RIWAYA: Msitu wa Solindo

RIWAYA: Msitu wa Solindo

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
3,450
Reaction score
6,211
MSITU WA SORONDO

Mtunzi Richard Mwambe

Simu 0754740668

1
Chau cafe Chau cafe
Amata Ga Imba aliendelea kunywa kahawa yake polepole kana kwamba hana
shughuli nyingine ya kufanya kwa siku hiyo, kichwani akiwa na mawazo mengi sana
akipanga na kupangua juu ya maisha yake ya sasa na baadae, alipotahamaki hata kashata
alizokuwa akila zilikwisha moyoni akajiuliza kama aliagiza kashata au ameshazila
zimekwisha! Hilo nalo likawa jambo jingine ambalo lilikosa jibu kabisa.
“Chausiku!!” aliita kwa nguvu kana kwamba aliyekuwa anamuita alikuwa umbali wa
kilomita kadhaa lakini kumbe wote walikuwa hapo jirani tu.
Watu walishtuka kwa sauti hiyo hata wengine walidiriki kumtupia maneno yasiyostahili
“Samahani waheshimiwa!” aliomba msamaha
“Samahani nini mjinga wewe!” mmoja alitamka kwa hasira
“Wengine tuna BP utatuuwa bure sura ka Sokwe!” mwingine aliongeza
Amata aliumia sana moyoni kwa tukio lile, akainamia mezani, akatikisa kichwa kisha
akasimama kwa hasira na kuelekea eneo la kunawia mikono, akajitazama kwenye kioo,
akatabasamu, kisha akageuka na kurudi alipoketi kwanza.
Kabla hajaketi alisikia sauti nyuma yake
“Umejiona ee? Ka sokwe, tena wa Gombe!” mmoja alimkejeli, wengine wakaangua
kicheko cha dharau na kupiga miluzi.
Hasira za ghafla zikamrudia Amata, akageuka na kuelekea upande ambao sauti ile
imesikika
“Nani aliyesema vile?” aliuliza kwa kung’aka, wakacheka tena
“Ukimuona utamfanya nini? Fala wewe mtoto wa porini!!” mwingine alisema na
wengine wakaangua kicheko. Amata alipiga hatua mbili mbele na kumkunja shati yule
aliyesema maneno hayo akamuinua kwa nguvu akamrusha chini, huyo akaanguka chini
mzimamzima kama gunia, jamaa akanyanyuka kwa hasia na kumvamia Amata, Amata
akamdaka na kupiga vichwa vitatu vya nguvu akamsukuma kidogo na kumrushia
makonde kama mvua, kijana yule alichanganyikiwa hata hakuweza kujibu mashambulizi
alianguka chini mara ya pili.
“Ameua! Ameua! Ameua!” kelele za watu zilijaza mgahawa ule mara watu wakajaa
wanataka kumshika Amata. Yule kijana bado alikuwa chini hajitambui kwa kipondo cha
ghafla alichokipata. Amata aliruka kutoka aliposimama akatua juu ya meza na kutaka
kutoroka kwa kupitia dirishani, watu walimgombania kwa kumshika shatia wengine
suruali, masikini Amata shati lake lilichanika vibaya akabaki na fulana ya ndani na
kuwaachia shati wananchi wenye hasira, alliruka kupitia dirisha la mgahawa huo na
kudondokea kwenye lundo la mawe kwa kutanguliza mkono, alihisi maumivu makali ya
mkono lakini alipogeuka aliona watu wale wanakuja pale alipo, akanyanyuka na kutimua
mbio
“Huyo huyo! Kamata muuaji huyo!!” kelele za wananchi wale zilikuwa kama kichocheo
kwa kijana Amata kuongeza spidi. Mara kwa mbele aligongana na pande la mtu na
kuangushwa mbali, alinyanyuka na kuanza kukimbia tena, watu walitoka majumbani na
kumuunganishia kama kawaida ya wananchi. Mbio ziliendelea na wananchi nao
hawakuchoka, alitokea kwenye wigo wa nyumba la! Hapakuwa na njia aliruka na kupanda ukuta kisha akatokea upande wapili na kupanda tena alitua chini kwa miguu
yake mikakamavu na kutimua mbio lakini la haula! Alipokuwa akijaribu kuvuka kichaka
kidogo katika eneo hilo alijikwaa vibaya na kuanguka chini, mchezo umekwisha. Watu
wakamkamata na kuanza kumpiga hata kumuumiza vibaya, Mungu si Athumani polisi
waliwahi kumuokoa kutoka kwenye mikono ya watu wenye hasira.
