Leo ni Siku ya Chakula Duniani. Je Tanzania, Tumeipa Siku Hii Umuhimu Stahiki? Kilele, Kesho, Tujitokeze kwa Wingi kwenye Kilele, Pia Kuchanja Bure

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,561
Wanabodi

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Chakula Duniani, huu ni uzi wa swali na wito, jee sisi Tanzania, tumeipa siku hii umuhimu stahiki?. Japo siku yenyewe kimataifa ni leo, ila kilele, kwa Tanzania, kimepangwa kesho, kutokana na ratiba kugongana na tukio jingine muhimu zaidi ya Siku ya Chakula, lililotokea hapa Mjini Moshi. Hivyo natoa wito kwa wakazi wa Moshi na vitongoji vyake, tujitokeze kwa wingi kwenye kilele, hapo kesho, kwenye viwanja vya Pasua, pia chanjo ya Korona, inatolewa bure bure hapa viwanjani. Kuchanja ni Bure, shime wana Moshi, njooni kwenye maonyesho muone vyakula na pia tuchanje.

Mwaka jana, nilibahatika kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Njombe, na sasa nahudhuria maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani kwa mwaka huu, yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Pasua, mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Kitu ninachokiona kwenye maadhimisho ya mwaka huu, nikilinganisha na yale maadhimisho ya mwaka jana, ni vitu viwili tofauti. Maadhimisho ya mwaka jana yalikuwa na msisimko wa hali ya juu, maadhimisho ya mwaka huu yamekosa kabisa msisimko, wakati ndio yalikuwa na fursa ya kupata hamasa ya hali ya juu kutokana na maadhimisho hayo kuchangamana na ziara ya Rais Samia mkoani Kilimanjaro.

Leo tarehe 16 October, ndio Siku rasmi yenyewe ya Chakula Duniani, lakini kutokana na sababu za maalum, kilele cha maadhimisho hayo, kimesongezwa hadi kesho Jumapili, tarehe 17 October, kwanza katika maisha yangu yote ya miaka 30 ya uandishi wa habari, sikuwahi kuona maadhimisho ya siku yoyote ya kimataifa yakizongezwa mbele kutokana na tukio jingine, jee ni tukio gani hili kubwa zaidi ya Siku ya Chakula?!.

Hii inamaanisha Siku hii ya Chakula kwa mwaka huu, haikupewa umuhimu stahiki, na kwavile sisi binadamu wote tunaamini Mungu, tunaamini tumeumbwa na Mungu, na Mungu ndiye ametupatia zawadi ya uhai kwa kupuliziwa pumzi ya uzima, hivyo…
  1. Kitu muhimu nambari moja kwa binaadamu ni Mungu, The Almighty God, The Father, The Creator, who created us, and everything yaani Mungu ametuumba na kila kilichopo duniani na chake, tukiwemo sisi binadamu ni wa kwake na kwake tutarejea.
  2. Kitu muhimu nambari mbili ni hewa, tunayovuta, pumzi ya uhai, “the air that we breathe,” hii tumepewa bure
  3. Na kitu muhimu nambari tatu ni chakula, “the food that we eat, to live, to survive”, yaani ili kila kiumbe kiishi, ni lazima kipate hewa na chakula.
Sasa kufuatia umuhimu wa chakula kwa binaadamu, Umoja wa Mataifa umeiteua siku ya October 16, kuwa ni Siku ya Chakula Duniani, "World Food Day", kitaifa maadhimisho hayo kwa Tanzania, yanafanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro, na inaadhimishwa kwa maonyesho ya vyakula, na teknolojia mbalimbali za uzalishaji wa chakula katika viwanja vya Pasua, mjini Moshi.

Kutokana na umuhimu wa siku hii, serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro, ikaamua kulichagua eneo la Pasua, kuwa ndilo eneo stahiki la kufanyia maandhimisho hayo, na maonyesho hayo, hivyo mimi nami, kama Mtanzania mwingine yoyote, niko Mkoani Kilimanjaro, kuwaletea, kila kinachoendelea kwenye viwanja hivi vya Pasua.

Hapo katika viwanja vya Pasua, pamoja na mambo mengine yote, pia Chanjo ya Corona inatolewa bure, huwezi amini, kutoka na uhamasishaji duni, kuna siku nimekaa mahali niiangalia hema ya kuchanja, nilikaa zaidi ya masaa 3, hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza.

Mimi kama kawaida yangu, huandaa vipindi vya uhamasishaji, kwa kufanya mahojiano na watu mbalimbali na kuonyesha mambanda na kinachoendelea, kisha kurusha vipindi kwenye TV mbalimbali, hivyo siku ya ufunguzi, nikawahoji wakuu wote na wote wakakubali kuhamasisha watu wajitokeze kwa wingi. Kuna Mhe. Waziri mmoja akaahidi kujitolea ku facilitate vipindi virushwe kila siku kwenye TV, mimi kama mtayarishaji, kila siku natayarisha kipindi ila kwenye TV haviruki!, Mwaka jana kule Njombe, kila siku kipindi cha saa nzima, dakika 60 cha maonyesho ya Siku ya Chakula, kilirushwa kupitia vituo vinne vya TV, lakini sasa… labda kesho siku ya Kilele ndio Taifa litaweza kuona, ile kwenye lile tukio muhimu ya hii ziara, ni live mubashara, zinangurumishwa toka kila kona.

