Uamuzi wa Kuingia Chama Kimoja: Maelezo ya Kleruu na Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi wa Kuingia Chama Kimoja: Maelezo ya Kleruu na Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 7, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  chamakimoja.png
  Tunapoendelea kutafakari miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania bara hatuna budi kupitia mojawapo ya kurasa nyeti sana za taifa letu - uamuzi wa kuondokana na mfumo wa vyama vingi na kuwa rasmi nchi ya chama kimoja. Uamuzi huu kwa wengine ndio uliomthibitisha Nyerere kuwa ni dikteta kwani "alifuta vyama vingi". Bahati mbaya sana watu wenye kuelezea uamuzi huu wanaangalia kwa mwanga ambao ukiufikiria sana ni vigumu sana kuuelewa kuwa demokrasia ni "vyama vingi" kwamba nje ya vyama vingi hakuna demokrasia. Hili kwa haraka linaonekana ni kweli.

  Na kutokana na hilo wapo wanaoamini kuwa vyama vingi vinaharakisha maendeleo na ya kuwa kama tungeendelea kuwa na vyama vingi labda tungepiga hatua za haraka za maendeleo. Kutokana na hili wapo wanaoshangaa kwanini wananchi walipoulizwa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama tuingie kwenye vyama vingi waliopata kutoa mawazo yao asilimia 80 walitaka kuwa na chama kimoja. Matokeo ya chaguzi mbalimbali bado yameonesha kuaminiwa kwa chama kimoja kwa muda mrefu kiasi kwamba sasa tunajua kabisa kuwa CCM kama kweli ingetaka kutawala vizuri na kuliongoza taifa kwenye maendeleo ingeweza kwani wananchi waliamini kweli na wapo ambao waliamini kuwa demokrasia iliyokuwemo ndani ya chama kimoja ilikuwa na nguvu zaidi kuliko demokrasia ya vyama vingi.

  Kuelewa hiyo kauli yangu hapo juu hatuna budi kurudi kwa miongoni mwa wanadharia wa kwanza wa CCM na mmoja wa viongozi walioamini kabisa Ujamaa Dr. Will Kleruu. Wengi wanamkumbuka zaidi kutokana na kifo chake - aliuawa kule Iringa na risasi ya Mwamindi na labda wimbo wa kwanza wa kumsifia kiongozi aliyependwa Tanzania ukiondoa Nyerere ulitungwa na Mbaraka Mwinshehe ule wa kumuaga Dr. Kleruu - "Dr. Kleruu ukalale pema kiongozi wetu shujaa, mwanamapinduzi".

  Kwanini tuliingia kwenye chama kimoja? Je ni kweli Nyerere aliamua tu kufuta vyama vingine? Je, kulikuwa na hoja gani zilizotolewa za kulipeleka taifa kwenye chama kimoja na je hoja hizo zingewa kupingwa vipi? Hapa basi, Dr. Kleruu ameandika kitu ambacho tunaweza kuita ni propaganda za TANU za kuhalalisha chama kimoja kwa kutumia hoja za kiakili (rational arguments). Je hoja zake nani angeweza kuzipinga wakati ule? Je leo ukizisoma hoja hizi ni ipi unaweza kuipangua na kusema hapa Dr. Kleruu alikosea?

  Pamoja na kijitabu cha Dr. Kleruu cha "Serikali ya Chama Kimoja" nimeambatanisha vile vile maelekezo ya Rais Nyerere kwa Tume ambayo ilitakiwa kubuni mfumo wa demokrasia ya chama kimoja iwe vipi. Ndani ya maelezo hayo kuna mambo ambayo aliyasimamia kama taifa kwamba bila kujali tuko kwenye chama kimoja au vingi kuna mambo ambayo ni lazima yawepo katika Tanzania - nina uhakika ukiyasoma utasisimka kwani ndiyo yaliyotufanya Watanzania tuwe Watanzania (rejea Utetezi wangu wa Tanzania sehemu zote mbili). Na kama burudani kwa wazee wenzangu na vijana ambao hawajahi kusikia wimbo huu, ninawakumbushia wimbo wa Mbaraka Mwinshehe wa buriani ya Dr. Kleruu.

  SWALI: Je, ni kweli demokrasia inajengwa peke yake kwa vyama vingi? Je, yawezekana kubuni mtindo wa kuwa na demokrasia ndani ya Chama kimoja? Faida na hasara za mifumo yote miwili ni nini hasa? Dr. Kleruu anajaribu kujibu. Kwa upande wetu leo hii tunatakiwa kujiuliza je Demokrasia ya vyama vingi imefanya yale ambayo tuliambiwa itaweza kufanya? Vietnam na China ni nchi zenye mfumo wa chama kimoja kwanini zinapiga hatua ya haraka ya maendeleo kuliko sisi?

