Kwa kuwa hawa wamarekani na Baadhi ya nchi za ulaya zimeonyesha ukigeugeu katika masuala ya mahusiano ya kimataifa(Tumeona IraQ, Na kaskazini mwa Afrika), na kwa kuwa silaha nyingine wanayoitumia kutishia mataifa mengine yanayopingana nayo katika masuala mbali mbali ni kufreeze assets of Central banks za nchi husika. Je Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(JMT) imejiandaaje kujikinga na silaha hii ya kufreeze assets za Central Bank( mfano Benki Kuu ya Tanzania)? Swali linaelekea kwa viongozi waandamizi wa JMT, lakini pia mwana JF unaweza kutoa majibu ya swali hili namna ungeweza kujikinga hili kama ungekuwa Kiongozi mwandamizi wa JMT.