Tuwe wakweli kwa hali ya kimpira tuliyo nayo Tanzania, kuajiri kocha MGENI ni kumzawadia mihela ya bure tu

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Kwa yeyote anayehusika na jambo hili ikiwa ni mchengerwa au karia ama mwingine yeyote akitumia akili yake bila kuipeleka likizo atakubaliana na mimi kwamba Kwa wachezaji wa timu ya taifa tuliyonayo sasa ni uharibifu wa mali za umma kuleta kocha Toka mataifa ya kigeni.

Kama wadau wako serious na mpira wa nchi hii basi nawashauri wawatafute wageni Kwa level ya consultance ya namna gani tutengeneze vijana watakaoliletea taifa makombe nyakati zijazo.

Kwa sasa atafutwe kocha yeyote tu mzawa mwenye sifa za kukaa kwenye benchi la ufundi ilimradi siku ziende.

Kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye timu ya taifa Kwa sasa ni kama kujaribu kumlipia ada ya chuo kikuu mwanafunzi mwenye zero ya o level.
 
Wachezaji ndio shida mfano mechi ile kim alifanya kazi yake sawia.

Shabalala anapiga danadana unategemea nini sasa?
ndo anachosema mleta mada,kwasasa hatuna wachezaji wenye ujuzi hata wakifundishwa na kocha bora wa Dunia,cha msingi wampe timu kocha mzawa mwenye sifa alafu wawekeze kwenye academic za kulea na kukuza vipaji.Kim ni kocha mzuri ila wachezaji hatuna.
 
Kama mtu Kama Karia anawekwa kuongoza mpira unategemea nn? Mi nilishaacha kuangalia mpira WA Tanzania zamani Sana.

Mabadiliko yaanze Kwa Raisi WA shirikisho na yeye atoke waje watu wenye weledi WA kuongoza kile chombo, sio vibaya hata tukiajiri foreigner ambaye CV yake inajitosheleza au hata tukimpa kazi ya Consultancy kusaidia soka letu.

Toka jamaa Aingie madarakani hakuna kipya Taifa Starz ilichofanya. Wao wanakaza kufaidisha matumbo Yao Tu huku soka letu likididimia.
 
Ni kweli kabisa mkuu kwa mpira wa hapa bongo na wachezaji wetu kuajiri kocha mgen ni bure
Wachezaji wenyew kwenye timu ya taifa naon kama hawana spirit ya kupamban kama taifa tofaut na wenzetu wa afrika magharib huko
 
Kwa yeyote anayehusika na jambo hili ikiwa ni mchengerwa au karia ama mwingine yeyote akitumia akili yake bila kuipeleka likizo atakubaliana na mimi kwamba Kwa wachezaji wa timu ya taifa tuliyonayo sasa ni uharibifu wa mali za umma kuleta kocha Toka mataifa ya kigeni.

Kama wadau wako serious na mpira wa nchi hii basi nawashauri wawatafute wageni Kwa level ya consultance ya namna gani tutengeneze vijana watakaoliletea taifa makombe nyakati zijazo.

Kwa sasa atafutwe kocha yeyote tu mzawa mwenye sifa za kukaa kwenye benchi la ufundi ilimradi siku ziende.

Kuwekeza nguvu nyingi sana kwenye timu ya taifa Kwa sasa ni kama kujaribu kumlipia ada ya chuo kikuu mwanafunzi mwenye zero ya o level.
Ukweli ambao wanaoongoz mpira bawataki kusikia. Wao wanajua kwamba hao makocha wa kigeni watawapa hizo 10% zao.

Uliona wapi kocha wa ukweli anakubali job alafu tayari mlishampangia assistant? Siku hizi watu wanakuja na watu wao period.

Kulipa kocha wakigeni wakati huwekezaji kwenye wachezaji hamna ni kutwanga maji kwenye kinu tuu.
 
Kama mtu Kama Karia anawekwa kuongoza mpira unategemea nn? Mi nilishaacha kuangalia mpira WA Tanzania zamani Sana.

Mabadiliko yaanze Kwa Raisi WA shirikisho na yeye atoke waje watu wenye weledi WA kuongoza kile chombo, sio vibaya hata tukiajiri foreigner ambaye CV yake inajitosheleza au hata tukimpa kazi ya Consultancy kusaidia soka letu.

Toka jamaa Aingie madarakani hakuna kipya Taifa Starz ilichofanya. Wao wanakaza kufaidisha matumbo Yao Tu huku soka letu likididimia.
Kwani Taifa stars iliwahi kufanya nini hata kabla ya Karia?
 