“Tuachie huyo tummalize! Muuaji huyo!” watu walipiga kelele na wengine bado
walidiriki kurusha hata mawe ambayo baadhi yaliwapata askari wale. Askari mmoja
akafyatua risasi hewani na watu wale wakatawanyika kwa woga wakikimbia uku na huku
wengine wakianguka na kukanyagana vibaya. Amata alichukuliwa mpaka kituo kidogo
cha polisi akiwa hatamaniki kwa jinsi alivyolowa damu hata fulana yake aliyobaki nayo
baada ya kuwaachia shati watu wale haikujulikana kama ni nyeupe au nyekundu, juu ya
jicho lake la kushoto jeraha kubwa lilikuwa bado linavuja damu, mkono wake umevimba,
kucha ya kidole gumba cha mguu wa kushoto haikujulikana hata imeng’okea wapi.
Askari wale walimpiga Tanganyika jeki bila huruma wala kujali kuwa mwenzao
ameumia namna ile wallimkokota tena na makofi juu mpaka kituo kidogo cha polisi na
kumlundika selo.
Ndani ya chumba kidogo cha selo katika kituo cha polisi cha kijiji wahalifu walijazana
mpaka hewa haikutosha kabisa, walichoka na hata wengine kukosa nguvu, kupoteza
fahamu kwa kukosa hewa ya kutosha. Amata aliingia kwenye selo hiyo katika hali ile
aliyokuwanayo, akakaribishwa na joto na harufu mbaya haja kubwa na ndogo
zilizochanganyika, mwanga hafifu uliopita katika kadirisha kadogo kenye ukubwa wa
mlango wa banda la njiwa ndio pekee kalikokuwa kanatoa faraja kwa binadamu hawa
waliokuwa na makazi ya muda ndani ya chumba hiki, wote walikuwa na sura za kutisha
ambazo bila kuuliza utajua kuwa sasa nimeingia kuzimu.
Ucku huo ulikuwa mrefu sana kwa Amata, mawazo mengi yalitawala kichwa chake,
maumivu makali yaliusumbua mwili wake, alijituliza kimya kwenye moja ya kona za
kijichumba hiko huku akisikia kichefuchefu kama mama mjamzito kila mara alitamani
kutema mate lakini atatemea wapi watu wamejazana hata wengine wamekaa kwa
kupakatana mh! Mawazo yaliendelea kumsonga hata usingizi mwepesi
uliokatishwakatishwa kwa nyimbo za kuchukiza za mbu masikioni mwake ulikuja na
kuondoka, aliwaza jinsi anavyoishi kwa tabu bila Baba wala Mama wa kumtetea, japo
aliachiwa shamba kubwa na kibanda cha kuishi lakini hakuujua uelekeo wa maisha yake,
“alikuwa analinga na Baba yake, ataona sasa” wengi walisema hivyo, Amata aliona ama
jamii yote haimtaki, dunia imemchukia au ulimwengu unampa adhabu?
“Kwa nini mimi?” alijiuliza uliza moyoni mara kwa mara hasa alipokuwa kwenye
kibanda chake huko shambani kwao ambako alipitisha maisha yake ya ujana tangu
wazazi wake walipofariki yeye akiwa na umri wa miaka michache nyuma, mama yake
aliuawa na Simba alipokwenda kuchota maji nje kidogo ya shamba lao ijapokuwa Baba
yake alijaribu kumtetea dhidi ya Simba hao wakali wenye uchu wa nyama lakini hakufua
dafu ‘kidole kimoja hakivunji Chawa’ alipiga kelele za msaada lakini hakuna aliyekuja.
Lakini Baba yake alikufa baada ya kuugua kwa muda mfupi miaka michache baadae.
Kila aliporudiwa na picha hizi alilia sana na kujiona kuwa yeye ni binadamu mwenye
mkosi, akuwahi kuwa na kaka wala dada isipokuwa ndugu tu ambao pia hawakuwa na
msaada nae kabisa. Amata!!!” aligutushwa na sauti kali ya askari iliyotokea kwenye kadirisha ka mlango wa
selo hiyo.
