Tuwafiche wapi watoto wetu wa kike?

Tuwafiche wapi watoto wetu wa kike?

Inabidi ifike mahali tubadilishe mila na desturi zetu kutokana na mabadiliko yaliyopo sasa ya sayansi,teknolojia pamoja na manzingira kama hilo halitawezekana basi zile mila zenye kuleta shaka kama unyago/jando tuziache kabisa afu jamii kibao wanaishi bila mila hizi na wanafanikiwa na vijana wanakuwa wakiwa wanajitambua !!!! TUBADILIKE TUNAISHI KARNE YA ISHIRINI NA MOJA.
 
Ila hili la kubakana watoto naona linasambaa achana na huyo alieonja utamu akakataa shule,
unakuta kikundi cha vivulani vidogo vinavizia katoto ka kike wanataka kubaka,
sijui watoto wanajifunzia wapi!
Au ndo madhara ya kulala chumba kimoja na wazazi pamoja na kuangalia picha za video!!
 
inabidi tuziangalie upya tujiulize wapi tunakosea
hili ndio la kufanya kwa sasa
sio kwamba hatujui wapi tunakosea tatizo ni je tunakubali tunakosea?
 
Sisi siku si tunajifanya kila mtu analea mwanae peke yake?! Ndio hapo tutatia akili. Back in the days when kids were collectively taken care of by the society things were much better. Mtoto hawezi kufanya ujinga kirahisi maana anajua atakula bakora hapohapo na asipokaa vizuri na nyumbani pia atakula bakora. Siku hizi kitoto kikiguswa kdogo kinamama wanakuwa wakali kama pilipili, sasa kakipigwa mtungo utashangaa?

Tumefeli au tunaelekea kufeli kama jamii. Inabidi tujiangalie upya.
 
wazazi wachizi tuu...mtoto mpaka kupinda hivyo ni kosa la wazazi
 
Mtoto wa miaka 12 hawezi kuwa kashindikana. Lawama kwa wazazi wake ambao wameruhusu hali hiyo.

Mtoto ni malezi tu, haya mambo yapo enzi na enzi ila malezi ya wazazi kwa mtoto ndio chimbuko la yajayo kesho
 
Wewe Sio pwani tu Njoo mitaa ya villa Mwanza ujionee majanga,huku Sio std4 huku hawajaenda xule kabisa vitoto vya miaka 9 mibaba inaponea huku so nijanga lakitaifa br tuombe sana mungu.
Dah habari hizi zinaniuma sana mimi mzazi kwa jinsi tunavyozaa kwa uchungu at the end of the day mtu anaharibu mtoto wako! Eeh Mungu tusaidie
 
Ila hili la kubakana watoto naona linasambaa achana na huyo alieonja utamu akakataa shule,unakuta kikundi cha vivulani vidogo vinavizia katoto ka kike wanataka kubaka,sijui watoto wanajifunzia wapi!Au ndo madhara ya kulala chumba kimoja na wazazi pamoja na kuangalia picha za video!!
Dah kuna haja somo la ukimwi lianzie kufundishwa chekechea! Maana tulipo Sasa sio pazuri
 
Mtoto wa miaka 12 hawezi kuwa kashindikana. Lawama kwa wazazi wake ambao wameruhusu hali hiyo. Mtoto ni malezi tu, haya mambo yapo enzi na enzi ila malezi ya wazazi kwa mtoto ndio chimbuko la yajayo kesho
Huyu mtoto hadi polisi kapelekwa lakini wapi!! Ni kwamba kashakubuhu
 
Imeandikwa: "Usimnyime mtoto kiboko, Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee" Sasa weewee miaka yoote hujjui nini malezi ya mtoto kwanzia kifamilia,kimungu,kimazingira,kidigitali,kiheshima nk leeo kavuja umeita ngoma hao wangoma wanakuja kumfunza nini? Mimba ubebe wewe na mtoto umzae mwenyewe mafunzo ya namna atakayokuja kuishi na kulea kwanini apewe na mtu mwingine? Narejea tena Mlee mtoto ktk njia impasayo,naye hataiacha hata hatakapokuwa mzee sasa wewe umeona njia impasayo ni kumwekea kigodoro mcheze uchi,mfanye ya kufanya adharani alafu utegemee akufelishe tena ktk somo ulilomletea alelewe nalooo? Aaaaaaggggghhhr its very sad eti huyu mtoto kanishiiiinda. Samaki mkunje angali mbichi
 
Habarini!?

Nimesikitishwa na tukio nililoliona wiki hii kwenye pitapita zangu ni binti Wa darasa la 4 amekataa shule akitaka aendelee na maisha ya kujiuza!

Ni binti ambae kwa mahesabu ya haraka atakuwa na miaka12 na kamwili kakuvutia kalikoletwa na kuvunja ungo mapema!

Baada tu ya kuvunja ungo ndipo akafundwa yale mambo ya pwani kuhusu ukubwa na tabia zake tangu hapo zikawa si nzuri!

Mtoto huyu kulala kwenye vigodoro ni kawaida kwake kupigwa mitungo na mengineyo!

Je hizi tamaduni zetu hatuwezi kuziacha? Au kupunguza makali ya mafunzo? Mbona watoto wetu wanaharibikiwa baada ya kufunzwa?

Tuwafiche wapi watoto wetu Wa kike?

Nawasilisha.

Swali langu ni dogo tu, wateja wa huyo mtoto ni rika gani?? Au ni vitoto vyenzie??

Kama ni watu wazima badi hao ndiyo wa kulaumu, angekosa wateja asingekataa shule huyo mtoto!
 
Acha wahalibike sababu ya digital

Weee shiindwa na ukakamaee! Mtoto wa mwenzio ni wakwako na uwezi juua sumu atakayomwaga mtoto huyo yaweza fika na kwa wakwako. Wazazi tukae chini upya tuzungumze na wanetu kbl mambo hayajawa maboo. Mbona sisi hatukuwa hiviii ni kwa 7bu kila mzazi alikuwa mzazi wako na ukifanya ovyu,bbaya lolote anaweza kukukemea mpk kukuchapa pia na uthubutu kwenda kusema nyumbani maana ukisema tuu lzm ule tena kichapoo alafu huku umeshikwa mkono unapelekwa kwa aliyekuchapa, wee mbona utakoma tenaa. Sasa hapo utake usitake kila mtoto anafata straigh line mtaa mzimaa. Si siku hizi ukizunguka tuu nyuma ya nyumba unasikia mtoto wa jirani anaboromosha matusi mpk wewe mtu mzima ndo unafanya kumkimbia. Tuwalee watoto wetu ktk misingi ya kumjua Mungu. Siku hizi sunday school hazina watoto eti kisaa mchana jua kali nk wenye sundy school za asb mzazi mwenyewe haendi kanisani so mtoto anakua yupoyupo tuu anajilea mwenyewe. Wamadrasa ndo hivyo tena eti muda huu akanichotee maji.
 
Mlee mtoto katika njia ipasayo naye hataiacha ata atakapo kua mzee..!
Mengi utayaona sasa kutokana na digital ila hakuna jipya chini ya jua..💏
 
Back
Top Bottom