Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"

UPDATE.
Nime happen kukutana na mjumbe mmoja wa CC ya Chadema asubuhi hii, amenifafanulia A-Z ya kilichotokea. Chadema walifanya kila waliloweza ili kuwarudisha kwenye mstari lakini ilishindikana. Hao madiwani walizidi kuitunishia misuli CC ya Chadema, hivyo Chadema kama chama, was left with no option bali kuwatimua.

However, kwa vile Mhe. Lema ni major player on one side, na madiwani on the other, sasa na tusubiri jinsi CC ya Chadema, itakavyomshughulikia, na kwa vile yeye ni mjumbe wa CC hiyo ya Chadema, tutawaomba Chadema, wasilimalize suala lake ndani kwa ndani bila kutoa taarifa kwa umma, ili kupusha dhana ya double standards.

Sasa naanza kuwaelewa Chadema kidogo kidogo.

Pasco

Mkuu as a political commentator kama unavyojiita mwenyewe inabidi uwe na facts at hands kabla ya kutoa opnions zako. Inaonyesha you were not well informed on what exactly happened.
 
Ni bora kuwa na wanachama watatu katika chama lakini wenye nidhamu kuliko kuwa na wanachama miilioni wasio na nidhamu. Ni heri CDM ikose hizo nafasi tano za madiwani huko Arusha katika uchaguzi mdogo utakaorudiwa, kuliko kuwa na hata madiwani wote wa mkoa ambao ni mzigo na maadui wa maendeleo ya chama. Kama chama, huo ndo ulikuwa uamuzi pekee wa busara kwa maslahi ya chama na wananchi wa Arusha. Hata Roma ilianguka kutokana na kuibuka kwa falme ndogondogo katikati ya ufalme mkuu. Hatuwezi tukawa na viongozi wa CHADEMA taifa, halafu kukawa na viongozi wengine somewhere ambao wanamaamuzi sawasawa na wale wa Taifa. Chadema walishasema tangu mwanzo, no body is above the party. Hakuna na hatatokea aliye maarufu kupita chama. Hilo litabaki hivyo na linapaswa liheshimiwe. Anayetafuta umaarufu unaokizidi chama aende CCM, huko ndiko mtu mmojammoja anaweza kuwa maarufu kukishinda chama according to makamba.

Machozi yalitaka kunidondoka kwa jinsi ulivyonyoosha, kwa kweli upo sahihi kabisa. Hivi inawezekenaje wizara ya nishati iaagize majenereta ya kuikoa nchi wakati rais Kikwete hajui juu ya mchakato mzima hata wizara hiyo ilikuwa na dhamira nzuri kabisa ya kuindoa nchi katika giza ambalo ni tatizo na siyo jambo la kubishaniwa?

Halafu JK amfukuze waziri wa Nishati kisha uone hakutenda haki waziri alikuwa na nia njema kabisa ya kuinusuru nchi na tatizo la umeme! Kama ukiurge hivyo lazima utakuwa na tatizo, kila kitu jamani tukublai ni lazima kifuate utaratibu na kuna limit ya maamuzi katika management ambayo mtu anaweza kufikia kwa cheo chake jamani!

Madiwani wa CDM kama hakukuwa na ushawishi wa ziada toka CCM wasingekuwa na jeuri kiasi kile cha kifikia hatua ya kuiwekea mashrati CC jinsi ya kuwahoji! Hivi jiulize tulipokuwa mavyuoni tunapokgoma tukitaka kurudishwa huwa tunahojiwa wote kwa pamoja au mmoja mmoja ili kupima ushiriki wake katika mchakato mzima wa tukio!

Kiukweli ni bora kupoteza kata hizo kuliko kuwa na watu ambao wameshaonyesha kungeuka kuliko wazi kabisa! Mimi nikiona kwenye cumputer yangu kuna virus wameingia na kukuna jinsi zaidi ya ku format basi nitachofanya ni kuweka back up yangu vizuri na ku - format kuliko kusubiri ije kushindwa start na nipoteze data muhimu au kuzipata tena kwa gharama kuliko ningechukua tahadhari!

Nimetumia mifano rahisi kabisa ili nieleweke uovu wa hawa madiwani huakuwa wa kuvumiliwa hata kidogo.
 
Mkuu as a political commentator kama unavyojiita mwenyewe inabidi uwe na facts at hands kabla ya kutoa opnions zako. Inaonyesha you were not well informed on what exactly happened.
Mkuu hata asingekutana na huyo mjumbe wa CDM kwa kutumia uelewa wa kawaida kabisa CDM ni chama kinachokuwa hivyo kisngependa kuingia migogoro isiyo rasmi bila sababu za msingi, hivyo kulingana na flow ya watu Pasco angetakiwa kuelewa ukweli.

Lakini kwa sababu ame update thread yake namtakia kila la kheri katika kuweka akili yake wazi na kuepuka ushabiki ambao kiasi huweza kuipa akili chongo ya kufikiri vyema na kuelewa kiini cha mgogoro ni CCM bila kuficha kujitahidi kuanzisha migogoro mingi kwenye chama hiki ili kiache mipango yanhe mimngine yenye tija na chama bali itumie muda wake mwingi ku compromise na member wakorofi ambao njaa yao ndiyo inayowasumbua.

Heko CDM, Heko Pasco kwa kufuatilia ukweli na kuujua na kuuweka jukwaani bila kuficha.

Kazi njema.
 
mbona nimeshasema hapo kuwa ilihitajika politics tupu hapo
slaa na wenzie wangeenda arusha na kuwashawishi tu
na sio kufanya mambo kimahakama
na kamaushahidi wa rushwa uikuwa hakuna,wangewaomba radhi na kuwaambia msimamo wa chama
ni upi ufuatwe.......kisiasa bila vitisho
acha mambo ya ajabu wewe huoni politics unazotaka wewe zifanywe na CDM hazina guarantee na juzi hapa tuliona huko Mbeya jamaa aliyeuza jimbo alivyokigeuka chama na ikumbukwe siasa ilitumika kumweka kwenye mstari sawa ila fweza za magamba zikazidi unga!

Btw hizo siasa unazotaka wewe zinafanywa na magamba na kuangamiza ustawi wa jamii kila siku! hebu angalia uwese hamna kwa sababu wafanyabiashara washazoea faida za kufuru ukiachia mbali uchakachuaji wa bidhaa yenyewe na misamaha ya kodi! tunahitaji maamuzi magumu sasa na CDM kinatia moyo kwa kinachofanya...
 
