TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601

Wanabodi,

Hii ni TV Program Alert nyingine kufuatia ile ya mwanzo.

Kufuatia mjadala mkali ulioibuka humu jf kuhusu uchaguzi uliopita kama ulikuwa huru na wa haki, na kama Tume ya Uchaguzi haikuchakachua matokeo, jee iliogopa nini independent bodies zisifanye independent tallying, na badala yake, independent tallying ya UKAWA na ile Kituo cha Haki za Binaadamu, vilivamiwa, kuporwa computers zao na wahusika kusweka ndani!, zoezi hili lilitafsiriwa kuwa, kama uchaguzi ulikuwa transparent, with nothing to hide, kwanini Tume ilizifamia zile independent tallying centers, ilikuwa inaogopa nini?!.

Kufuati baadhi ya hoja za jf, kuwa ni hoja za msingi kabisa, nilimtafuta Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, anazijibu hizo hoja na nyingine nyingi, katika kipindi maalum cha Ushiriki wa Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane.

Kipindi hicho kitarushwa leo Tarehe 8/8/2016Saa 12:25 ITV na Saa 3:45 Star TV.

Kesho kitarushwa Channel Ten Saa 2:30 usiku na TBC1 saa 4:00 usiku.

Wewe kama mwana jf, una advantage ya be the first to know, hivyo natoa wito, hata kama uliamini Tume haikutenda haki, na uchaguzi uliopita haukuwa huru na wa haki, lakini information is power!, get the info, ili uujue ukweli wa mambo!, kiukweli watu walidanganywa sana!, na ukiishadanganywa na mtu unaemuamini, akitokea mwingine usiemuamini akakueleza ukweli na kukujulisha, kile ulichoaminishwa mwanzo ni uwongo, umedanganywa, wewe unakuwa huru kuendelea kumuamini yule unayemuamini, kuwa uwongo wake ndio ukweli, na ukweli wa usiomuamini ndio uwongo, wewe utakuwa ni ... bila kujijua!.

Seek the truth, and the truth will set you free.

Karibuni kuangalia.
Natanguliza shukrani,

Paskali.
 
Paskali nimekwambia kwa kuanza kujua kama ni uonngo ama si uongo hebu pitia hukumu ya Uchaguzi wa Jimbo la Vwawa halafu uje hapa tujadiliane. Angekuwa ni Masawe anamtetea Mbowe mngesema ni ukabila, Wewe ulifurahia hadi kusalimiwa kisukuma na kuja humu kutuambia kwamba umesalimiwa kisukuma!!
 
Kama katiba inaruhusu mikutano na maandamano na inavunjwa
sembuse uchaguzi ?

Hapa JF tu threads zinafutwa za kuwakosoa.....

Tuko kwenye 'police state' kiukweli...propaganda za kutuaminisha tupo huru na tunaishi kwa sheria zitawachota wachache
wenye upeo mdogo
Mkuu unacholalamikia ni jipya nchi hii? Watanzania wasahaulifu sana. Tumesahau kabisa mazito kuminya Uhuru wa habari enzi za JK ikiwemo mauaji ya mwangosi,sheria za mitandao,kufungiwa magazeti likiwemo mwanahalisi lakini wapinzani sasa wanamuona JPM ndio dikteta wa kutisha bora ya JK! Wewe ni moja ya wakongwe humu na unajua mijadala mizito ya muda mrefu ilijikita kwenye nini. Tunawajibu wa kuelimisha umma jinsi ya kusimamia haki zao nje ya box ya vyama vya siasa. Kosa tunalofanya ni kupiga kelele pale uhuru wa vyama unapoguswa kuliko pale haki zetu za msingi zinaposiginwa. Ni rahisi vyama kudhibitiwa indirectly hata bila nguvu kama ilivyodhibitiwa NCCR lakini tutafanikiwa pale wanasiasa watapojua hatuyumbishwi na itikadi za vyama bali haki zetu. Vyama vinaishi kilaghai huku umma ukiweka matumaini ya mabadiliko kupitia siasa zao.
 
Whither TZ??? I am scared of September 1.
 