Ni kweli kabisa mkuu kwa mpira wa hapa bongo na wachezaji wetu kuajiri kocha mgen ni bure
Wachezaji wenyew kwenye timu ya taifa naon kama hawana spirit ya kupamban kama taifa tofaut na wenzetu wa afrika magharib huko
Ata huko kwenyewe watu wao wanalalamika kuwa hawajitumi kama wakiwa kwenye vilabu vya ulaya.
Problem kubwa ni kwamba hatuwajali pia wachezaji wetu.

Match bonuses mara sijui kuwasafirisha wachezaji economy wakati wakiwa kwenye timu zao ulaya wanasagiri business class au ata private jet.
 
Kwani Taifa stars iliwahi kufanya nini hata kabla ya Karia?
Kipindi cha Mbrazili maendeleo yalikuwa yanaonekana.

Wale wote waliokuwa wanafatilia mpira watakwambia.

Hata uwanjani watu walikuwa wanahamasika kwenda.
Mpira ulikuwa unavutia Sana, wachezaji na hata viongozi walijitoa Kwa ajili ya timu.
 
Kama mtu Kama Karia anawekwa kuongoza mpira unategemea nn? Mi nilishaacha kuangalia mpira WA Tanzania zamani Sana.

Mabadiliko yaanze Kwa Raisi WA shirikisho na yeye atoke waje watu wenye weledi WA kuongoza kile chombo, sio vibaya hata tukiajiri foreigner ambaye CV yake inajitosheleza au hata tukimpa kazi ya Consultancy kusaidia soka letu.

Toka jamaa Aingie madarakani hakuna kipya Taifa Starz ilichofanya. Wao wanakaza kufaidisha matumbo Yao Tu huku soka letu likididimia.
Kuwekeza lawama nyingi sana Kwa karia ni kama kumuonea tu, Kwa maoni yangu jukumu kubwa sana la rais wa shirikisho ni kusimamia utawala Bora wa ili ogani zote za mpira zifanye kazi kwa mujibu wa taratibu, Kwa maoni yangu hata kama si Kwa kiwango kikubwa hilo linajitahidi kufanyika.

Ninachofikiria ni kwamba tunahitaji kupunguza gharama kwenye timu ya taifa bali tuwekeze kwenye KUTENGENEZA kizazi kipya cha wacheza soka wenye uwezo mkubwa.
 
Kwa miaka 5 iliyopita alivyokuwa Raisi amesaidia nini kwenye timu ya Taifa?

Lawama lazima zimuangukie yeye maana yeye ndo kiongozi WA kile chombo, Kama serikali wanatoa pesa kwenda TFF, FIFA nao wanatoa mzigo wao, lakini soka letu halikui lipo pale pale Nani wakumlaumu zaidi ya aliyepewa majukumu kuongoza?

Ni dhahiri kuwa jamaa Hana creativity kabisa. Na Sisi tunahitaji mabadiliko.
 
Kipindi cha Mbrazili maendeleo yalikuwa yanaonekana.

Wale wote waliokuwa wanafatilia mpira watakwambia.

Hata uwanjani watu walikuwa wanahamasika kwenda.
Mpira ulikuwa unavutia Sana, wachezaji na hata viongozi walijitoa Kwa ajili ya timu.
Hujampa muuliza swali majibu yenye akili zaidi umepiga bla bla. Nilitegemea ujibu lamda kipindi cha Raisi wa TFF Fulani timu ya taifa ilishika nafasi Fulani kwenye rank za FIFA tofauti na Sasa lamda tupo chini sana au tulichukua kombe Fulani ukilinganisha na Sasa au tuliuza wachezaji kadhaa kwenda kucheza ulaya na nchi nyingine kulinganisha na Sasa.
 
Kwa miaka 5 iliyopita alivyokuwa Raisi amesaidia nini kwenye timu ya Taifa?

Lawama lazima zimuangukie yeye maana yeye ndo kiongozi WA kile chombo, Kama serikali wanatoa pesa kwenda TFF, FIFA nao wanatoa mzigo wao, lakini soka letu halikui lipo pale pale Nani wakumlaumu zaidi ya aliyepewa majukumu kuongoza?

Ni dhahiri kuwa jamaa Hana creativity kabisa. Na Sisi tunahitaji mabadiliko.
Hebu nikuulize kidogo tufanye wewe ndiye umekalia kiti Cha karia unadhani ni njia gani utatumia kuifanya timu ya taifa ishinde? Hebu jaribu kuniwekea mfano wa mikakati yako ambayo Iko katika wigo wa rais wa shirikisho
 
Kama mtu Kama Karia anawekwa kuongoza mpira unategemea nn? Mi nilishaacha kuangalia mpira WA Tanzania zamani Sana.

