Kommando muuza madafu
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 2,698
- 5,915
Na declare interest mimi ni mdau wa usafirishaji Tanzania.
Lengo la kuanzisha huu uzi sio kuharibu biashara au maisha/ajira za watu ila ni kuokoa maisha ya watanzania wanaokufa kila siku kama panzi kwa uzembe na ujinga wa hawa madereva.
Mimi ni mkazi wa Mkoa wa Mbeya na huwa nafanya kazi za usafirishaji na mara nyingi huwa nakuwa barabarani na muda mwingine huwa pale Uyole stendi, Nane nane stendi au kule Ipogolo Iringa na Msamvu stendi pale Morogoro.
Kumekuwa na tabia ya ushabiki wa wapiga debe kwenye hizi stendi zetu kuhusu nani anakua wa kwanza kufika akitokea sehemu gani. Mfano kwa mabasi ya Dar-Mbeya pale Uyole kumekuwa na ushabiki huo. Mara nyingi vijana hawa wapiga Debe humu katika hizi stend zetu huwa na "team" na hujichangisha pesa na kufikia kiwango fulani mfano Tsh 200,000/= au 300,000/= hivyo hukubaliana. Gari litakalo wahi kufika dereva atapewa 100,000/= na hiyo nyingine 100,000/= au 200,000/= itapewa timu ya Gari iliyobet kuwa litawahi kufika stendi.
Kitendo hiki kipo kila stendi nchi hii na nimekishuhudia kwa macho yangu katika stendi za Uyole na nanenane Mbeya, Igumbilo Iringa, Msamvu Morogoro naBabati Manyara. Hali hii husababisha madereva kukimbiza na kukimbizana barabarani bila sababu yoyote. Wamekuwa wanafanya overtaking za hovyo bila kujali usalama wao na wa abiria zao.
Kuna siku nilisafiri toka Iringa naenda Mbeya na nilikuwa kwenye gari binafsi, tulipitwa na Newforce na nyuma yake ikaja Sauli. Walikuwa wana kimbizana. Sauli akitaka kumpita Newforce, Newforce hampi nafasi ya kupita na kama kuna gari linakuja mbele itabidi lile gari la mbele likae pembeni ili wao wapite. Hali hii ni mbaya sana na vyombo vya usalama vipo na vinaona.
Leo nimeletewa dokezo hili ili wewe mtanzania mwenye nia njema ukataji madereva wa mabasi wanaofanya huo ujinga kwa kuendesha rough ili kuwahi Beijing za kwenye mastend. Naamini vyombo vya usalama vipo humu na vitasaidia kuchukua hatua na kama hawatachukua hatua, damu za watanzania wenzetu zinazomwagika hukunwao wanafurahia kukusanya elfu 5 ziwe juu yao.
1. Mi naanza kumtaja yule dereva mwarabu mwembamba wa Kapricon Coach toka Mbeya kwenda Arusha.
2. Wengine ni madereva wote wa Sauli na newforce za Dar-Mbeya/Songwe.