3. Sisi ambao hatuna vyama, lakini tuna shauku ya kuona Tanzania inaongozwa na chama mbadala, tumekuwa na imani kubwa sana na Chadema kama ndicho chama pekee mbadala ambacho kimethibitisha kikiaminiwa, kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo tunategemea Chadema kitafanya maamuzi yanayofuata misingi ya haki. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".

mpendwa, hapo kwenye #3 naona haijakaa sawa, tamlo lao rasmi la kamati kuu lilisema kuwa walipewa nafasi ya kujitetea na hata hapa jamvini kuna mtu alibandika picha hao madiwani wakiwa pamoja wakisubiri kuingia ndani ya kamati kuu kujitetea, kwa hiyo niaona kuwa walihukumiwa baada ya kusikilizwa ipasavyo.

kuhusu uamuzi kama ni mzuri au la, mi sina shaka kabisa kuwa hata kama chadema kitapoteza kata zote katika chaguzi ndogo za marudio, bado watakuwa wameshinda na uamuzi huu utabaki kuwa precedence ya kurejea siku za usoni. chama kama ccm kina ndhamu kubwa sana ndani ya chama kwa sababu nyingi ikiwamo kuwa mwenyekiti wake ni rais wa nchi na hutambulika hivyo hata akiwa ndani ya kikao cha chama na huambatana na alama zote za ukuu wa dola, kwa hiyo utaona hakuna mwanya wowote wa kubishana naye

imagine dr Slaa angekuwa rais leo, hao madiwani wangefikia hatua ya kubishana na chama chao kwa kiwango hicho wakati rais wa nchi ndiye katibu mkuu wa chama chao na ameshiriki kikao kilichowajadili? kule uchina rais Hu Jintao ndiye katibu mkuu wa chama cha kikomunist cha nchi hiyo, na kikao chochote anachushiriki kina uzito huenda hata kushinda uzito wa vikao vya baraza la mawaziri!

kwa kweli... to sum up, mie sioni mistake yoyote hapo ila naona kuwa wamefanikiwa ku-set precedence ya maana sana kwa siku zijazo!

mbarikiwe sana wapendwa
 
Pasco, nimefurahishwa sana na utatambuzi wako wa kina kuhusu suala hili. Lakini napenda kukuuliza swali moja, kuna tofauti gani kati ya Chama na Wananchi? Je Chama si ndio wananchi, na Wananchi sio Chama? ni vipi unatenganisha hivi vitu viwili?

Je tunaweza kuwa na Chama bila Wananchi? au Wananchi bila Chama? Au umechukua tafsiri ipi ya Wananchi na Wanachama? Kwa kusoma thread yako, inaonyesha umechukulia kuwa Wananchi ni watanzania wote bila kujali chama, na chama ni kikundi cha wananchi fulani waliojipambanua kuamini na kufuata itikadi fulani. Ikiwa kama ni hivyo, na hawa Madiwani walikuwa ndani ya kikundi hicho chenye itikadi yake, sasa wanaasi, unadhani ni Wananchi wapi watakao athirika? ni wale Wananchi wa itikadi au ni hao Wananchi Watanzania?

Kwa maoni yangu CDM wamefanya maamuzi sahihi, kwa njia kuu mbili,

1. Wanakijenga Chama kwa kadili ya itikadi yao,
2. Wanajenga nidhamu ya chama, kwa wanachama wao wote, kwani ni hiari kuamua kujiunga na chama chochote, na kama ukiingia chama chenye nidhamu, ni lazima uwe na nidhamu, ukiingia chama cha ufisadi, ni lazima utakuwa fisadi.

Hitimisho:
Pasco hoja yako inajibiwa na maneno mawili tu nayo ni " Collective Responsibility"

Tanzania tupo hapa tulipofika kutokana na Collective Responsibility, ndio maana Mwalimu Nyerere, wakati anajenga nchi hii, itikadi yake ilikuwa ni ya collective responsibility, ambayo ukiiangalia kwa undani sana ndipo tunapata neno UJAMAA. Hata kwenye chama cha kibepari, wanafanya mambo kijamaa, kwenye mfumo wa chama kimoja, lazima wafanye Kijamaa, kwenye ufisani, lazima wafanye kijamaa, na Chama makini lazima kifanye Kijamaa. Sasa Pasco, Wananchi ni nani na Wanachama ni Nani?
 
Well said Pasco,Chadema as a people's party they need to consider this,tuache maneno ya kurusha rusha tu.Binafsi sikubaliani na maamuzi ya CC,je hawajajifunza toka kwa Kafulila????
 
Wenzao CCM walipokuja na makelele ya kujivua gamba, nilisema CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, na kelele zote za Nape na Chiligati, hawana ubavu wa kuwavua uanachama hao watuhumiwa wa ufisadi kwa kuhofia retaliation ya watu wao, ndio maana mtashuhudia kwenye kampeni za Igunga, CCM lazima impigie magoti RA. Amini nakuambia, hawawezi kuwafanya lolote EL na AC, sana sana watawabembeleza kujiudhuru nyadhifa zao, lakini sio kuwavua uanachama, kwanini Chadema, chama cha matumaini, kifanye makosa ambayo CCM iliyochokwa, haiwezi kuyafanya, ya kuwavua uanachama wachaguliwa wa wananchi?!. That is "A Big Mistake!".
Pasco,
Mkuu nimekusoma lakini unaweza kuyatumia maneno haya haya kwa Magamba ambao wote ni Wabunge waliochaguliwa na wananchi na wametakiwa kujivua.

Kwa kutumia mifano yako hapo juu nionyeshe makosa ya hatua za CCM dhidi ya Magamba kuwa ni Big Mistake kwa chama!.. Nina hakika ushahidi wako utajikuta ukifagilia Ufisadi zaidi.
 
Pasco,baada ya mkutano wa CDM jana Arusha ,ningependa kusikia tena analysis yako katika hii thread.
 
Pasco,
Mkuu nimekusoma lakini unaweza kuyatumia maneno haya haya kwa Magamba ambao wote ni Wabunge waliochaguliwa na wananchi na wametakiwa kujivua. Kwa kutumia mifano yako hapo juu nionyeshe makosa ya hatua za CCM dhidi ya Magamba kuwa ni Big Mistake kwa chama!.. Nina hakika ushahidi wako utajikuta ukifagilia Ufisadi zaidi.
Mkandara,
Bado nasimama na hoja yangu kuwa Magamba hawawezi kuwafanya EL na AC lolote. RA kajivua kwa kukereka sio kwa kuitikia mwito. Watakachofanya sio kuwavua uanachama (kwa kosa lipi?, kama ni ufisadi, mbona wote ni mafisadi, top-butom!), bali watawavua nyadhifa zao zote ndani ya chama kubakia ordinary members ili wasiyapoteze majimbo yao.

