Tuubatize jina gani msitu wa pande?

Tuubatize jina gani msitu wa pande?

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,388
Reaction score
683
Habari zenu wana jamii, nimetafakari sana na kutaka kudadisi na kuufahamu huu msitu wa PANDE. Mara ya kwanza nilianza kuusikia huu msitu pale ambapo polisi waliwamiminia risasi za visogo wafanya biashara wawili wa madini pamoja na dereva tax wao. Pia nimedokezwa kwamba wakufunzi wa TISS hasa waliopo katika ile kambi ya BUNJU hupelekwa pale kufanya mazoezi yao. Kiongozi wa madaktari nchini Dr Ulimboka baada ya kukamatwa na watu wanaodhaniwa maofisa usalama wamempeleka na kumtesa katika msitu huo. Ameharibiwa sehemu za siri na kungolewa meno, pia amevunjwa mbavu. Haya mateso niyakufunzwa kabisa. Je msitu huu una majoka na wanyama wakali?. Haya ni miongoni mwa maswali mengi ninayojiuliza kichwani. Wana jamvini mnaonaje tukiubatiza jina msitu huu?. Hebu pendekeza hapa jina linalofaa kuitwa msitu huu.
 
Mkuu inahuzunisha. Napendekeza uitwe: MSITU WA DAMU

Humo ndani zimemwagwa damu za wenzetu waliouwawa kinyama tangu enzi za utumwa wa Mwarabu.
 
...msitu wa dhuluma...
...msitu wa kifo...
...ukipona bahati...
...kitanzi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom