Tuzo ya MO Ibrahim 2013

Tuzo ya MO Ibrahim 2013

naamini kama rais angalikuwa dk slaa. icc zamani ingalikuwa ishapiga hodi tz
 
hiyo tuzo anastahili Dr Slaa japokuwa sio Rais,maana amefanya mengi makubwa,list of shame(Mwembeyanga),EPA,MEREMETA,KAGODA,RICHMOND na mengineyo.
 
Rais Jakaya kikwete awali alitajwa kuwa angepokea Tuzo ya MO-Ibrahim na gazeti moja la Marekani lakini katika hali isiyo ya kawaida mwaka huu tena Tuzo hii tena imekosa mtu,

Sababu zinazotajwa kuwa sababu kubwa za Jakaya kikwete kukosa Tuzo hiyo hizi hapa:

Kwanza kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya dola kunyanyasa Raia wake.

Kushindwa kudhibiti mianya ya Rushwa kwa vitendo.

Kuminya demokrasia kwa vyama pinzani, hii imeelezewa kuwa polisi ndo wamemsababishia sana.

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari na kushindwa kuchukua hatua kama mkuu wa nchi, hapa imeelezwa kuwa kufungia vyombo vya habari bila sababu za msingi na mauaji ya waandishi wa habari, hapa Idara ya habari maelezo na wizara ya habari imelaumiwa sana katika hili pamoja na polisi kwa kumnyima Mkuu Tuzo hii.

vigezo vingine vyote alikuwa ameshinda, Jakaya ajitahidi tu achukue hatua na afanyie kazi haya yote mwakani atapewa tu.

source: Vigezo vya MO-IBRAHIMU KATIKA KUTOA TUZO KWA VIONGOZI WA AFRIKA.

Yaonekana hata ufuatilii kujua masharti ya Tuzo hii. Hii wanapewa Marais waliochaguliwa kidemokrasia na kuachia madaraka kwa mujibu wa sheria kidemokrasia. Haitolewi kwa marais walio bado madarakani. Labda ungemsema Mh. Mkapa na Mh. Mwinyi.
 
Tuzo hii ingejivunjia heshima kama ingemtunukia na ingekua ni matusi na dharau kwa watanzania.Ingekua Tuzo ya Aibu!

Afterall,Ni kwa wastaafu

Iweje matusi kwa watz wakati wao ndio waliomuweka JK madarakani?
 
Kwa mara nyingine tena hakuna mshindi wa tuzo binafsi yenye thamani duniani- Tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora barani Afrika. Ni mara ya 4 katika kipindi cha miaka 7 mshindi wa dola milioni tano anakosekana. Zawadi hiyo hutolewa kwa viongozi waliochaguliwa kidemokrasia na kuachia ngazi kwa hiari. Je vigezo vimekuwa vigumu na vinahitaji kubadilishwa? Tweets Salym

[h=2]Tuzo ya Mo Ibrahim yakosa mshindi tena[/h]
Nini kimewasibu? Utawala Bora ndio propaganda inayotawala kusimamia nchi huku viognozi wengi wakihaha kuhusu upatikanaji wa rasilimali ikiwemo nishati na jinsi ya kugawa rasilimali hizo, nchi za magharibi zikiwa hazijali tena swala la uongozi bora bali kusisitiza utawala bora ambapo wanyonge si lazima wawe kipaumbele na aliyeko madarakani ili mradi analinda malsahi ya Magharibi basi anapaswa kubaki hapo.
 
Last edited by a moderator:
The Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership
Criteria
-former African Executive Head of State or Government
-left office in the last three years
-democratically elected
-served his/her constitutionally mandated term
-demonstrated exceptional leadership.
Source: http://www.moibrahimfoundation.org/ibrahim-prize/
Thus, the first criterion disqualifies JK. You don't even need to look at other above-mentioned criteria.

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
ikifikia dk slaa atakuwa rais. tz itaingia katika historia mpya ya viongozi wao kwenda mahakama ya kimataifa
 
Iweje matusi kwa watz wakati wao ndio waliomuweka JK madarakani?

Achana na mbeba sumu mifukoni huyo.

Kasoma lakini elimu yake haijamkomboa amegeuzwa kuwa yaya wa mtoto wa Mshumbusi.
 
Si kuna mtu alisema hapa leo kasikia fununu Kikwete kachaguliwa,imekuwaje?
 
Nyie magwanda wacheni uongo hiyo tuzo hapewi kiongozi aliyopo madarakani.

The Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership

Established in 2007, the Ibrahim Prize celebrates excellence in African leadership. It is awarded to a former Executive Head of State or Government by an independent Prize Committee composed of eminent figures, including two Nobel Laureates.

Source: Ibrahim Prize | Mo Ibrahim Foundation
 
Hivi si inakuwa kwa ajili ya viongozi wastaafu au wamebadili?