“Afande!” aliitikia kwa uchovu na kujaribu kujiinua kutoa alipokuwepo lakini alijikuta
anapata kizunguzungu na kuwaangukia wenzake waliokuwa hapo. Alifika mlangoni pale
kwa shida mbele yake alimuona msichana mrembo sana kasimama, mrefu wa wastani
maji ya kunde, alivalia vizuri suruali yake ya kitambaa nyeusi na blauzi yake nyeupe
huku shingoni kafunga skafu yenye mchanganyiko wa rangi, nywele zake fupi
zilizokatwa kiumahili na vinyozi wanaojua kazi yao, kiatu chake kirefu kilimfanya
aonekane kuwa ni mrembo anayetunzwa na pedeshee fulani. Dada yule alijivuta taratibu
mpaka kwenye dirisha lile. Amata alipokea pumzi safi iliyonukia na kuvutia kutoka kwa
mrembo huyo, hakuamini anachokiona ni malaika au binadamu, aliduwaa, akapigwa na
bumbuwazi, mikono yake ikiwa imeshika nondo mbili zenye kutu alijikuta anaishiwa
nguvu. Mrembo yule alishika nondo zile kwa kubana mikono ya Amata akaiangalia sura
ya Amata iliyochoka na kukaukiwa na damu..
“Saringo! Naitwa Saringo” almwambia Amata kwa sauti ya chini
“Hunijui, ila utanijua punde tu” aliendelea “Haujaua ila umeumiza vibaya, sasa unastahili
zawadi kwa kazi uliyoifanya bila kujua, na zawadi hiyo utaipata ukimaliza kazi yako”
Saringo alishusha pumzi na kumwangalia Amata usoni na kumuona jinsi
alivyochanganyikiwa, akaendelea kumwambia mashairi yake yasiyoeleweka kwa mtu
mwenye akili timamu, sasa kwa kukunja sura akamwambia Amata “ Lazima ufungwe,
uishie jela!” akageuka nakuondoka zake. Amata akazidi kulowa jasho, maswali yasiyo na
majibu yalimzunguka tena ‘nilijua malaika mwema kaja kuniokoa kumbe malaika mbaya
wa mauti kanitembelea’ alijiwazia na kuanza kulia. Amata hakupata jibu mwanamke yule
ni nani, na anataka nini, utata. Asubuhi ile kalandinga liliwachukua mpaka mahakama ya
kijiji, jalada la Amata lilikuwa la tatu kuitwa, taratibu akiwa na pingu mikononi
aliingizwa katika chumba cha hakimu na kusomewa mashitaka ya kudhuru mwili,
alijikuta hana cha kukana isipokuwa kukubali, kesi ikahairishwa mpaka baada ya siku
kumi na nne. Walipokuwa wanarudi kwenye kalandinga alimuona binti yuleyule akiwa
amesimama katika kundi la watu waliokuja mahakamani hapo, muonekano wake ulikuwa
tofauti na wote pale kwani ndiye aliyevaa nadhifu kuliko wote ‘huyu ni nani?’ Amata
alijiuliza hakupata jibu, moyoni alimlaani kuliko anavyomlaani shetani walipogongana
macho Amata alitema mate chini na kumuonesha kidole cha kati. Mara alijikuta
anatandikwa kofi la kisogoni au vijana huita ‘mbata’
“Panda juu unatuchelewesha!” sauti kali ya askari ilisikika. Amata na wengine
wakapanda na lori lile kuondoka kwa kasi.
[emoji814][emoji814][emoji814]
“Una mpenzi mzuri sana, mtoto kaumbika kama Malaika, he he he mbona wewe na yeye
hamuendani kabisa au wewe ni mchunga ng’ombe wao!” mmoja wa mahabusu
alimuuliza Amata kwa sauti mbaya ya kukwaruza isitoshe inatisha. Amata aligeuka na
kumwangalia akatabasamu kwa sura iliyochoka
“Simjui hata anatoka wapi” alimjibu
“Kwangu ni kama shetani tu yule, anataka kuniua, kunifunga, hilo ndilo limemleta hapa”
aliendelea kumueleza yule mahabusuKwa nini aje kukuona asubuhi yote ile? Au kuna uhusiano wowote na kesi yako?”
aliendelea kudadisi mahabusu yule,
“Sijui chochote! Mbona maswali mengi umempenda? Mfwate basi, mi nshakwambia
smjui! Yule ni shetani tu” Amata alijibu kwa hasira kidogo na mahabusu yule
hakuendelea na maswali yake.