Kilio cha ufisadi kinawahusu Watanzania wote, lakini katika majimbo yao, Igunga, Monduli na Bariadi, hao jamaa ni malaika, ndio maana nikasema CCM inahaha kumpigia magoti RA aje kuongoza kampeni zao, vinginevyo jimbo ndio hilo linaondoka.

Mkandara, sifagilii ufisadi, bali mimi ni mpenda haki itendeke, sio mara moja wala mbili nimeuliza, hao watatu wamefanya kosa gani kisheria kustahili adhabu kali namna hiyo, kama JK mwenyewe alisimama jukwaani kuwapigia kampeni na wengine ambao tayari wameishapandishwa kizimbani, CCM wanayo moral authority gani kutaka kuwatimua?.

Dhana ya kujivua gamba ni 'sugar coating' strategy ya CCM kuendelea kuwa 'populist party' kupata umaarufu tuu, na sio ya kusafisha chama, wakati Chadema imewatimua wale madiwani to get rid of bad elements baada ya njia zote mbadala kushindikana.

Nilisema siasa za Kaskazini wanachagua watu na sio chama, jana nimeuona mkutano wa Chadema ulivyofunga, naanza kuiona Chadema katika mwanga mpya. Inawezekana sasa wananchi wa Kaskazini nao wamepata mwamko, sasa wanachagua chama na sio watu. Kama ni hiyo, na ule umati wote wa jana kama ndio wapiga kura wenyewe, basi nina imani kuwa Chadema itavitetea viti vyake vyote vitano, and you never know with Igunga.
 
Well said Pasco,Chadema as a people's party they need to consider this,tuache maneno ya kurusha rusha tu.Binafsi sikubaliani na maamuzi ya CC,je hawajajifunza toka kwa Kafulila????
Iteitei Lya Kitee,
Jana nimeona, na nimekubali, japo nilisema siasa za Kaskazini wanachagua watu na sio chama, jana nimeuona mkutano wa Chadema ulivyofunga, naanza kuiona Chadema katika mwanga mpya.

Inawezekana sasa wananchi wa Kaskazini nao wamepata mwamko, sasa wanachagua chama na sio watu. Kama ni hiyo, na ule umati wote wa jana kama ndio wapiga kura wenyewe, basi nina imani kuwa Chadema itavitetea viti vyake vyote vitano, and you never know with Igunga.
 
Iteitei Lya Kitee,
Jana nimeona, na nimekubali, japo nilisema siasa za Kaskazini wanachagua watu na sio chama, jana nimeuona mkutano wa Chadema ulivyofunga, naanza kuiona Chadema katika mwanga mpya. Inawezekana sasa wananchi wa Kaskazini nao wamepata mwamko, sasa wanachagua chama na sio watu. Kama ni hiyo, na ule umati wote wa jana kama ndio wapiga kura wenyewe, basi nina imani kuwa Chadema itavitetea viti vyake vyote vitano, and you never know with Igunga.

Hujatutendea haki wananchi wa kaskazini. Hapo kwenye nyekundu rejea mgombea binafsi Mh. Sarwat wakati wa Nyerere, ni wazi alichaguliwa kwa kuelewa matakwa ya ya wananchi wake. Issue ya madiwani waliofukuzwa Arusha NI KUKIUKA MATARAJIO ya wapiga kura yao yaliyotafitiwa na uongozi wa CDM.

Sahihisho lingine CDM haina haja ya kutetea viti hivyo, inachotaka CDM sheria na taratibu zilizopo zitumike ili matakwa ya wananchi yawakilishwe kwa haki.

Hata hivyo nashukuru kwa wewe kuwaelewa watu wa kaskazini.
 
Mkandara,
Bado nasimama na hoja yangu kuwa Magamba hawawezi kuwafanya EL na AC lolote. RA kajivua kwa kukereka sio kwa kuitikia mwito. Watakachofanya sio kuwavua uanachama (kwa kosa lipi?, kama ni ufisadi, mbona wote ni mafisadi, top-butom!), bali watawavua nyadhifa zao zote ndani ya chama kubakia ordinary members ili wasiyapoteze majimbo yao.

Kilio cha ufisadi kinawahusu Watanzania wote, lakini katika majimbo yao, Igunga, Monduli na Bariadi, hao jamaa ni malaika, ndio maana nikasema CCM inahaha kumpigia magoti RA aje kuongoza kampeni zao, vinginevyo jimbo ndio hilo linaondoka.

Mkandara, sifagilii ufisadi, bali mimi ni mpenda haki itendeke, sio mara moja wala mbili nimeuliza, hao watatu wamefanya kosa gani kisheria kustahili adhabu kali namna hiyo, kama JK mwenyewe alisimama jukwaani kuwapigia kampeni na wengine ambao tayari wameishapandishwa kizimbani, CCM wanayo moral authority gani kutaka kuwatimua?.

Dhana ya kujivua gamba ni 'sugar coating' strategy ya CCM kuendelea kuwa 'populist party' kupata umaarufu tuu, na sio ya kusafisha chama, wakati Chadema imewatimua wale madiwani to get rid of bad elements baada ya njia zote mbadala kushindikana.

Nilisema siasa za Kaskazini wanachagua watu na sio chama, jana nimeuona mkutano wa Chadema ulivyofunga, naanza kuiona Chadema katika mwanga mpya. Inawezekana sasa wananchi wa Kaskazini nao wamepata mwamko, sasa wanachagua chama na sio watu. Kama ni hiyo, na ule umati wote wa jana kama ndio wapiga kura wenyewe, basi nina imani kuwa Chadema itavitetea viti vyake vyote vitano, and you never know with Igunga.
Nakusoma sana mkuu lakini ebu rudia kujisoma wewe mwenyewe tena.

Utaona kwamba sasa hivi game limegeuka..Unawawekea shaka Uwezo wa CCM kuwavua magamba hivyo udhaifu upo kwa CCM..Na ni makosa kwa CCM kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vigogo hao.. lakini unapokuja kwa CDM ambao wameweza kuchukua maamuzi unasema tena nao ni makosa vile vile kuwafukuza watu ambao wamechaguliwa na wananchi.. Sasa makosa ya CCM yako wapi ikiwa hao pia ni wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi? au unaona ni fahari nzuri ya CCM kuwaacha hawa magamba bila kuwavua uanachama hata kama wamekataa kujivua wenyewe..

