TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Mkuu Mohammed Khatibu, Mwenyekiti wa NEC hateuliwi na Mwenyekiti wa CCM, anateuliwa na Rais wa JMT.
Tanzania ina mihimili mitatu huru na vyombo huru vifuatavyo, huru kwa maana ya independent kutokana na sheria inavyoviunda
Serikali
Bunge
Mahakama
Tume ya Uchaguzi
Tume ya Haki za Binaadam
Tume ya Tabia za Viongozi
Tume ya Kuzuia Rushwa
Tume ya Madawa ya Kulevya
Ofisi ya CAG
Ofisi ya DPP
Etc
Wakuu wa vyombo vyote hivyo wanateuliwa na rais wa JMT, Spika wa Bunge ndie Mkuu wa Mhimili lakini mtendaji Mkuu wa Bunge ni Katibu wa Bunge.
Kama Bunge ni huru, mahakama ni huru na NEC pia ni huru, ila sio Shirikishi.
P
Unazeeka vibaya sana wewe mzee siku hizi. Uhuru wa Tume hautokani na imeteuliwa na Mungu au Shetani bali utendaji wa tume hiyo kisheria na kimantiki kwa Wadau wote unawaridhisha ? Je mchakato wa kuteuliwa huyo mtendaji umepitia vigezo gani shirikishi ?

Tume imekataa kuwapa vibali mawakala wa Upinzani mpaka wanaandamana na Akwilina kuuawa bila hatia wewe unaleta poroja za hovyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, bila shaka utakua umemuuliza kuhusu upande wa Z'bar pia (uchaguzi wa awali ulikua huru, wazi na haki? Uhalali wa kufuta na kurudia uchaguzi, nk). Japo naamini jibu lake litakua NEC haihusiki Z'bar bali ZEC. I subscribe na sitakosa kuangalia.

Uchaguzi wa Zanzibar ulifutwa na dola, time ya uchaguzi ilovamiwa na dola na kumlazimisha jecha kufuta kuchaguzi kwa bunduki

Serikali ya jamuhuri ya muungano chino ya chombo ya ulinzi,chini ya Rais mtaafu jakaya kikwete, kuvamia tume kwa nguvu na kupora mamlaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli unajulilana
UKAWA hawakuwa na mgombea wa maana
Hakuna cha kuchaka chua matokeo wala nini
Ni story za wakosaji.

Mnakuwa na Unafiki ktk chama mtegemee kushinda kweli!!?

Watu hawataki kukubari kuwa
Kitendo cha kumchukua lowassa kili wakwaza wengi,
Wapo walio kuwa na mbwembwe kwa lowassa lakini hawakumpa kura
Kwakuwa uchaguzi ule ulijawa na Mbwembwe na ili uonekane wa sasa lazima uwe mpinzani,
Bila kujali hoja na malengo ya mgombea.

Tunatambua fika uchaguzi ulikuwa huru
Kila mtu alikuwa huru kuamua lipi aongee na yupi amchague,
Kwa walio fuatilia uchaguzi wa Uganda lazima wataafiki Tanzania uchaguzi wake ulikuwa huru.
Kikatiba tuna mihimili ifuatayo:
1. Mahakama,
2. Bunge, na
3. Dola.
Watendaji wakuu wa mahakama ni wateule wa rais. Bunge pia lina mkono wa rais. Muhimili upi kati ya hiyo ni huru?
Kinadharia kila muhimili una uhuru kiutendaji lakini inategemeana. Dola inaamua inavyotaka. Hakuna siku wateule wa rais watamkatalia jambo.
 
Mkuu hakuna kitu Kama hicho!

Huyu Rais tulienae hafahamu code of ethics!

Ushawahi kuona wapi magufuli anaiacha ccm anapokuwa anatekeleza majukum yake Kama raisI wa URT ?

Uteuzi wa nafasi mbalimbali ni kwa mujibu wa katiba zinafanywa na rais wa JMT. Hata inapotokea rais wa JMT ndiye huyo huyo Mwenyekiti wa CCM, uteuzi anateua kwa mujibu wa katiba ya JMT na sio katiba ya CCM. Kwa vile the dividing line between rais Magufuli as rais wa JMT and Magufuli as Mwenyekiti wa CCM is very thin, hivyo you can think whatever you think if it makes you happy, be Happy!.

Baada ya Mungu, anayefuatia kwa madaraka makubwa ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - maneno ya Dr Lwaitama

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Uchaguzi wa Zanzibar ulifutwa na dola, tume ya uchaguzi ilovamiwa na dola na kumlazimisha Jecha kufuta kuchaguzi kwa bunduki

Serikali ya Jamhuri ya Muungano chini ya chombo ya ulinzi, chini ya Rais mtaafu Jakaya Kikwete, kuvamia tume kwa nguvu na kupora mamlaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliona popote Jecha kashikiwa bunduki?.
Niliwaeleza uchaguzi mwingine ni mwaka huu 2020, hivyo acheni kulia lia, jipangeni upya mtupe tena jarife, labda this time mtaambulia angalau chochote kitu.
P
 
Hii kitu kumbe uliiposti tangu 2016 lakini Bahati mbaya mimi ndo naiona leo...