Kesi ilitajwa tena baada ya siku kumi na nne, Amata na wenzake wakiwa na pingu
mikononi waliingizwa katika chumba maalumu cha mahabusu mahakamani hapo, Amata
alisimama karibu na mlango, mara ghafla alipata mshtuko mkubwa, hakuamini
alichokiona nje ya jingo hilo, akakaza macho kutazama kwa makini akayafikicha kidogo
aone labda alikuwa ndotoni lakini hapana alichokiona ni sahihi na macho
hayakumdanganya. Hakutaka kupoteza hata sekunde katika lile alilokuwa anliona lakini
bahati mbaya hakuweza kusikia kinachozungumzwa. ‘Yule sio Chausiku?’ alijiuliza
moyoni lakini pia hakutaka kuyaamini macho yake.
Chausiki Binti Saidi, msichana mfupi mwenye afya njema kibonge, mmiliki wa mgahawa
unaojulikana kwa jina la Chau Café, msichana huyu ambaye amekuwa pamoja na Amata,
wamesoma shule moja ya msingi kijijini hapo na kucheza michezo mingi ya utoto
pamoja, yeye alifanikiwa kufika japo darasa la saba wakati Amata alifukuzwa shule
akiwa darasa la tano kwa kisa cha kumpiga mawe mwalimu wake wa darasa. Maisha
yalimwendea kombo Amata kielimu japo alijitahidi sana katika rasilimali alizoachiwa na
marehemu baba yake Chausiku alimpenda kutokana na bidii yake katika kazi. Watu
walimbeza sana Chausiku kwa jinsi alivyoonesha upendo kwa Amata hii ikapelekea
Chausiku kutokuwa karibu sana na kijana huyu ambaye japo aliugusa moyo wake,
pamoja na ukorofi lakini hakuweza kumtoa moyoni mwake, moyoni mwa Chausiku
Amata alikuwa kama maji yatuliavyo mtungini yasipoguswa. Vijana wengi walipenda
kwenda mgahawani kwake japo tu roho zao zisuhuzike kwa kumuona binti huyu, wapo
waliomdanganya kwa pesa na vitu mbalimbali lakini msimamo wake thabiti
haukumfanya ayumbishwe na vitu vyote hivyo bali aliuacha moyo wake utue kama
kipepeo atuavyo katika ua alilolichagua.
Chausiku aliumizwa sana na kisa kilichomkuta Amata, alijua kuwa Amata kwa hali
aliyonayo asingeweza kupata msaada wowote wa kisheria au utetezi katika kesi yake,
alijitahidi kufanya kila awezalo ili tu amsaidie Amata katika hili.
Jalada la Amata liliitwa, polisi walimtoa katika chumba kile akiwa chini ya ulinzi na
kupelekwa katika chumba cha mahakama, akiwa anapita katika kikorido kidogo cha
jengo hilo alisikia sauti nyembamba tamu ikipenya masikioni mwake, ilikuwa si ya
mwingine bali Chausiku ambaye alikuwa akilia kwa machozi mazito “Mnyezi Mungu
akusaidie” ni maneno aliyomwambia, Amata aligeuka kwa kuiba, alifarijika kuona
kumbe wapo katika binadamu awa hawa wanaompenda, kidogo alijisikia mtu kati ya
watu.
Kesi ya Amata ilikwisha alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi sita jela.
Waliondolewa mahakamani na Amata alianza kutumikia kifungo chake huko gereza la
kilimo Sogera, gereza lenye kazi ngumu, kulima, kupanda, kuvuna, muda wote mkiwa
katika matope, maji machafu, mnakula chakula huku mnanyeshewa na mvua, mateso!.