Hata hivyo umeuliza ni kwa makosa gani imefikia hadi hawa Madiwani wapewe adhabu kali kiasi hicho..Nitakujibu tena kwa urahisi sana:- Haikuwa adhabu hata kidogo kama wangekubali kujiondoa ktk Uongozi wa Halamashauri huu ulikuwa utaratibu wa kufuata kanuni za chama. Na kama wangejiondoa ktk Halmashauri ya jiji wangebakia kuwa wanachama na Madiwani hadhi ambazo wewe unashindwa kuzipa uzito na thamani kama wangeamua kufuata maagizo ya makao makuu, lakini walipokataa kujiuzulu nafasi za halmashuri ndipo chama kilipochukua maamuzi ya kuwaondoa Uanachama ili wasipate nafasi ya kutambuliwa kama Madiwani..

Kumbuka tu kwamba madiwani wamechaguliwa na wananchi ambao waliingia barabarani kupinga uchaguzi wa Meya na ni jukumu la hawa madiwani kuwalinda wananchi ambao baadhi yao waliuawa na kesi zipo mahakamani. Ingependeza sana kama makao makuu wangekuwa wakifanya Muafaka na chama CCM lakini madiwani wakakataa kukubali muafaka huo kwa sababu wanakilisha wana Arusha waliokufa kupinga uchaguzi wa Meya.. Hapo tungesema CDM CC wamefanya makosa makubwa kuwafukuza madiwani wanaotetea wananchi waliowachagua lakini sio madiwani wafanye kinyume cha matakjwa ya wananchi kisha tuwape support kwa sababu tu maamuzi yamefanywa na kamati kuu ya chama..
Wewe nani (diwani) kufikia kuwasamehe watu wali o fanya mauaji ya ndugu zetu kwa kuweka muafaka wa amani kama vile hakuna lilotokea au kesi na madai ya wananchi hayana uzito zaidi na nafasi zao ktk uongozi wa halmashauri.. Na tofauti baina yao na Rostam ni kwamba Rostam hakuwa na kiburi, alifanya kile alichoagizwa na chama hivyo hawezi kupoteza uanachama wake..alikubali kujiuzulu na ndio maana chama chake hakikufikia kuchukua maamuzi ambayo yangeondoa Ubunge wake.

CCM hawawezi kumvua gamba EL ama Chenge kwa sababu hawa watu wanajua fika kwamba wakijitoa ktk uongozi na chama ndio imetoka. EL hawezi kurudia makosa aloyafanya akiwa Waziri mkuu na amejifunza toka historia ya nchi yetu kwamba siku unaondolewa ktk madaraka basi heshima ya Mdanganyika nayo inakuaga. Hutaheshimika na utanyanyaswa hata kama una nguvu ya kisiasa au utajiri wa aina gani.. Tumewaona kina Jumbe, Sozigwa na viongozi wengi enzi za mwalimu, Mwinyi, Mkapa ambao leo wamedata ubaoni wakisubiri pension zao. Tanzania ukifilsika kisiasa basi ndio maisha yako pia yanakwihs utanyanyaswa hata na Mgambo..EL anayajua haya na hawezi kufanya makosa hayo akijua fika kwamba JK hawezi kumfanya lolote kwa sababu wamefanya mambo mengi amchafu wakiwa pamoja..

Hivyo basi CDM haiwezi kuwabeba hawa madiwani kama vile viongozi wa CDM nao walikuwa na mbinu moja na hawa madiwani. Na isingewezekana kabisa kuwawajibisha viongozi hawa kwa njia nyingine yeyote KISHERIA pasipo kuwavua Uanachama hivyo kuufanya udiwani wao kuwa batili..

Acha hivyo mkuu wangu kuna mshikaji wangu mmoja alinitonya ya kwamba hawa jamaa walijimaini kiasi kwamba walisema makao makuu ya chama haiwezi kuwafanya chochote. Jeuri ile ile ya magamba kina EL hali hakuna mtu alokula nao sahani moja na bila kujua jeuri ile kwamba walilishwa na mapandikizi wa CCM ili kukiweka chama ktk nafasi ngumu kama hii. Wakifukuzwa CCM watapata nafasi ya kuurudisha Mkoa wa Arusha mikoni mwao.

Jambo moja tu ambalo wewe umeshindwa kulifahamu ni kwamba CCM itafanya kila hila kuhakikisha mikoa ya Arusha na Mwanza inarudi mikononi mwao. Na viongozi wa mikoa ngazi zote lazima wawe makini sana ktk mbinu chafu ambazo CCM wanazitumia kuisambaratisha chama..Na hakika wewe ndiye uloshindwa kuelewa kwamba sababu ya Mikoa ya Kaskazini kuichagua CDM ni kwa sababu wamechoka na utawala wa CCM.. Leo unakuja tambua haya baada ya mkutano wa jana?... dah! kazi kweli kweli mbona mimi naipenda CDM sii kwa sababu ya Mbowe, Dr.Slaa au Zitto isipokuwa msimamo wa chama na nguvu ya kuleta mabadaliko.

Watu tumejipanga nyuma ya CDM sio kwa sababu ya majina ya watu iwe Mbowe, Lema au nani nakuomba jifunze kutoka kwa sisi wanachama wenyewe. Mbunge wa Ukerewe na Mwanza wote ni watu ambao walikuwa hawajulikani kabisa na nakuhakikishia karibu asilimi 70 ya wabunge wa CDM wote wameshinda kutokana na jina la chama na sio majina yao.

Hawakuwa chochote sii lolote kabla ya uchaguzi.
 