Mabadiliko yaanze Kwa Raisi WA shirikisho na yeye atoke waje watu wenye weledi WA kuongoza kile chombo, sio vibaya hata tukiajiri foreigner ambaye CV yake inajitosheleza au hata tukimpa kazi ya Consultancy kusaidia soka letu.

Toka jamaa Aingie madarakani hakuna kipya Taifa Starz ilichofanya. Wao wanakaza kufaidisha matumbo Yao Tu huku soka letu likididimia.
Mimi Yanga mwenzio lakini tatizo siyo Kiria. Tatizo ni michezaji yenyewe tu ya hovyo. Sisi tunaangalia mpira miaka mingi michezaji yetu ni ya Hovyo. Wakati tunaitwa Kichww cha Mwendawazimu Kiria hakuwepo.
 
Kipindi cha Mbrazili maendeleo yalikuwa yanaonekana.

Wale wote waliokuwa wanafatilia mpira watakwambia.

Hata uwanjani watu walikuwa wanahamasika kwenda.
Mpira ulikuwa unavutia Sana, wachezaji na hata viongozi walijitoa Kwa ajili ya timu.
Huu nao ilikuwa moja ya mikakati dhaifu sana mheshiwa rais wa awamu ya nne alikuwa na nia njema sana ya kuuendeleza mpira wetu ila njia iliyotumika ya kumleta kocha na kuongeza hamasa Kwa wananchi sio majibu sahihi Kwa mpira wetu.

Laiti kama wakati huo mheshimiwa rais wa awamu ya nne angetengeneza miundombinu ya kutengeneza vijana washindani na miundombinu ya kuwasaidia kukuza na kuimarisha vipaji vyao haya matatizo yaliyopo leo yangekuwa yamepungua sana kama si kuisha kabisa.

Kuwekeza kwenye mpira wetu Kwa kuwa na benchi zuri la ufundi ni kujidanganya. Haisaidii chchote wala haiongezi chochote.

Hii ndio maana haishangazi kwamba wachezaji makocha marefa tulionao hapa ndani hawauziki sana huko nje.
 
Wewe si Mtanzania. Watanzania wengi hawafikirii hivi. Huwa wanatafuta wa kumwagia maji machafu na si kuangalia tatizo. Mpira hauendelei kwa hamasa... Ni uwekezaji wa muda mrefu. na hatujawahi fanya hivyo. Leo tunamlaumu Karia wakati yeye anafanya kazi yake. Michezaji yetu ndo haikui. Ikichezea team ya Taifa unana haina kitu. Tatizo siyo Karia. Ni Usimba na Uyanga. Ni kutowekeza kwenye mpira
 
Ata huko kwenyewe watu wao wanalalamika kuwa hawajitumi kama wakiwa kwenye vilabu vya ulaya.
Problem kubwa ni kwamba hatuwajali pia wachezaji wetu.

Match bonuses mara sijui kuwasafirisha wachezaji economy wakati wakiwa kwenye timu zao ulaya wanasagiri business class au ata private jet.
Ndugu mzabzab hawa tulio nao hata tungewajali vipi hata kama tukisema Kila mtu asafiri na jet yake na kiwango Cha kulipwa ajitajie mwenyewe haitasaidia Kwa sababu uwezo wao umeishia hapo walipofikia ndio maana tumeishia kuwa dalaja la kupandia wenzetu.

Ni uzwazwa uliopindukia kukazana kuingia gharama kubwa kuajiri makocha wenye CV kubwa na wanaolipwa hela nyingi waje wafundishe hapa.

Ni sawa na kununua mitambo mikubwa sana ya kisasa wakati una umeme hafifu alafu mitambo ikianza kusumbua uanze kulaumu mafundimitambo, nakuhakikishia utafukuza na kufukuza as long as hutatatua tatizo la udhaifu wa umeme wako hutatatua tatizo.

Naomba nieleweke siwalaumu wachezaji wetu naamini wanajituma na huenda wanatoa %100 ya uwezo wao but hivyo ndivyo tulivyowaandaa.

Kama tuna nia ya kuleta mabadiliko ya kweli ni lazima tubadilishe namna ya kuwaandaa watu wetu. Na hili linaihitaji wizara pamoja na TFF kukaa pamoja na kupeana majukumu ya namna ya kutengeneza kizazi kipya cha ushindani na weledi.
 
Back
Top Bottom