Ubaguzi wa rangi waunda sera ya kigeni ya Marekani kuhusu Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
微信图片_20220927083049.jpg

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi ilitoa ripoti ya tathmini ya jinsi Marekani inavyotekeleza Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi wa Rangi, ikisema uhalifu na kauli za chuki nchini Marekani vimeongezeka kidhahiri katika miaka kadhaa iliyopita, na watu wasio wazungu na walio wachache wanaendelea kukabiliwa na ubaguzi katika sekta mbalimbali. Matokeo ya kura za maoni ya Kituo cha Utafiti cha Pew pia yanathibitisha hali hiyo - 65% ya watu wazima weusi nchini Marekani wanaamini kwamba licha ya kuongezeka kwa ufuatiliaji mkubwa juu ya kukosekana kwa usawa wa rangi katika jamii ya Marerani, maisha yao bado hayajaboreka.

Baada ya maandamano yaliyochochewa na mauaji ya mmarekani mweusi George Floyd miaka miwili iliyopita, watu walidhani maandamano hayo yatachochea mabadiliko katika maisha ya weusi. Lakini kuna msemo wa kichina kwamba “barafu haiwezi kuganda kwa futi tatu ndani ya siku moja”. Miaka ya kuepuka historia ya biashara haramu ya binadamu na kupuuza tatizo la sasa la ubaguzi wa rangi, vimefanya ubaguzi kuwa ugonjwa sugu katika jamii ya Marekani.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa uliadhimisho miaka 15 ya "Siku ya Kimataifa ya Kutokomezwa kwa Biashara Haramu ya Watumwa Weusi ", ambayo kwa mara nyingine tena ilitoa fursa kwa jumuiya ya kimataifa kutafakari masuala yanayosababishwa na historia hiyo na kuwakumbusha watu kuwa macho dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Kwa zaidi ya miaka 400 biashara haramu ya utumwa ikiwa ni sura ya giza na uoevu zaidi katika historia ya binadamu, imeleta maumivu makubwa kwa watu wa Afrika. Waafrika walifanywa watumwa katika ardhi yao, uhuru na haki na hata mamlaka yao viliporwa na wakoloni wa Magharibi. Walilazimishwa kufanya kazi, na utajiri waliounda ukapelekwa katika nchi za wakoloni. Lakini hadi leo hii, ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wa asili ya Afrika huko Marekani na nchi nyingine za Magharibi haujakoma, na kesi ya Floyd ambayo Wamarekani wenye asili ya Afrika walidhani ingechochea "mabadiliko ya kihistoria" ni mwuonekano mwingine wa utumwa wa kihistoria - umegeuka kuwa vurugu dhidi ya watu wa rangi tofauti. Mbali na Marekani, mabaki ya kihistoria ya utumwa pia yamemejitokeza katika sera ya kisasa ya Marekani kuhusu Afrika.

Nchi na watu wowote wana haki e ya kuchagua na kujua nini cha kufanya kwa manufaa yao wenyewe, na nchi za Afrika hazina tofauti. Lakini kama alivyosema profesa wa uhusiano wa kimataifa wa Kenya Macharia Munene katika mahojiano ya hivi majuzi, tangu mwanzoni mwa karne ya 20 hadi leo, Marekani, Uingereza na Ufaransa wamekuwa wanaamua kila wakati kile kinachoitwa kizuri kwa Waafrika, au nini Waafrika wanapaswa kufikiria, bila kujali Waafrika wenyewe wanafikiria nini. Leo, iwe ni kuzilazimisha nchi za Afrika "kuchagua upande" katika mgogoro kati ya Russia na Ukraine, au hata kuzishurutisha kwa vikwazo, au kuchafua na kuupaka matope ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, yote hayo yanaonyesha dharau ya Marekani dhidi ya uhuru wa nchi za Afrika.

Mwezi uliopita tu, wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken barani Afrika, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini Naledi Pandor alikosoa hadharani tabia ya nchi za Magharibi ya "uonevu" dhidi ya bara la Afrika katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, akizishutumu nchi za Magharibi kwa unafiki na uingiliaji wa kisiasa. "Afrika Kusini haipendi kulazimishwa 'kwa njia moja au nyingine' na haitaki kulazimishwa kuchagua upande."

Ingawa historia ya biashara ya utumwa imeisha, ubaguzi na upendeleo bado upo nchini Marekani na katika maingiliano yake na nchi za Afrika. Serikali ya Marekani inapaswa kuelewa kwamba maelewano na usawa kwa wote sio tu ni mahitaji ya ndani, bali pia ni msingi wa maendeleo ya uhusiano kati ya Marekani na Afrika.
 

Attachments

  • VCG111395952117.jpg
    VCG111395952117.jpg
    32.9 KB · Views: 11
Back
Top Bottom