i
Nakusoma sana mkuu lakini ebu rudia kujisoma wewe mwenyewe tena.
Utaona kwamba sasa hivi game limegeuka..Unawawekea shaka Uwezo wa CCM kuwavua magamba hivyo udhaifu upo kwa CCM..Na ni makosa kwa CCM kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vigogo hao.. lakini unapokuja kwa CDM ambao wameweza kuchukua maamuzi unasema tena nao ni makosa vile vile kuwafukuza watu ambao wamechaguliwa na wananchi.. Sasa makosa ya CCM yako wapi ikiwa hao pia ni wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi? au unaona ni fahari nzuri ya CCM kuwaacha hawa magamba bila kuwavua uanachama hata kama wamekataa kujivua wenyewe..
Hata hivyo umeuliza ni kwa makosa gani imefikia hadi hawa Madiwani wapewe adhabu kali kiasi hicho..Nitakujibu tena kwa urahisi sana:- Haikuwa adhabu hata kidogo kama wangekubali kujiondoa ktk Uongozi wa Halamashauri huu ulikuwa utaratibu wa kufuata kanuni za chama. Na kama wangejiondoa ktk Halmashauri ya jiji wangebakia kuwa wanachama na Madiwani hadhi ambazo wewe unashindwa kuzipa uzito na thamani kama wangeamua kufuata maagizo ya makao makuu, lakini walipokataa kujiuzulu nafasi za halmashuri ndipo chama kilipochukua maamuzi ya kuwaondoa Uanachama ili wasipate nafasi ya kutambuliwa kama Madiwani..
Kumbuka tu kwamba madiwani wamechaguliwa na wananchi ambao waliingia barabarani kupinga uchaguzi wa Meya na ni jukumu la hawa madiwani kuwalinda wananchi ambao baadhi yao waliuawa na kesi zipo mahakamani. Ingependeza sana kama makao makuu wangekuwa wakifanya Muafaka na chama CCM lakini madiwani wakakataa kukubali muafaka huo kwa sababu wanakilisha wana Arusha waliokufa kupinga uchaguzi wa Meya.. Hapo tungesema CDM CC wamefanya makosa makubwa kuwafukuza madiwani wanaotetea wananchi waliowachagua lakini sio madiwani wafanye kinyume cha matakjwa ya wananchi kisha tuwape support kwa sababu tu maamuzi yamefanywa na kamati kuu ya chama..
Wewe nani (diwani) kufikia kuwasamehe watu wali o fanya mauaji ya ndugu zetu kwa kuweka muafaka wa amani kama vile hakuna lilotokea au kesi na madai ya wananchi hayana uzito zaidi na nafasi zao ktk uongozi wa halmashauri.. Na tofauti baina yao na Rostam ni kwamba Rostam hakuwa na kiburi, alifanya kile alichoagizwa na chama hivyo hawezi kupoteza uanachama wake..alikubali kujiuzulu na ndio maana chama chake hakikufikia kuchukua maamuzi ambayo yangeondoa Ubunge wake.
CCM hawawezi kumvua gamba EL ama Chenge kwa sababu hawa watu wanajua fika kwamba wakijitoa ktk uongozi na chama ndio imetoka. EL hawezi kurudia makosa aloyafanya akiwa Waziri mkuu na amejifunza toka historia ya nchi yetu kwamba siku unaondolewa ktk madaraka basi heshima ya Mdanganyika nayo inakuaga. Hutaheshimika na utanyanyaswa hata kama una nguvu ya kisiasa au utajiri wa aina gani.. Tumewaona kina Jumbe, Sozigwa na viongozi wengi enzi za mwalimu, Mwinyi, Mkapa ambao leo wamedata ubaoni wakisubiri pension zao. Tanzania ukifilsika kisiasa basi ndio maisha yako pia yanakwihs utanyanyaswa hata na Mgambo..EL anayajua haya na hawezi kufanya makosa hayo akijua fika kwamba JK hawezi kumfanya lolote kwa sababu wamefanya mambo mengi amchafu wakiwa pamoja..
Hivyo basi CDM haiwezi kuwabeba hawa madiwani kama vile viongozi wa CDM nao walikuwa na mbinu moja na hawa madiwani. Na isingewezekana kabisa kuwawajibisha viongozi hawa kwa njia nyingine yeyote KISHERIA pasipo kuwavua Uanachama hivyo kuufanya udiwani wao kuwa batili..
Acha hivyo mkuu wangu kuna mshikaji wangu mmoja alinitonya ya kwamba hawa jamaa walijimaini kiasi kwamba walisema makao makuu ya chama haiwezi kuwafanya chochote. Jeuri ile ile ya magamba kina EL hali hakuna mtu alokula nao sahani moja na bila kujua jeuri ile kwamba walilishwa na mapandikizi wa CCM ili kukiweka chama ktk nafasi ngumu kama hii. Wakifukuzwa CCM watapata nafasi ya kuurudisha Mkoa wa Arusha mikoni mwao.
Jambo moja tu ambalo wewe umeshindwa kulifahamu ni kwamba CCM itafanya kila hila kuhakikisha mikoa ya Arusha na Mwanza inarudi mikononi mwao. Na viongozi wa mikoa ngazi zote lazima wawe makini sana ktk mbinu chafu ambazo CCM wanazitumia kuisambaratisha chama..Na hakika wewe ndiye uloshindwa kuelewa kwamba sababu ya Mikoa ya Kaskazini kuichagua CDM ni kwa sababu wamechoka na utawala wa CCM.. Leo unakuja tambua haya baada ya mkutano wa jana?... dah! kazi kweli kweli mbona mimi naipenda CDM sii kwa sababu ya Mbowe, Dr.Slaa au Zitto isipokuwa msimamo wa chama na nguvu ya kuleta mabadaliko.. Watu tumejipanga nyuma ya CDM sio kwa sababu ya majina ya watu iwe Mbowe, Lema au nani nakuomba jifunze kutoka kwa sisi wanachama wenyewe. Mbunge wa Ukerewe na Mwanza wote ni watu ambao walikuwa hawajulikani kabisa na nakuhakikishia karibu asilimi 70 ya wabunge wa CDM wote wameshinda kutokana na jina la chama na sio majina yao. Hawakuwa chochote sii lolote kabla ya uchaguzi.
. Mkuu Mkandara asante kwa hili, nilishakiri sasa naanza kuielewa Chadema kidogo kidogo, ni kupitia post kama hizi, hutusaidia sisi wagumu wa kuelewa kuanza kuwaelewa.

Japo sasa nimeshakubaliana na uamuzi wa Chadema as the last option lakini hili la kuitumia bad law ya kudhaminiwa na vyama kugombea nafasi yoyote na pia kuadhibiwa na chama baada ya kuchaguliwa na wananchi haijatulia.

Lazima tufike mahali tutekeleze demokrasia ya kweli kwa kuzipinga sheria kandamizi kandamizi kwa maneno na matendo na tutafute namna ya kuwawajibisha hawa wateule wetu wanapofanya kinyume bila kutumia rungu la chama. Maadam tuko kwenye mchakato wa kuekea katiba mpya, naamini hili litarekebishwa sambamba na kupata wagombea huru ili pia kutupa fursa akina sisi ambao bado hatujaona vyama vya kujuinga navyo, tutupe karata zetu 2015.
 
Thanks CHADEMA CC for standing your ground in purging out of your party those corrupt, indisplined and self absorbed councillors.

