BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,792
- 287,994
Unakuja hapa kutaka kutuaminisha kwamba huyu mteule wa Rais ataongea kweli tupu kwamba uchaguzi ule haukuwa wa haki. Kama utakumbuka kuna kura zilikamatwa katika baadhi ya mikoa nchini na nyingine ziliokotwa kule Kagera. Serikali ilituzuia kusema chochote kuhusu kura zilizokamatwa na kuokotwa na kama utakumbuka kura zote zilikuwa zimeshapigwa kwa wagombea wa CCM tu.
Hebu itendee haki akili yako ya kumhoji mtu ambaye tungependa kumsikia badala ya huyu mteule wa Rais. Muhoji Mwenyekiti wa Tume ya maadili kuhusu uchunguzi wake ulipofikia wa wale waliopokea rushwa toka kwa Rugemarila na pesa za wizi za Escrow. Pamoja naye kuwa ni mteule wa Rais hili tunataka sana kulisikia.