Mfumo wa chama kimoja ni sumu ya muda mrefu ya demokrasia kulinganisha na Ufalme au Jeshi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,267
Ni rahisi zaidi nchi ya kifalme au kutoka katika ufalme kuingia katika demokrasia imara ndani ya muda mfupi kuliko kutoka katika chama kimoja kuingia katika demokrasia.

Ukiangalia katika historia mataifa mengi ya kifalme hata pale raia wachache walipoamua kuingia katika demokrasia walichukua muda mfupi zaidi kupata demokrasia kamili. Hiyo ni kwa mataifa ya kijeshi pia kama Korea Kusin.

Kwa upande mwingine mataifa yaliyoingia katika mfumo wa chama kimoja imekuwa ni vigumu sana kuingia katika demokrasia kamili hata pale raia wengi wanapotaka hivyo. Mifano ni mingi kuanzia China, Vietnam, Korea Kaskazini, Urusi, mataifa ya zamani ya kisovieti, Cuba, Mexico, na Mataifa mengi ya Africa.

Mataifa yote yaliowahi kuingia katika ndoano ya chama kimoja haijawa jambo rahisi kuingia katika demokrasia halisi.
 
Ni kweli, wakati fulani ili kuvunja mfumo wa chama kimoja unahitaji coup de tat kisha ndio uanzishwe mfumo mpya huku chama tawala cha zamani kilipigwa marufuku kabisa.
 
Back
Top Bottom