Let everybody stay reminded that some of us from other parts of this great country than Arusha, regards CHADEMA highly as a beacon of hope in Tanzanian politics, and we know that CHADEMA is greater than and can do without any bunch of reckless individual party members, kwanza hawana aibu hivi wamesahau watu waliouliwa na polisi pamoja na mke wa Dr Slaa aliyeumizwa na kuonyeshwa damu yake ikitiririka!!! kama wao wamesahau basi wajue watanzania kutoka sehemu nyingine za nchi hii bado wanakumbuka.

CHADEMA is still growing and shinning, Arusha deserves better CHADEMA leaders with a sense of discipline and who can be trusted to stand with their leaders all the way to victory !! Mapambano ya ukombozi wa nchi yetu kisiasa bado yanaendelea, Sheria za vitani zinaruhusu kuuawa askari anayekaidi na kuasi amri na maelekezo halali ya viongozi wake.

Kwa upande wa CHADEMA yatosha kuwafukuza hao jamaa, hata kama CHADEMA Itapoteza baadhi ya viti vya Udiwani Arusha, itakuwa imejenga msingi wa kuaminiwa na watu makini wenye uchungu na nchi hii katika maeneo mengine ya nchi yetu na mwisho wa yote CHADEMA Itapata viti vingi zaidi vya udiwani na ubunge kwa watu makini na wenye kuaminika kutoka maeneo mengine ya Tanzania.

Bravo CC Aluta continua.
 
Mkuu Pasco. Habari.Nimefuatilia posts zako zote,kuna kitu nimekugundua.

1. Pamoja na kuwa Mtanzania Mzalendo na mchambuzi wa masuala ya siasa bado hujazifahamu siasa za Tanzania na uendeshaji wa vyama vya siasa.Kuna wakati bora kupoteza kiti cha Ubunge au Udiwani ili kilinda hadhi ya chama.Sio wakati wote kuna maana ya kuwa na posts hizo.Kujitoa mhanga ni vitu visivyoepukika ili kukijenga chama chochote Cha siasa.

2. Chambuzi zako nyingi huwa zinaongozwa na hisia zaidi kuliko uhalisia. Mwanzoni ulipinga uamuzi wa CHADEMA kwa kuona kuwa CHADEMA iliwaonea madiwani wale. Leo umebadilika kwa Kuongozwa na umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa viwanja vya NMC kitu ambacho sio analysis sahihi.

3. inawezekana kabisa kuwa kuna wakati wapiga kura huchagua watu na sio vyama lakini kupitia watu hao huvipenda vyama. Na endapo mtu huyo atakigeuka chama hicho basi na wapiga kura nao humgeuka mtu huyo hasa Kama mtu huyo atakuwa amekiasi chama hicho.Ila kama itathibitika kuwa mtu huyo ameonewa basi wapiga kura wanakuwa pamoja naye.

4. Ili uwe mchambuzi mzuri unatakiwa usiwe biased hasa kama unamtazamo hasi kuhusu jambo husika.Mchambuzi mzuri huwa anabalance.

Wish You all the best..
i. Mkuu Mkandara asante kwa hili, nilishakiri sasa naanza kuielewa Chadema kidogo kidogo, ni kupitia post kama hizi, hutusaidia sisi wagumu wa kuelewa kuanza kuwaelewa.HJapo sasa nimeshakubaliana na uamuzi wa Chadema as the last option lakini hili la kuitumia bad law ya kudhaminiwa na vyama kugombea nafasi yoyote na pia kuadhibiwa na chama baada ya kuchaguliwa na wananchi haijatulia.

Lazima tufike mahali tutekeleze demokrasia ya kweli kwa kuzipinga sheria kandamizi kandamizi kwa maneno na matendo na tutafute namna ya kuwawajibisha hawa wateule wetu wanapofanya kinyume bila kutumia rungu la chama. Maadam tuko kwenye mchakato wa kuekea katiba mpya, naamini hili litarekebishwa sambamba na kupata wagombea huru ili pia kutupa fursa akina sisi ambao bado hatujaona vyama vya kujuinga navyo, tutupe karata zetu 2015.
 
i. Mkuu Mkandara asante kwa hili, nilishakiri sasa naanza kuielewa Chadema kidogo kidogo, ni kupitia post kama hizi, hutusaidia sisi wagumu wa kuelewa kuanza kuwaelewa.

Japo sasa nimeshakubaliana na uamuzi wa Chadema as the last option lakini hili la kuitumia bad law ya kudhaminiwa na vyama kugombea nafasi yoyote na pia kuadhibiwa na chama baada ya kuchaguliwa na wananchi haijatulia.

Lazima tufike mahali tutekeleze demokrasia ya kweli kwa kuzipinga sheria kandamizi kandamizi kwa maneno na matendo na tutafute namna ya kuwawajibisha hawa wateule wetu wanapofanya kinyume bila kutumia rungu la chama. Maadam tuko kwenye mchakato wa kuekea katiba mpya, naamini hili litarekebishwa sambamba na kupata wagombea huru ili pia kutupa fursa akina sisi ambao bado hatujaona vyama vya kujuinga navyo, tutupe karata zetu 2015.
Pasco Haaa haaa haaa! wee mhuni kweli kweli!..

Mimi nafikiri unashindwa kuitazama picha nzima jinsi ilivyo. Sisi ndio tunamchagua rais na Bunge linaweza kumwondoa rais madarakani wakikosa imani naye..Na sababu ni kwamba haiwezekani watu wote nchini ndio waamue tena nafasi ya rais hata kama amevunja kanuni..

Na mbali na hivyo Mimi nina hakika kabisa kwamba kama kamati kuu ya CCM wakikosa imani na JK na wakaamua kumpokonya uanachama kwa kosa la kukiuka kanuni za chama.. sioni kosa la chama hata kidogo....kwa sababu tukiacha mamlaka yote mikononi mwa viongozi wanaweza hata kuiuza nchi kinyume cha kanuni za mamlaka walokabidhiwa...Nakumbuka Marekani kabla uya uchaguzi ulopita kuna Mbunge wa Pennsylvania alikiuka kanuni za Republican tena kama sikosei kwa kuunga mkono sera za Demokratic, ilibidi kuondolewa akajiunga na Demokratic lakini alishindwa uchaguzi ulofuata kama sikosei.

Pili, tatizo jingine bado ni imani yako kwamba wananchi wanachagua MTU na sio chama.. Hapo ndipo unapokosea kwa sababu sera za chama na ilani zake ndizo zinatakiwa kuwavuta wananchi.. hakuna kiongozi hata mmoja anaweza kuyaleta maendeleo yeye peke yake ama kwa kufuatia uchaguzi wake bali ni ushirikiano baina yake na chama chake ktk kutekeleza hizo ilani za chama..Na nakuomba sana rudia kuzisoma kanuni za vyama utakuta kwamba ni SERA na ILANI za chama ndizo humtangulia mtu aliyechaguliwa...
 