Mimi naona unakabiliwa na changamoto ama tatizo moja kama mtangazaji huru unayehoji kupata majibu ya baadhi ya maswali yanayohojiwa na wadau mbalimbali....

Tatizo ulilonalo ni wewe kuwa na majibu ya upande unaoutetea ktk jambo hili...

Hili limenifanya mimi niione taarifa yote uliyoiandaa kutokuwa na credibility zaidi ya kuwa ni propaganda za wanasiasa watuhumiwa wa uchakachuaji wa matokeo...!!
 
Amesema kukusanya matokeo sio kosa, kosa ni kuyatangaza.
P
Amesema kukusanya matokeo sio kosa, kosa ni kuyatangaza.
P
acha ulaghai utajidhalilisha bure walichokuwa wanafanya wale wa mlimani city si ndiyo hicho hicho walokuwa wakifanya kina January Makamba
hebu wachani kutuona sisi ni wajinga hili swali ulivyomuuliza alijibu kuwa ni kosa kutangaza matokeo na kuyaweka kwa computer tayari ni kuyatangaza sasa hili mbona pia CCM walilifanya bila kuchukuliwa hatua acheni porojo za kijinga we na tume yako feki
 
Hoja ya Tume huru ya uchaguzi inaendelea, wakati viongozi mbalimbali wakijitokeza kuikosoa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa sio Tume huru, viongozi wengine wanajotokeza na kuitetea ni Tume Huru
NCHI YETU HATUJAWAHI KUFANYA UCHAGUZI BILA TUME HURU YA UCHAGUZI.
Mkuu Mhe. Mwigulu Nchemba, asante sana kulizungumzia hili la Tume huru ya uchaguzi.

Tupo pia tuliolizungumza sana lakini Watanzania wanahitaji kuelimishwa kikamilifu kuhusu hili ili lieleweke vizuri, na hata Watanzania wenyewe kwa ridhaa zao na kwa ujumla wao, kwenye uchaguzi wa October, waki amua kuichagua CCM tuu and only CCM katika uchaguzi Mkuu huru na wa haki na bila waangalizi wowote kutoka nje, hivyo CCM ndio pekee ikachaguliwa naomba tuu watuelewe.

Hili la Tume huru tumelijadili sana humu

Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

TV Prog. Alert: Tume ya Uchaguzi, NEC, Yajibu Hoja za JF Kuhusu Uchaguzi Huru na Wa Haki!

Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Japo umegharimiwa kwa machozi, jasho na damu, ulikuwa huru na wa haki!. Hongera CCM, CHADEMA poleni!. Mungu saidia Tz

TV Program Alert: Msidanywe na Wanasiasa Kuhusu Uchaguzi Mkuu: Ulikuwa Huru na wa Haki!. Shuhudia!

Ila naomba siku ukipata muda au nafasi, urejee kwenye bandiko lako hili,
Ana kwa ana na Mwigulu Nchemba: Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020
Kuna swali hujalijibu ila pia you are free kutoyajibu depending on how busy you are.
P
 
Wanabodi,

Hii ni TV Program Alert nyingine kufuatia ile ya mwanzo.

Kufuatia mjadala mkali ulioibuka humu jf kuhusu uchaguzi uliopita kama ulikuwa huru na wa haki, na kama Tume ya Uchaguzi haikuchakachua matokeo, jee iliogopa nini independent bodies zisifanye independent tallying, na badala yake, independent tallying ya UKAWA na ile Kituo cha Haki za Binaadamu, vilivamiwa, kuporwa computers zao na wahusika kusweka ndani!, zoezi hili lilitafsiriwa kuwa, kama uchaguzi ulikuwa transparent, with nothing to hide, kwanini Tume ilizifamia zile independent tallying centers, ilikuwa inaogopa nini?!.

Kufuati baadhi ya hoja za jf, kuwa ni hoja za msingi kabisa, nilimtafuta Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, anazijibu hizo hoja na nyingine nyingi, katika kipindi maalum cha Ushiriki wa Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane.

Kipindi hicho kitarushwa leo Tarehe 8/8/2016Saa 12:25 ITV na Saa 3:45 Star TV.

Kesho kitarushwa Channel Ten Saa 2:30 usiku na TBC1 saa 4:00 usiku.

Wewe kama mwana jf, una advantage ya be the first to know, hivyo natoa wito, hata kama uliamini Tume haikutenda haki, na uchaguzi uliopita haukuwa huru na wa haki, lakini information is power!, get the info, ili uujue ukweli wa mambo!, kiukweli watu walidanganywa sana!, na ukiishadanganywa na mtu unaemuamini, akitokea mwingine usiemuamini akakueleza ukweli na kukujulisha, kile ulichoaminishwa mwanzo ni uwongo, umedanganywa, wewe unakuwa huru kuendelea kumuamini yule unayemuamini, kuwa uwongo wake ndio ukweli, na ukweli wa usiomuamini ndio uwongo, wewe utakuwa ni ... bila kujijua!.