  Do Enjoy!!

  MMM


   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Thanks Mwanakijiji, i appreciate your efforts to make us informed on important issues....
   
 3. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 581
  Trophy Points: 280
  dr kleruu kiukweli mi sina shida na maandiko ya **** kama huyu, na bora aliuwawa maana alikuwa dikteta haswa, viva mwamwindi hata kama hukutungiwa wimbo wewe kwetu sisi wahehe unabaki kuwa shujaa daima, tunafahamu ulipotea kama mwanga wajua usiku lakini wanamapinduzi wa kihehe daima utakuwa mfano wa kuigwa kwetu, japo historia yako hawataki iandikwe lakini itadumu milele, hakika uliwakilisha na kuuonyesha ushujaa wa mhehe na kufanya iringa iheshimike maana baada ya hapo hakuna hata mtu mmja aliyeletwa akfanya uonezi kama wa mshenzi kleruu. nakumbuka harakati za wahehe walipokua wakipinga chuo kile kubadilishwa jina yaani kutoka iringa tearchers college hadi kleruu. Niliongea na dokta magoti aliyekuwa mkuu wa chuo wakati huo akaniambia ilikuwa ni shida sana kutembea na magari yaliyoandikwa kleruu maana yalikuwa yanapigwa mawe kwasababu ya jina hilo. kizazi cha sasa tunajipanga kuhakikisha kuwa kile chuo kinafutwa jina lile kwani ni fedheha kwetu kwa dr kleruu kuendelea kuenziwa kwenye ardhi yetu. unajua daima wahehe hatupendi kudhalauliwa kiasi hiki na nimekereka mno na hii post yako mwanakijiji, eti umeweka na wimbo wa kumuenzi mshenzi kleruu, huu ni upuuzi na ni kutuabisha watu wa iringa, hafai hata kidogo kupewa sifa yoyote kichaa huyu. wewe na hao wazee wenzio bora mngeitana bar na kuusikiliza huo wimbo. na ingekuwa amri ya watu wa iringa mwili wa huyu mkono wa chuma wangepewa mbwa wale kuliko kuimbiwa buriani.EHE! MUNGU KAMA KWELI KUNA MOTO BASI HUYU SHETANI KLERUU MFANYE KUWA KUNI NA MAJIVU YAKE MPE LUCIFERI ATUMIE KAMA KIUNGO KWENYE MBOGA ZAKE. mwamwindi fikra zako za ukombozi zidumu daima nadaima hata na vizazi vya sasa visimuliwe ili navyo vifanye maamuzi magumu kama haya.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  To me its rather being misinformed and being brainwashed into thinking that nyerere and his team were godly, saints or rather Angels which is quite the opposite of what they were and what they presented, absolute misery and calamity, they were destructive tyrannical authoritarians or simply dictators who drained the country and left it in deep poverty with scarcity of all basic necessities in manners never seen before their coming and never seen after they were gone.

  For most, who were lucky enough for not being there and have never experienced the hard times we went thru during their reign will always be misinformed by the few who were in the or left overs of those who were in the most inner circles of the domineering clan who were mostly the chosen ones from one group of the population. The said group is putting all efforts into creating a Saint who never was.
   
 5. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Je ni jadi yao kulewa madaraka? ukiangalia approach iliyopelekea yeye Kleruu kuuwawa naona kuna ka ukweli fulani hapo juu penye red, hebu angalia msemo wao kuwa CCM itatawala daima inamaanisha nini? Usemi wa kuwa watanzania hata kama ni kula majani lazima Ndege ya rais itanunuliwa na kweli wakanunua kwa lugha hizi hizi za kifedhuli, Wapi Philipo Marmo na kejeli zake, Wapi leo Mramba

  Nafikiri MMKJ fikra za Nyerere na Kleruu zilikuwa moja ila approach zilitofautiana sana, nikimaanisha hawa viongozi wa sasa kifikra ni type ya Kleruu na sio Nyerere type.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Are we not in hard times now after more than 25 years since Nyerere's reign ended? Hakuna umeme, hakuna maji, wizi unafanywa na watu wakubwa kabisa tuliowaamini kwa kuwapa madaraka ndio maana kuna EPA, radar, Dowans na mengine mengi ambayo wakati muafaka utakapofika tutayajua?
  Unafahamu 10 years down the road, majadiliano yatakuwa sio kwa Nyerere, bali ni viongozi waliomfuata wamefanya nini? Well, labda mambo yamebadilika kwa wale wapiga domu ambao sasa wanaweza kuingia kwenye ndege kubwa kama delegation ya Tanzania kusaka wawekezaji huko nje...guess what!! Hawana hata biashara ya kuuza peremende ila wanatafuta wawekezaji kutoka ng'ambo....nani kasema kuna mwekezaji atakuja kuwekeza sehemu hakuna umeme wala maji? Mhhh, kweli mdomo kila mtu anao na hautozwi kodi...ruksa kusema unayotaka
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Demokrasia tunayoipigania sisi inatusaidia nini? Kutupa uchaguzi huru? Kutuletea viongozi waadilifu? Au kuongeza mishemishe kwenye ofisi za umma?Maana nahisi tumekuwa kama watu tusiojua tunataka nini.
   