1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni 'unconstitutional' na kiwe struck out from the books of law!. Naamini Chadema hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho ambacho ni bad law, to its advantage, is "A Big Mistake!".

2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is "A Big Mistake!".

3. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".

4. Uzoefu wa siasa za Kanda ya Kaskazini, watu wanachagua watu na sio vyama, ndio maana CCM wanajua wazi kuwa, wao CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, sekretariat yake, CC yao na NEC nzima ya CCM, hata wakapige kambi Moshi mjini, wakeshe kwa siku 30 mfululizo usiku na mchana huku wakipiga kampeni ya nguvu kwa kutumia mabilioni yao wanayofisidi, na kuwavisha wanamoshi wote, zile T.Shirt na kofia, pamoja na kulisha pilau la nguvu siku zote 30, Ndesa hawatamng'oa!. Kitendo cha Chadema kuwavua uanachama watu wa watu mjini Arusha, it's "A Big Mistake!".

5. Wenzao CCM walipokuja na makelele ya kujivua gamba, nilisema CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, na kelele zote za Nape na Chiligati, hawana ubavu wa kuwavua uanachama hao watuhumiwa wa ufisadi kwa kuhofia retaliation ya watu wao, ndio maana mtashuhudia kwenye kampeni za Igunga, CCM lazima impigie magoti RA. Amini nakuambia, hawawezi kuwafanya lolote EL na AC, sana sana watawabembeleza kujiudhuru nyadhifa zao, lakini sio kuwavua uanachama, kwanini Chadema, chama cha matumaini, kifanye makosa ambayo CCM iliyochokwa, haiwezi kuyafanya, ya kuwavua uanachama wachaguliwa wa wananchi?!. That is "A Big Mistake!".

6. Chama makini kama Chadema, is expected to do the right thing, at the right time. Hatua hii, ya kuwavua uanachama madiwani pendwa Arusha, hata kama it was the right step, imekuja at the wrong time!, wakati wakitafuta justification ya kulitwaa jimbo la Igunga, ndio chama kinaanzisha tifu kanda ya Kaskazini ambako ndiko kwenye mizizi yake, mimi sijui, Chadema, imeyafanya hayo kwa kutegemea nini?.

7. Wakati nikiuleta ukosoaji huu, sio vibaya nikiwakumbusha Chadema baadhi ya maamuzi yake na matokeo yake. -Kumuengua Mwera Tarime, niliwaambia humu humu JF, kuwa it was a mistake, matokeo sote tunayajua!. Kususia kutangazwa kwa matokeo na kutomtambua rais, nilicoment humu humu, matokeo yake sote tunayajua, na jinsi Chadema ilivyonufaika na hatua hizo.

8. Niliwahi kuwapa Chadema, ushauri fulani, wapenzi na mashabiki wa Chadema, mlinibeza sana, including viongozi wenu. Mimi nikawasisitizia kuhusu, internal reforms na 'the winning coalition' including strategies kuelekea 2015, mpaka leo, bado sijaona, tuendelee kusubiri, 'the playing ground is not level, and never will it be, hivyo, 2015, tutaingia tena kwenye mechi ile ile, katika mazingira yale yale halafu tutegemee matokeo tofauti? UPDATE. Nime happen kukutana na mjumbe mmoja wa CC ya Chadema asubuhi hii, amenifafanulia A-Z ya kilichotokea. Chadema walifanya kila waliloweza ili kuwarudisha kwenye mstari lakini ilishindikana. Hao madiwani walizidi kuitunishia misuli CC ya Chadema, hivyo Chadema kama chama, was left with no option bali kuwatimuaPasco
Mkuu Pasco niruhusu nizirejee hoja zako kama ilivyozileta nikiwa na mawazo huru yasiyofungamana na siasa za upande wowote au kuwa na ushawishi.
Hoja # 1:Ni kweli sheria hiyo si sahihi kwasababu ulizozitaja. Mahakama kuu ilitoa hukumu nadhani kesi ya Mtikila(Judge Rugakingira RIP). Serikali ilikata rufaa na suala hilo bado lipo mahakamani na sijui kwanini mahakama imeamua kulikalia kimya, pengine ni kutokana na conflict of interest kati ya wateule wa mahakama. Chadema inawajibika kwa sheria za nchi hata kama haikubaliani nazo hadi itapokuwa vinginevyo. Sisi wananchi tuna jukumu la kushinikiza kuhusu mabadiliko hayo. Labda ungesema Chadema walipaswa kuonyesha mfano tofauti ,lakini pia inategmea matokeo ya majadiliano kama ulivyoyaleta katika update yako.

#2: Bado tunarudi pale pale kuwa sheria zetu zina utata sana na sio kwa Chadema tu. Chama kinapokudhamini ni sawa na mwajiri wako wa zamani anapokupa reference letter na ukishaajiriwa ndio mwisho wa influency yake. Ndivyo ilivyo kwa madiwani, wabunge n.k mwajiri wao ni wananchi na wanawajibika kwao, lakini ni sheria hiyo hiyo inayosema chama kinauwezo wa kumvua uongozi mchaguliwa bila kumpa haki mwajiri (mwananchi) kumvua uongozi. Kwa mazingira yaliyopo Chadema ilikuwa na uamuzi unaolingana na sheria zetu, kama ni sahihi au la hilo ni jambo lingine,lakini je walifanya kulingangana na taratibu zetu, jibu ni ndiyo. Hapa ndipo tunatakiwa tuangalie upya wakati wa kujadili katiba mpya.

#3: Nadhani waliitwa katika vikao halali na hawakuwa condemned.Rejea update yako.

#4: Chadema haina sababu ya kufuata mipangilio ya CCM, na inadhima kubwa sana ya kubadilisha mwelekeo wa watu kuhusu uchaguzi ili watu wachague sera za chama na si mtu au watu. Kosa hilo limefanywa na CCM na linawagharimu ni vema Chadema wakalitafutia dawa.

#5: Haa! yaani makosa yaliyofanywa na CCM ndiyo yarudiwe na Chadema! CCM kinameguka kwasababu kiliacha misingi ya uongozi (principles) na kukumbatia haiba(personalities). Uamuzi wa Chadema ni wa kuonyesha njia kuwa wao wanaweza na hakuna zaidi ya Chama. Kuendelea kuwalea watovu wa nidhani ni kufuga na kuzalisha vi-EL na vi-RA au vi-CH vidogo vidogo na vitakapo ota mbawa ndipo yatawakuta ya CCM. Kinga ni bora kulilo kuponya.

