Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Je, leo hii katika vyama vingi tuna umoja wa kupigana vita ya kuwa hai? Unafikiri vyama vingi vimejenga umoja wa Watanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujenzi wa taifa kuliko ilivyokuwa wakati wa chama kimoja? Kwa maneno mengine, je Watanzania ni wamoja zaidi sasa hivi kuliko wakati wa chama kimoja?
Ni kuturudisha nyuma nusu karme mtu kushupaza mishipa kichwani kujadili maisha ya mwaka 1960 kwa kizazi cha leo, kwani utabaki kuumia nyongo wakati mtazamo, fikra na mazingira ya leo na ya miaka ile inatofautiana mno. Kwa wakati ule kufikiri na kufanya kama walivyofanya ilikubalika na hakikuwa kitu cha kushangaza tofauti na kizazi cha leo.
Wapembuzi yakinifu wanachofanya ni kusoma yale yaliyofanyika wakati ule, kuyachuja na kuchukua yale ambayo katika kizazi cha leo yana nafasi. Kuendelea sijui kumjadili Nyerere, Kleruu na wengine na kuchukulia hoja kwamba wao ndio waliosababisha matatizo tuliyo nayo leo ni fikra finyu sana. Ndio maana nchi ye yote ile ina baraza la wawakilishi kama sisi tulivyo na bunge ambalo hupitia miswada mbalimbali mipya na kuibadilisha au kuongeza vipengere vipya kutokana na mabadiliko ya wakati kuendana na kizazi cha muda tulio nao. Tungekuwa na mfumo dume kama mawe yasiyobadilika na kubaki kama yalivyo hatungehitaji bunge liwepo muda wote. Nadhani mmenielewa.
Tunahitaji kujadili mambo yetu ya wakati huu wa sasa yanavyoenda na kizazi cha leo tunataka nini, na tunaweza bado kudonoa mazuri ya wakati uliopita ambayo bado yana mshiko, hayajachuja, kinyume cha hapo ni sawa na kumshambulia babako kwa nini alikuzoesha kunywa mbege ulipokuwa mdogo badala ya soda au bia ambayo unaoina inakufaa sasa wakati nafasi na uwezo unakuruhusu, tatizo hapo hupimi nafasi na uwezo wa baba alipokuwa anaishi bado kijijini, una unakuwa na mtazamo wa leo unapoishi mjini na hata vijijini ambako leo wanaweza kutumia simu za mkononi hata wanapochunga mbuzi.