 8. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mambo hayakuanzia hapo, mwaka 59 , Mpangaranyiko wa Tanu, ndipo walipotoka wengi na kuanzisha vyama vya ANC na UPC Nk. Waliobaki ndani ya Tanu au walikumbianchi au waliishia kizuizini. Kilichotokea ni kwamba kufikia 1963 wananchi walionyesha dalili za kukubali mfumo wa vyama vingi, na walianza kuhama TANU, Kipindi hichohicho zilitaka kunyukwa kavukavu pale mjengo mkuu kati ya Mkiti Tanu na ANC, Kisa mazungumzo ya kutenganisha shughuli za siasa na serikali, Mori wa mkiti wa TANU ulipanda na mkutano kuvunjika. Yapo mengi yaliyopotoshwa, lakini kwa kifupi mkiti TANU alikuwa muoga sana wa mawazo mbadala na hasa vyama vya upinzani. Asidanganywe mtu ni uoga tu.

  Inabidi wanahistoria kuwatafuta viongozi wa UPC na ANC ambao bado wako hai kupata ukweli wa mambo.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine huwa watu wanafeli mitihani kirahisi kweli; na hakuna kitu kibaya kama kuangalia vitu kwa hisia zilizoumizwa. Niliwahi kuambiwa kuwa for some people "when pain begins, life stops". Hoja iliyopo ni suala la uamuzi wa kuingia chama kimoja... hoja ya maisha na mauaji ya Kleruu mbona yameshadiliwa sana hapa.
   
 10. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nina hakika kama ningelikuwa kwenye position ya Mwamwindi, nisingemwacha Kleruu arudi salama, ningelifanya the same..., nampongeza sana Mwamwindi kwa uamuzi alioufanya, viongozi Madikteta kama Kleruu hawana moral authority ya kuzungumzia demokrasia na alistahili kufanyiwa alichofanyiwa na kuzidi...

  Lala salama Mwamwindi...
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  It is quit hypocritical how you defend CCM with all your might in your post while the same people you defend are from the so called "chosen ones".
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ninajiuliza hivi Mjerumani anaweza kuandika historia ya Hitler objectively? Myahudi je? Je watu wa Iran wakiandika kuhusu Sadam au Wamarekani juu ya Emperor wa Japan wanaweza kumuangalia na kumsoma kihistoria - objectively? Naweza kusema katika yote hayo "ndiyo" kwa sababu hisia zao zinatakiwa ziwe pembeni ya kile wanachokisoma. HIvyo, watu husoma maandishi ya Hitler na kumuelewa bila kujali hisia zao. Katika Tanzania yetu wapo wasomi ambao kwao ni kukataa kumsoma mtu fulani kwa sababu kawaudhi - hivyo wenye kumchukia Nyerere hawataki hata kumsoma bali kumtupilia mbali kwa sababu "ni dikteta". Nimeona hilo kwa Kleruu vile vile, msomi aliyeumizwa ni vigumu sana kutoa maoni objectively ndio maana labda sisi wengine tunaweza kupitia wasomi hawa tukijitahidi kuweka hisia zetu pembeni. Vinginevyo, tunaweza kujikuta tunatengeneza kundi la wasomi wa ajabu kidogo.

  Kwanini tuliingia kwenye chama kimoja, je ni kweli Nyerere alifuta vyama vingi? Majibu yapo - au sehemu majibu ipo - lakini bahati mbaya wenye kutoa majibu wametuumiza kwa hiyo kwa kweli hatutaki hata majibu yao. I would call this the intellectual deficiencies of our society - where we only read the people we like or agree with or have positive emotional attachment with.
   
 13. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Thanks for a good document

  Je, ni kweli demokrasia inajengwa peke yake kwa vyama vingi?

  Hiyo red inaharibu swali. Demokrasia kwa baadhi yetu ni kuheshimu mawazo, mfumo na utendaji mdala wa kisera na mkakati. Singependa kujibu kwa kuuliza swali ila historia imejidhihirisha kuwa si rahisi demokrasia kustawi kwenye chama kimoja itaishia kiwango fulani cha udikteta.