Seek the truth, and the truth will set you free.

Karibuni kuangalia.
Natanguliza shukrani,

Paskali.

Haya ni majibu mazuti sana kwa wafuasi wa Chadema ambao baada ya kug'amua kuwa wameshashindwa uchaguzi. Wanaleta kisingizio kuwa tume sio huru. Kumbe mchakato huwa unafanyika kwa uhuru na uwazi kabisa. Tunashukuru kwa hii elimu.
 
Acha visingizio vya kitoto. Mbona inaplay bila shida. Tume ipo huru,mawakala wanasaini fomu za matokeo na zinabandikwa ngazi zote alafu mnapotosha umma eti mnaibiawa!

Kwangu haichezi, simaanishi kwa wengine haichezi. Kila kituo kinabandika ya kwake. Je jumla juu inakuwa sawa? Hilo moja, nimeona kwa macho yangu mawakala wakilazimishwa na polisi tena kwa vipigo, kusaini fomu za matokeo zisizo halali. Hilo la pili, je yale mabox yanatolewa vituoni na kwenda kujazwa kura za ccm, kwa uratibu wa jeshi la polisi inakuwaje hapo? Sina chembe ya shaka na nilichokuambia.
 
Mh...Hiyo ni ngumu kuamini,fomu za matokeo zinabandikwa kila kituo kwa uwazi,na kila wakala anasaini kwa hiari.Matokeo yanabandikwa nje na masanduku yanasindizwa na mawakala kuanzia ngazi ya kituo mpaka mwisho. Hizo habari za uongo za polisi kujaza masanduku nani ataziamini?
 
Sikulazimishi ww au nyinyi kuziamini, maana kwa kiwango kikubwa zinakufedhehesha. Kimsingi ukweli hauhitaji nguvu kubwa kuutetea, maana ukweli unajisimamia wenyewe. Haya mambo ninayokuambia yamefanyika mbele ya macho ya wapiga kura, hiyo ndio sababu hasa ya watu kulidharau box la kura, na kutokujitokeza kujiandikisha au kupiga kura. Sishangai ww kuukataa ukweli, maana ukweli kwa namna yoyote ile unaumiza. Sio mara moja au mbili, nimekuwa nikikuambia kuwa ww ni mtetezi uovu sababu ya mambo ya mahaba niue.
 
Acha hasira,kama kuna mawakala wanalazimishwa kusaini fomu na maboksi yanajazwa kura kwa nguvu na polisi,mbona hatujasikia mkienda mahakamani?
 
Wanabodi,

Hii ni TV Program Alert nyingine kufuatia ile ya mwanzo.

Kufuatia mjadala mkali ulioibuka humu jf kuhusu uchaguzi uliopita kama ulikuwa huru na wa haki, na kama Tume ya Uchaguzi haikuchakachua matokeo, jee iliogopa nini independent bodies zisifanye independent tallying, na badala yake, independent tallying ya UKAWA na ile Kituo cha Haki za Binaadamu, vilivamiwa, kuporwa computers zao na wahusika kusweka ndani!, zoezi hili lilitafsiriwa kuwa, kama uchaguzi ulikuwa transparent, with nothing to hide, kwanini Tume ilizifamia zile independent tallying centers, ilikuwa inaogopa nini?!.

Kufuati baadhi ya hoja za jf, kuwa ni hoja za msingi kabisa, nilimtafuta Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, anazijibu hizo hoja na nyingine nyingi, katika kipindi maalum cha Ushiriki wa Tume ya Uchaguzi kwenye Maonyesho ya Nane Nane.

Kipindi hicho kitarushwa leo Tarehe 8/8/2016Saa 12:25 ITV na Saa 3:45 Star TV.

Kesho kitarushwa Channel Ten Saa 2:30 usiku na TBC1 saa 4:00 usiku.

Wewe kama mwana jf, una advantage ya be the first to know, hivyo natoa wito, hata kama uliamini Tume haikutenda haki, na uchaguzi uliopita haukuwa huru na wa haki, lakini information is power!, get the info, ili uujue ukweli wa mambo!, kiukweli watu walidanganywa sana!, na ukiishadanganywa na mtu unaemuamini, akitokea mwingine usiemuamini akakueleza ukweli na kukujulisha, kile ulichoaminishwa mwanzo ni uwongo, umedanganywa, wewe unakuwa huru kuendelea kumuamini yule unayemuamini, kuwa uwongo wake ndio ukweli, na ukweli wa usiomuamini ndio uwongo, wewe utakuwa ni ... bila kujijua!.

Seek the truth, and the truth will set you free.

Karibuni kuangalia.
Natanguliza shukrani,

Paskali.

Hebu tusikilize tena kilichosemwa kwenye dakika ya 2 na sekunde ya 40 ndipo tuendelee na hoja
 
Back
Top Bottom