#6: Uamuzi sahihi ni ule unaofaa kwa muda muafaka. Igunga ni jimbo moja tu na pengine RA asingejiuzulu tusingekuwa na uchaguzi. Ni bora Chama kikajijengea imani ya kuaminika bila hofu ya uchaguzi kwani chaguzi zipo nyingi na zitakuja lakini credibility ya chama hutengenezwa kwa miaka mingi na kuharibika kwa saa moja. Hakuna haja ya kuogopa maamuzi magumu kama yanayoisumbua CCM na serikali yake kwa hofu ya jimbo moja au mawili, gharama za credibility ya chama ni kubwa sana.

#7: Siasa za Tarime ni very complicated, Mwera alipotemwa Chadema akarudi CCM huyu hakuwa muumini wa sera bali tumbo lake. Nashukuru mh Mbowe alikwenda Tarime na kuwapasha ukweli. Kwa hali yoyote lazima tukubali siasa za Tarime ni beyond politics, ideology na policy.

#8: Nakubaliana na wewe kuwa bado uwanja wa mapambano si sawa(level), kuhusu kuunda coalition nadhani una maanisha na wapinzani wengine, labda tujiulize Mrema ba Cheyo ni wapinzani? CUF yenye uhusiano wa karibu na CCM ni wapinzani. Nadhani ili tuwe na uwanja mzuri agenda ya katiba mpya lazima ipewe kipaumbele , ichukuliwe na Chadema kabla ya mwaka kesho.

Hitimisho
Uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama ni sahihi kwasababu hakuna mtu au watu au Organization iliyowahi kufanikiwa bila nidhamu.
Ni nidhamu inayowatesa CCM sasa hivi.

Nilishawahi kuwaonya Chadema kuwa suala la Arusha lilikuwa la kitaifa na zaidi, na kuliachia madiwani ilikuwa kosa kubwa sana.
Hata baada ya kutangazwa muafaka niliwasihi watoe msimamo cha kushangaza walikaa kimya kwa wiki mbili.
Hii inaonyesha kuwa Chadema hawana vitengo vya kutathmini hali ya kisiasa na kufanya maamuzi ya haraka na busara.
Hili lilipelekea political base' kuwa demoralized.

Mkuatano wao wa Arusha na maoni juu ya uamuzi wao katika blogs na vijiwe unatetea hoja yangu kuwa wapenzi na wanachama walikereka sana na mwenendo wa Chama chao na kwamba maamuzi magumu waliyochukua wame excite base yao tena.

Ingawaje naunga mkono maamuzi ya CC lakini nadhani kuna mapungufu ambayo hayaelezeki kwa njia ya kawaida.
Uongozi wa mkoa na wilaya ulihusika vipi katika sakata zima na je hakuna uzembe miongoni mwao.
Najua uongozi wa wilaya umejikosha kwa kufanya mabadiliko lakini CC ya Chadema inapaswa kutoa kauli kuhusu ushiriki wao.

Pili, je mbunge wa Arusha anahusika vipi na amechukuliwa hatua gani. Kama uwajibikaji wake akiwa mjumbe wa Halamshauri ya jiji la Arusha ungekuwa sahihi mambo yasingefikia hapo yalipofikia. Yeye angekuwa kiungo muhimu sana kwa mawasiliano kati ya makao makuu na madiwani.
Nadhani inabidi CC itolee kauli kuhusu ushiriki wake vinginevyo itakuwa ni double standard.

Mwisho, je muundo wa Chadema upo kamilifu? Vinginevyo habari hizi zisingekuwa za mshtuko, na hii inapelekea niamini kuwa kuna vitengo ndani ya chama haviwajibiki. Utamaduni wa kuunda tume ni ishara ya uzembe kama tunavyoona ndani ya CCM na serikali yake.

Haiwezekani chama chanye sekretariati na CC vishindwe kuelewa nini kinaendelea katika political sphere hasa mambo ndani ya chama chao.
Kuna umuhimu wa Chadema kurejea utendaji wa vitengo vyake na wawepo watu makini zaidi. Chama hakiendeshwi na tume bali facts and principles

Ahsante
 
Mkuu Pasco niruhusu nizirejee hoja zako kama ilivyozileta nikiwa na mawazo huru yasiyofungamana na siasa za upande wowote au kuwa na ushawishi.

Hitimisho
Uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama ni sahihi kwasababu hakuna mtu au watu au Organization iliyowahi kufanikiwa bila nidhamu.
Ni nidhamu inayowatesa CCM sasa hivi.

Ingawaje naunga mkono maamuzi ya CC lakini nadhani kuna mapungufu ambayo hayaelezeki kwa njia ya kawaida.

Mwisho, je muundo wa Chadema upo kamilifu?

Haiwezekani chama chanye sekretariati na CC vishindwe kuelewa nini kinaendelea katika political sphere hasa mambo ndani ya chama chao.
Kuna umuhimu wa Chadema kurejea utendaji wa vitengo vyake na wawepo watu makini zaidi. Chama hakiendeshwi na tume bali facts and principles

Ahsante

Nimejikita kujibu baadhi ya masuala uliyoyaanika hapa jamvini. Nitajibu kiujumla sana.

Kwanza nilitegemea nione "declared interest" yako kwenye hili swala kwa sababu unatumila lugha yenye madaraka makubwa.

Pili kwa baadhi yetu kutokana na uzoefu uchambuzi ungetambua "Risks na Assumptions" katika mchakato na utaratibu mzima wa kufikia maamuzi. Kwa maoni yangu Risk kubwa ilitokana na CCM kutaka kuhodhi mustakabali wa hili suala. Assumption kubwa ilikuwa pande zote zilikuwa na dhamiri njema. Singependa kukufanyia uchambuzi ila ebu zijaribu (test) risk na assumption uone unabakia na option zipi?

Mwisho facts na principles ni guiding factors kwa ajili ya kufikia conclusion fulani. Kwa maoni yangu CDM walichukua tahadhali na muda muafaka kuona dot zina connect vipi.

Mimi nilishiriki kwenye madaraka, uhuru na jamhuri wa nchi hii; nimeona jinsi siasa zilivyogeuzwa na kubadirika kuwa mchezo mchafu. Sasa sijui utailamu timu yako au timu unayocheza nayo ili ufikie lengo?
 
Back
Top Bottom