tu ya fursa za wazungu”, na hawana haki sawa na watu weupe katika kupata utajiri, afya, elimu na mambo ya kisiasa. Data za uchunguzi kuhusu hali ya kifedha ya watumiaji nchini Marekani zinaonyesha kuwa, wastani wa mali za familia ya Wamarekani weupe ni mara nane kuliko familia ya Wamarekani weusi. Wastani wa mali za familia ya watu weupe ni dola 983,400 za kimarekani, huku wastani wa mali za familia ya watu weusi ukiwa dola 142,500 tu za kimarekani.

Suala la ardhi ni chanzo kingine muhimu cha umaskini wa Wamarekani wenye asili ya Afrika. Ripoti iliyotolewa tarehe 3 Mei na Shirika la Habari la Uingereza Reuters inasema, wakulima wenye asili ya Afrika nchini Marekani walipoteza takriban ardhi yenye thamani ya dola bilioni 326 za kimarekani katika karne ya 20 kutokana na sera za ubaguzi wa rangi. Kuanzia mwaka 1922 hadi 1997, mashamba ya kilimo ya wakulima weusi katika majimbo 17 nchini Marekani yalipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na “vitendo vya kimabavu vilivyoungwa mkono na serikali”, pamoja na sera ya ubaguzi wa rangi katika utoaji wa mikopo, na hatua ya kuwalazimisha watu weusi kuuza mashamba yao.

Takwimu za Sensa iliyofanywa na Wizara ya Kilimo ya Marekani zinaonesha kuwa, mwaka 1910, wakulima wenye asili ya Afrika nchini humo walikuwa wanamiliki mashamba zaidi ya ekari milioni 16, ikiwa ni asilimia 14 ya mashamba yote ya kilimo nchini Marekani. Lakini hadi kufikia mwaka 2017, wakulima weusi walikuwa wanamiliki mashamba ekari milioni 4.7 tu. Hivi leo ni asilimia 1 tu ya watu weusi wanaomiliki mashamba nchini Marekani, ambao wanamiliki asilimia 0.1 tu ya mashamba ya kilimo ya nchi hiyo.

Ubaguzi wa rangi nchini Marekani umekuwa tatizo sugu lisilotatuliwa, na kuifanya Marekani ambayo inajifanya kuhimiza haki na usawa duniani, kuonekana inafanya mzaha.
Hawa ndio huwa wanatufundisha masuala ya haki za binadamu.

Kweli ukistaajabu ya Mussa.
 
Mimi nimewahi kuishi Marekani miaka ya nyuma hivyo ninafahamu watu na maisha ya huko vizuri sana.

Hao Black Americans ni watu wenye asili ya ukorofi sana na hata mimi kabla sijaenda huko nilikuwa nafikiria hivyo hivyo kwamba wanaonewa kumbe waliathiriwa sana na ile fikra ya utumwa inayowafanya wawe na Inferiority Complex mbele ya wazungu.

Sasa ktk kupambana na hiyo Inferiority Complex wanakuwa na Violent Attitude, ili kujaribu kuishinda hiyo Inferiority Complex, hasa kwa watu weupe.

Nilishangaa mbona wazungu hawana shida na sisi watu tunaotoka Afrika na kwenda Marekani..?? Tena utakuta wanakushauri usirudi Afrika ila ukae tu Marekani utafute maisha kwa sababu wanaamini nchi yao ni nzuri sana na ina fursa nyingi kwa mtu mwenye bidii ya kusaka maisha mazuri.

Kuna African Americans wengine hata hawataki kabisa kuongea na sisi tuliotoka Afrika kwa madai kwamba eti machifu wetu ndio waliwauza mababu zao kwa wazungu enzi za biashara haramu ya utumwa hivyo wana chuki isiyoisha karne na karne..

Marekani ndio nchi pekee duniani, nje ya Afrika, ambapo mtu mweusi anaweza akathaminiwa na kupewa hata madaraka makubwa kabisa tofauti na mataifa mengine kama China, India au Russia ambapo hata choo cha stendi ya mabasi tu mtu mweusi hawezi kuruhusiwa kuajiriwa kufanyapo hata usafi.

Lakini pia tusisahau kwamba ubaguzi uko popote duniani hata hapa tumeona jinsi wafuasi wa vyama vya upinzani hasa Chadema walivyo fanywa hadi hata wengine hadi leo haijulikani walipo, huo nao ni ubaguzi tu na sio lazima ufanywe na mzungu ndio uwe ubaguzi. Tuache unafiki.
 
Back
Top Bottom