  Je, yawezekana kubuni mtindo wa kuwa na demokrasia ndani ya Chama kimoja?

  Haiwezekani kwa sababu tayari kwenye chama kimoja umewafanya binadamu ni wamoja kifikra, kimaudhui na kimwenendo.

  Faida na hasara za mifumo yote miwili ni nini hasa?

  Ni katika utekelezaji wa sera na mipango mikakati ndipo utakutana na faida na hasara za mifumo yote miwilli. Moja kubwa kwangu ni checks and balances zinavyokuwa managed.

  Dr. Kleruu anajaribu kujibu. Kwa upande wetu leo hii tunatakiwa kujiuliza je Demokrasia ya vyama vingi imefanya yale ambayo tuliambiwa itaweza kufanya? Vietnam na China ni nchi zenye mfumo wa chama kimoja kwanini zinapiga hatua ya haraka ya maendeleo kuliko sisi?

  Tujiulize mafanikio hayo yana msingi gani?

  1. Uchumi una kanuni zake za kuundesha iwe katika chama kimoja au vyama vingi. Wengi wetu misingi hiyo ni uzalishaji kwa faida, efficiency and effectiveness kwenye all deliveries na kuchukua "timely interventions" vitu hivi havina itikadi

  2. Ushiriki wa jamii ni kitu cha pili ambacho hiki kina kiwango kikubwa sana cha itikadi. Ila, kinakuwa influenced na historia. Uhuru wa kwenye sahani si sawa na uhuru wa mtutu. Nidhamu ya uhuru wa sahani si sawa na nidhamu ya uhuru unaotokana na mapambano ya nguvu.


  Mwisho nachangia tu kuwa kuna demokrasia moja tu ile inayokubarika na jamii na si makundi ya ushawishi usiozingatia usawa (ubaguzi) ndani ya jamii.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndahani,
  Mabaya yote yalifanyika enzi za Nyerere. Hivi sasa Tanzania ni paradiso. Thanks for your answer. Hawa wanatafuta pa kutokea kumsifia Mkwe're lakini tutakula nao tu sahani moja.
   
 15. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Wewe mwoga mkubwa unayependa kujivika ushujaa usiostahili, Tanzania ya sasa imejaa viongozi wachafu na wezi, ni nini basi kinachokuzuia kufanya huo "ushujaa wa kuwaua" ? Huna lolote, hata ungekuwa na wewe uko kwenye nafasi ya huyo jamaa ungeishia kujiharishia uharo tu....
  Unaogopa hata jina lako lisijulikane sembuse kuua... mawe...... kanye ulale...
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi ukiona ilivyosemwa it is more personal than anything.. uliza kwanini alimchukia Kleruu?
   
 17. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  nyerere hakuwa Mungu kuwa sahihi kwa yote, ila katika aliyowahi fanya naamini more than 90% alikuwa sawa. sometimes ili mambo yaende udiktekta inabidi utumike.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi yetu bado tuna fikra za kizamani kwamba ili watu wa kutambue lazima ufungue mziki full kutoka ndani ya nyumba yako. Tunatoa majibu rahisi kwenye maswali magumu sana....Nyerere ninavyoona mimi, itakuwa ngumu sana kumuita failure kwa kulinganisha na viongozi hawa ambao bila aibu wanadiliki kutamka mbele ya watu waliowapa uongozi kwanza hawawezi kutengeneza mvua kutatua tatizo la umeme....jiu la aina hii moja kwa moja linaonyesha uwezo mdogo uliopo wa kutatua matatizo yanayotuzunguka. Hawaongelei kwanini hatujengi pipeline nyingine kuleta gas Dar ili tutengeneza umeme! Hawaongelei kwanini Kiwira coal mine haifanyi uzalishaji wa umeme! Wanachukulia uongozi ni kupanda ndege kwenda kwenye vikao visivyo na tija yoyote kwa nchi yetu hii maskini
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani hata kwa chama kimoja demorasia inawezekana lakini nadhani katika critc amabyo nami naweza kukubalina nayo kuhusu nyerer ni pale alipopalilia utamaduni wa kupigiwa kura na kuvuli au kupitishwa bila kupingwa ndani ya chama
   
 20. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kuwa mchambuzi mzuri na ili uweze kuelewa mambo kwa mapana, inabidi uwasikilize (usome habari ) adui zako na watu usio wapenda pia. Kama utaamua kufuatilia habari za unaowapenda tu, utakuwa umejijengea wigo wa maarifa. Ni ushauri tu.
   
Loading...