Mkuu ni sawa, ila kumbuka kuwa, Tume maalumu ya kuangalia vigezo hivi huwa inafanya hivi,

Inaandaa majina ya viongozi waliopo madarakani na Nchi zao, then, wanaandaa orodha ya viongozi waliostaafu na Nchi zao,

Baada ya hapo wanaanza kuangalia vigezo vya Nchi husika kwa viongozi waliopita na wa sasa, then baadae tena watatumia vigezo hivi hivi kutafuta mshindi,

Mfano:

Rais Mkapa alipokuwa madarakani waliorodhesha jina lake na Nchi yake yaani Tanzania,

Sasa wakapima utendaji wake kwa vigezo vya MO-IBRAHIMU, wakasema HAFAI.

Sasa kwa utendaji ule ule na vigezo vile vile vya MKAPA wakaangalia je kuna mabadiliko kati ya MKAPA NA KIKWETE?

Ndo Vigezo hivi hivi vitatumika sasa kwa kikwete.
 
Someni hiyo habari kabla ya kushadadia na comments....Habari inasema tuzo ni kwa marais wastaafu na sio walioko madarakani na miaka yote imekua hivyo...sasa mnamsakama JK as if alishamaliza muda wake
 
Rais Jakaya kikwete awali alitajwa kuwa angepokea Tuzo ya MO-Ibrahim na gazeti moja la Marekani lakini katika hali isiyo ya kawaida mwaka huu tena Tuzo hii tena imekosa mtu,

Sababu zinazotajwa kuwa sababu kubwa za Jakaya kikwete kukosa Tuzo hiyo hizi hapa:

Kwanza kushindwa kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya dola kunyanyasa Raia wake.

Kushindwa kudhibiti mianya ya Rushwa kwa vitendo.

Kuminya demokrasia kwa vyama pinzani, hii imeelezewa kuwa polisi ndo wamemsababishia sana.

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari na kushindwa kuchukua hatua kama mkuu wa nchi, hapa imeelezwa kuwa kufungia vyombo vya habari bila sababu za msingi na mauaji ya waandishi wa habari, hapa Idara ya habari maelezo na wizara ya habari imelaumiwa sana katika hili pamoja na polisi kwa kumnyima Mkuu Tuzo hii.

vigezo vingine vyote alikuwa ameshinda, Jakaya ajitahidi tu achukue hatua na afanyie kazi haya yote mwakani atapewa tu.

source: Vigezo vya MO-IBRAHIMU KATIKA KUTOA TUZO KWA VIONGOZI WA AFRIKA.

Duh, hapa awe mwangalifu!
Hawa watendaji wake kama wamemkosesha tuzo wanaweza kumfikisha hata the Hague!
 
Tuzo ya utawala bora Afrika kwa mwaka 2013 imekosa mshindi. Tuzo hii hupewa kiongozi aliyefanya vizuri katika nyanja ya afya,elimu,usalama na maendeleo ya kiuchumi. Hii ninakua mara ya nne kutopatikana mshindi pia mwaka 2009,2010,2012 alikosekana mshindi.

Tuzo hiyo ina thamani ya $5 (malipo ya awali) na $200,000 kwa kila mwaka kwa maisha yote ya mshindi na inadhaminiwa na Bw Mo Ibrahim (Tycoon) na mzaliwa wa Sudan

Source: DW - Kiswahili

==============

Niliposoma hapo kwenye red nilidhani mdhamini wa hiyo tuzo ni yeye huyo adumuye milele; aliyeishinda kuzimu. Nilipofika hapo kwenye blue nikashangaa, tena nikajiuliza yeye hataonja umauti? Kumbe inadhaminiwa na Mo? Mbona siku za hiyo "tuzo" wala sio nyingi, tena zapita kama ua la kondeni? Viongozi chapeni kazi, achaneni na tuzo za Mo.
 
Tuzo ya utawala bora Afrika kwa mwaka 2013 imekosa mshindi. Tuzo hii hupewa kiongozi aliyefanya vizuri katika nyanja ya afya,elimu,usalama na maendeleo ya kiuchumi. Hii ninakua mara ya nne kutopatikana mshindi pia mwaka 2009,2010,2012 alikosekana mshindi.

Tuzo hiyo ina thamani ya $5 (malipo ya awali) na $200,000 kwa kila mwaka kwa maisha yote ya mshindi na inadhaminiwa na Bw Mo Ibrahim (Tycoon) na mzaliwa wa Sudan

Source: DW - Kiswahili

==============

Kama wanakubali zawadi hii, sasa ICC wanaikataa nini. Walishakubali udhaifu wa utawala wao, wana walakini katika maongozi yao. madikteta wakubwa, zawadi ililenga kuwashawishi waache udikteta na wakakubali kuwa wao wana mapungufu inabidi wahamasishwe kubadilika. Anayefanya vizuri anapata fedha, anayefanya vibaya anapelekwa ICC!
 
Back
Top Bottom