 
MSITU WA SORONDO 2

Mtunzi Richard Mwambe

Simu 0754740668

Gereza la Sogera Gereza la Sogera
Sogera ni gereza kubwa sana lililoko nje kabisa ya mji wa Mgosola, lilijengwa zamani na
wajerumani wakoloni juu ya mlima. Limezungukwa na ukuta usiopungua mita ishirini
kwenda juu na chini ya ukuta huo kumepandwa mikonge kuzunguka gereza zima, katika
kona zote na katikati ya pande zote kuna vibanda vipatavyo nane juu kabisa vyenye
walinzi wawiliwawili kila kimoja wakiwa na silaha kali, juu ya ukuta kumezungushwa
waya maalumu ambao una umeme kwa masaa ishirini na nne, doria haziishi nadani ya
gereza hili lenye kila aina ya sifa. Amata alifungwa ndani ya gereza hilo, hakuwahi
kufikiri hata siku moja kama angefika mahali pale daima alisikia hadithi tu watu
wakisimulia na kusifia sifa mbaya za jingo hilo, aliona kuwa sasa ndio amefika mwisho
wa maisha yake, jehanum ya duniani, alikata tama ya kuona tena kijiji chake
alichokipenda, watu aliyowapenda, michezo aliyoipenda, shamba lake aliloachiwa na
wazazi wake, kila kitu kwake aliona kimefika mwisho na kama kuna kitu alichokichukia
tangu muda huo ni Saringo msichana mrembo aliyemhakikishia kufungwa na kuozea jela.
‘Shetani huyu! Shetani mkubwa! Aombe nisitoke ila nifie humu, laiti nikitoka
namkatakata vipande na nyama nawapa mbwa wale, naapa’ Amata alijiwazia kwa hasira
na uchungu. Akiwa bado ameketi kwenye kigodoro kidogo alisikia sauti ya king’ora
hakujua kinahashiria nini alipochungulia katika kadirisha ka mlango aliona wafungwa
wote wanakimbilia kwenye uwanja mkubwa, mara mlango wake ukafunguliwa
“haya mfungwa kwenda kwa wenzio haraka!!” sauti ya askari ilimfanya atoke mbio,
alifika na kukaa katika mstari paamoja na wengine. Akasimama askari mmoja katikati
akiwa na kipaaza sauti “leo ni sherehe!!!!” alitangaza “tunakaribisha wageni na pia
tunapunguza wengine” aliongeza, uwanja ulikuwa kimya sana alisikika yeye peke yake
“wale wote waliofika hapa peponi leo waje mstari wa mbele haraka!” alitoa amri
Amata na wenzake saba walisogea mbele wakiwa bado na pingu mikononi, wakasimama
mbele, hapo waliweza kuona kila kitu kwa vizuri zaidi.
“kwanza napenda kukukaribisheni hapa Sogera, sehemu takatifu ambayo huna budi
kuacha ujinga wako!” aliendelea kusema
“Mnaowaona hapa wote ni watoto wazuri wenye roho nzuri wasiopenda ujinga!” alisema
huku akitafuna big G yake, askari huyu mrefu mpana mwenye tambo la kiaskari hasa
aliongea maneno haya bila kuonesha tabasamu wala kutikisika, akiwa na bastola yake
kiunoni na sare yake ya magereza iliyomkaa vizuri alionekana si wa kuchezea.
“Nyie was*nge! Mliokuja hapa wiki hii, hii ngome ya mjerumani, ukitaka kuishi vizuri
fuata amri kumi za hapa ndani, ukiambiwa inama, inama, usilete ubishi kwani waliopo
hapa ni binadamu kama wewe wana mahitaji”alisema askari yule.