Sasa imetokea tuu kama zali, maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani mkoani Kilimanjaro, yamepata bahati ya mtende, ku concide ya ziara ya mtu mmoja muhimu, kufanya ziara ya kiserikali mkoani Kilimanjaro. Kwa vile ziara zote za kiserikali ni ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndio huratibu kwa kushirikiana na wizara husika, mgeni atembelee wapi na wapi, na kumpangia siku ya kuzungumza na wananchi. Sasa kwa vile ugeni huu ume coincide na Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani, sasa kufuatia umuhimu wa Chakula kwa binadamu na kwa nchi yetu, hili ni ombi langu kwa serikali ya Mkoa, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, na Wizara ya Mifugo, mleteni mgeni huyu viwanja vya Pasua. Tena ningekuwa mimi ndio RC wa Kilimanjaro, ile siku ya mgeni wetu kuzungumza na wana Moshi, ningempangia azungumzie viwanja vya Pasua, ili pia wana Moshi na wana Kilimanjaro, wajitokeze kwa wingi, sio tuu kumsikiliza mgeni wetu akizungumza na wana Moshi na wana Kilimanjaro, bali pia atahamasisha, wana Moshi na Wana Kilimanjaro, kujitokeza kwa wingi, kuchanja.

Hivyo huu ni wito wangu kwa RC wa Kilimanjaro, Waziri wa Kilimo na Waziri wa Mifugo, kufuatia umuhimu wa chakula kwa uhai wa binaadamu na viumbe wote, ambapo baada ya umuhimu wa Mungu aliyetuumba, na pumzi ya uhai tunayoivuta, chakula ndicho kitu muhimu kuliko vitu vingine vyote, hivyo angalau leo siku ya mwisho, tuitendee haki siku ya Chakula, tuipe umuhumu inaostahili, leo kwenye kilele cha maadhimisho haya, turushe live ili angalau Watanzania waone umuhimu wa siku ya chakula duniani.

Paskali,
Pasua, Moshi,
Kilimanjaro.
 
Waziri aliyekuahidi ku “facilitate” vipindi virushwe kila siku kwenye TV ni Mkenda? If so, kwanini usimuulize imekuwaje ahadi yake haijatimilizwa?
 
Pascal hata sikujua kama leo ni siku ya chakula duniani ila nilikuwa na taarifa za ziara ya mheshimiwa rais mkoani Kilimanjaro tangu jana.

Kweli naungana nawe kuwa siku hii haikupewa umuhimu wake na wala hakuna uhamasishaji wowote hili ni kosa kwa wahusika kuanzia wizarani.

Hongera Pascal kwa kuliona hilo na kulisimamia kidete.
 
Chamuhimu tuzalishe chakula kwawingi,sio kung'ang'ana nakasiku kamoja walikoamua wazungu.
Usiandikage mambo meeeengi ku-adress kakitu kadooogo kwanza sio cha kisiasa kiivyo
 
Waziri aliyekuahidi ku “facilitate” vipindi virushwe kila siku kwenye TV ni Mkenda? If so, kwanini usimuulize imekuwaje ahadi yake haijatimilizwa?
Mkuu jmushi1 , waziri aliyeahidi sio Prof. Mkenda, huyu ni for real, akiahidi anatekeleza, ila kiukweli kabisa, kuna baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita, ambao mama anaendelea nao, ni mizigo! Maneno mingi, vitendo 0!. Ila na mimi pia najaribu kuvaa viatu vya huyo waziri, naamini kabisa, alipoahidi, aliahidi kwa nia njema kabisa, with a solid promise, lakini ulipofika wakati wa kuiweka hiyo commitment in black and white, ndipo alisita, baada ya kuona the figures of what it takes. Ila mimi, ninae, ahadi ni deni, leo na kesho lazima vipindi viruke, ila ikitokea ameshindwa, nitamshauri atengue ahadi!.
P
 
Hivi kila makala yako lazima iwe ndefu Pascal Mayalla ??
Mkuu Bayyo , kwanza mimi ni story teller, ila pia baadhi ya makala zangu, directional and targeted, ili ku hit the bull, lazima ni beat sana around the bush, ili watakao elewa wawe ni wale walengwa tuu, hivyo nawaanzia mbali, nawapeleka kule hadi mbinguni kwa Mungu, kisha nawashusha duniani nawazungusha zungusha, kila ndio nawawasha. A shot cut is always a wrong cut, a long way ndio yenyewe, japo slow, but sure!.
P
 
Back
Top Bottom