Kwass ningumu cn kubadilishana kitu ambacho mtu anaamin kwn kwenye mind set ya watu wanaamin uchaguzi hukuwa wa haki wengne wanaamin ulikuwa wa haki ss bwn paskali unachokisema ni kweli lakn kubadilika kwa mtu mpaka yy mwenyewe akubali je hiki ninachokiamini ni kwel au c kwel
 
Mkuu unacholalamikia ni jipya nchi hii? Watanzania wasahaulifu sana. Tumesahau kabisa mazito kuminya Uhuru wa habari enzi za JK ikiwemo mauaji ya mwangosi,sheria za mitandao,kufungiwa magazeti likiwemo mwanahalisi lakini wapinzani sasa wanamuona JPM ndio dikteta wa kutisha bora ya JK! Wewe ni moja ya wakongwe humu na unajua mijadala mizito ya muda mrefu ilijikita kwenye nini. Tunawajibu wa kuelimisha umma jinsi ya kusimamia haki zao nje ya box ya vyama vya siasa. Kosa tunalofanya ni kupiga kelele pale uhuru wa vyama unapoguswa kuliko pale haki zetu za msingi zinaposiginwa. Ni rahisi vyama kudhibitiwa indirectly hata bila nguvu kama ilivyodhibitiwa NCCR lakini tutafanikiwa pale wanasiasa watapojua hatuyumbishwi na itikadi za vyama bali haki zetu. Vyama vinaishi kilaghai huku umma ukiweka matumaini ya mabadiliko kupitia siasa zao.

Mkuu Mtazamo naunga mkono kabisa mawazo yako na wala sitaki kuyapinga bali umeongea kinadharia zaidi bila kuangalia uhalisia. Katika mazingira ya nchi yetu ni rahisi kuupinga watawala wa nchi hii bila kuwa mwanasiasa? Wewe ni mgeni kusikia viongozi wa dini waliojaribu kukemea ukiukwaji wa katiba kwa kuambiwa wavue majoho ili waingie kwenye siasa? Wanaharakati sio ndio hao wakipinga ukiukwaji wa mambo wanaambiwa watafuatiliwa nani yuko nyuma ya taasisi zao? Hebu niambie unaweza kupinga ukiukwaji wa mambo nchi hii ukitokea kundi gani? Kama wewe ni mkulima utaanza kupinga kupitia wapi, kama ni mfanyakazi utaanza kupinga kupitia wapi, kama ni mmachinga utatumia jukwaa gani kupinga ukiukwaji huo? Hebu nipe mfano halisi unaodhani unaweza kupinga na ukawa na nafasi ya kusikilizwa unachosema mbali ya siasa. Hebu nisaidie kwenye hilo, vinginevyo utakuwa na mawazo mazuri lakini ya kinadharia zaidi. Hayo huwa nayaita mawazo ya kisomi lakini ukimkabidhi mradi unaishia kufa maana mambo mengi yako ya nadharia za darasani. Niko nakungoja hapa umwage nje ya siasa ni jukwaa gani lingine unaweza kufukuta?
 
By
Kama katiba inaruhusu mikutano na maandamano na inavunjwa
sembuse uchaguzi ?

Hapa JF tu threads zinafutwa za kuwakosoa.....

Tuko kwenye 'police state' kiukweli...propaganda za kutuaminisha tupo huru na tunaishi kwa sheria zitawachota wachache
wenye upeo mdogo
Hasante sana mkuu, hata hawa jf naamini ni wahanga, kilicho ikuta jf kipindi hicho hakijasahaulika. Tabia za selekali baada ya uchaguzi nazo ni mashaka mengine juu ya kile kinacho itwa ushindi
 
Ukweli unajulilana
UKAWA hawakuwa na mgombea wa maana
Hakuna cha kuchaka chua matokeo wala nini
Ni story za wakosaji.

Mnakuwa na Unafiki ktk chama mtegemee kushinda kweli!!?

Watu hawataki kukubari kuwa
Kitendo cha kumchukua lowassa kili wakwaza wengi,
Wapo walio kuwa na mbwembwe kwa lowassa lakini hawakumpa kura
Kwakuwa uchaguzi ule ulijawa na Mbwembwe na ili uonekane wa sasa lazima uwe mpinzani,
Bila kujali hoja na malengo ya mgombea.

Tunatambua fika uchaguzi ulikuwa huru
Kila mtu alikuwa huru kuamua lipi aongee na yupi amchague,
Kwa walio fuatilia uchaguzi wa Uganda lazima wataafiki Tanzania uchaguzi wake ulikuwa huru.
 
Kama katiba inaruhusu mikutano na maandamano na inavunjwa
sembuse uchaguzi ?

Hapa JF tu threads zinafutwa za kuwakosoa.....

Tuko kwenye 'police state' kiukweli...propaganda za kutuaminisha tupo huru na tunaishi kwa sheria zitawachota wachache
wenye upeo mdogo
as a matter of fact huyuhuyu Pascal Mayalla alikuwa anatuhumiwa kuinfluence uongozi wa JF kufuta threads ambazo zilikuwa critical kwa mabosi wake

he has no moral authority kutuambia kitu humu.
 
Back
Top Bottom