Guus
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 1,167
- 907
Kwa nini umesema kuwa mwezi May Tanzania tutakuwa kwenye peak ya mashambulizi na vifo?? Wewe ni nani hata useme hivyo?? Wewe ni Mungu uliyeumba mbingu na nchi?
Lock down ni nzuri lakini kama wewe umesema kuwa Tz tunaenda kufa kwa sababu tu hatujafunga majumba yetu na kujifungia ndani basi nimekuchukia kabisaaa. Huna hata huruma kabisa weye. Ni heri nini kwetu?
Tulivyopigika kwa sasa unataka tujifungie ndani ya majumba yetu wakati huu sisi wakulima ndio tunajitahidi kuwahi mvua za masika?? Hivi, ni mtanzania anayejielewa anayasema haya au?
Nadhani mnahitaji kwenda kupimwa akili zenyu. Chuki zenu kwa JPM zisitufanye hata sisi tusiojua siasa kuumizwa na uchokozi wenyu.
Tiyari tushachelewa kujifungia ndani. Acha tuu tungojee vifo vyako ulivyoviona lakini, nadhani huo mwezi May, tutakuwa tunakufa lakini sisi wakulima tutakufa tukichoma mahindi mabichi. Upo hapo?
Ngojea hao unaosema walifanya vyema kujifungia waanze kutoka humo ndani kwa sababu ya njaa uone vita yao. Ndipo na sisi tutaifunga mipaka tuone watakula nini kama sio vumbi la corona.
Tumuombe Mungu kwa bidii na kuziacha njia zetu mbaya. Alisema JPM. Hebu tumuunge mkono
Usiongee kwa mihemko, tumia akili hata kidogo. Unadhani hiyo aliyokuambia JPM uombe kwa bidii ndiyo dawa ya covid-19. Wewe unadhani ni Tanzania pekee ndiyo kwenye dini? Unafikiri nchi nyingine zilizo katika maambukizi ya juu hawakuwa na dini na huwa hawaingii katika nyumba za ibada!! Msiwe vibaraka wa dini hadi mkasahau kuwa ninyi ni binadamu, si wanyama. Mungu huyohuyo alikuwa na nia njema nasi (hata akatuumba kuwa viumbe wenye uelewa, uwezo wa kufikiri na kutafuta suluhu ya matatizo yanayotuzunguka). Ametupa uwezo wa kuwa na madaktari, wahandisi na kadhalika. Au huwa mnahisi hivyo vyote vimeletwa na shetani!!? Akili yako iliyoshikiliwa na dini imekufanya kumuona mtoa mada kama ameiombea "Tanzania kuwa kwenye peak mwezi May", wakati sehemu yeyote yenye maambukizi ni lazima ifike kwenye peak, na Tanzania lazima tufike huko (hata ukitoa povu).