Amata aliposikia maneno hayo alisisimka na mwili ulikufa ganzi, askari yule
aliendelea…
“Usije kujaribu kutoroka, zawadi ya kutoroka ni kama hii mtayoiona sasa!!!” akageuka
nyuma akapaza sauti “Afande, lete hao!” mara wafungwa wanne waliletwa wakiwa
wamefungwa kamba mikononi wakiburuzwa kama magunia, walijaribu kukukuruka
lakini haikusaidia. Pale aliposimama askari yule palikua na jukwaa kubwa lenye kitu
kama goli la mpira, lakini juu yake kulikuwa na kitu tofauti, ubao mnene mkubwa wenye
tundu la nusu duara lakini katika tundu lile kulikuwa na kitu kilichokamilisha duala lile
kiling’aa sana kana kwamba kuna chuma katikati, stailess steel, na upande wa chini wa
goli hilo kulikuwa na ubao mwingine kama ule lakini huu kwenye tundu lake haukuwa na
kile kitu kama chuma. Mfungwa mmoja aliburuzwa mpaka pale na kufungwa kwa kamba
katika goli lile akielezewa chini shingo yake ikiwa imepachikwa kwenye ile nusu duara
mwili ukiwa upande wa pili na kichwa upande mwingine, mara kibao kile cha juu
kilifyatuka na kuteremka kwa kasi, akiwa bado kapigwa na bumbuazi Amata alihisi kitu
kama jiwe la duara kikimgonga miguuni na kuhisi maumivu, alipoangalia chini ni kitu
gani hakuamini macho yake, kichwa cha mtu kinachovuja damu mbichi kikiwa
kimekatwa kutoka kwa mfungwa yule aliyefungwa pale golini, Amata alichanganyikiwa
hajawahi maishani mwake kuona kichwa kisicho na kiwiliwili, akaanza kukimbia.
“Kamata huyo!” amri ilitolewa, askari wawili walianza kumkimbiza, alipigwa ngwala
lakini kwa umahiri mkubwa Amata aliruka samasoti na kutua kwa miguu miwili kabla
hajakaa sawa alistukia kamba iliyorushwa kwa ustadi ikimfunga shingoni, akageuka na
kurusha ngumi iliyompata askari yule sawia shavuni, kabla hajakaa sawa alipigwa teke
moja la kifua na kuyumba akaangukia katika mtaro wa maji machafu akatoka kwa haraka
alipata pigo lingine maridadi lililompoteza kabisa akaanguka tena, askari wale
wakamfunga kamba na kumburuza mpaka uwanjani naye akawekwa pamoja na wale
wanaosubiri kunyongwa, akafunikwa nguo nyeusi kichwani asiweze kuona chochote.
“He he he safi sana kijana! Umediriki kufanya kosa ambalo leo litagharimu maisha
yako!” askari yule aliyekuwa na kipaza sauti alimwambia amata
“Mleteni mbele!” akasogezwa mbele ya lile jukwaa la kunyongea
“Mtoeni kitambaa!” akatolewa kitambaa
“Mfungueni pingu!” akafunguliwa pingu na kubaki huru. Askari yule akasema
“umeonesha ujeuri, umempiga askari wangu, sasa utashughulikiwa ili ujue kuwa hapa ni
mahali pa pekee” alimsogelea Amata na kumwangalia usoni
“kwanza umechoka! Mwili na roho! Nani aliyekuleta huku? Leo utajutia ulichowafanyia
wananchi huko uraiani!” alisema yule askari huku amemkazia macho Amata, Amata
alimwangalia askari huyu mwenye macho mabaya, mekundu na alikuwa kila akiongea
mdomoni mwake kulitoka harufu ya tumbaku na gongo. Askari yule alimzunguka Amata
kama mara tatu hivi.
“Cockroach!” alimtukana Amata kwa lugha ambayo hakuielewa. Amata aliona kuwa sasa
mwisho wake umefika.
“Aje mwanaume amshughulikie huyu!” aliita askari yule. Mara akajitokeza pande la mtu,
lenye mwili mkubwa, kifua kipana, sura yake ilionesha kila dalili ya kutokuwa na
huruma na mtu, lilimsogelea Amata pale alipo, Amata akarudi nyuma kidogo, lile jitu
likamsogelea zaidi, Amata alishikwa na hofu ya kifo alipogeuka nyuma akakuta watu
tayari wamefanya duara kubwa hamna pa kupenya, alihisi pigo moja la mgongo
lililompeleka chini alipojigeuza kuangalia juu aliliona lile jitu likinyanyua mguu
kumkanyaga akajiviringisha upande wa pili na jitu lile likakanyaga chini kwa nguvu
kishindo ambacho kilitimua vumbi, amata kwa kutumia nguvu zote alirusha teke
lililompata nyuma ya magoti jitu lile likajikuta limepiga magoti, Amata alijinyanyua
haraka. Kelele za wafungwa za kumshangilia Amata zilimpa nguvu akiwa bado
anawaangalia wanaomshangilia alipigwa roba maridadi ambayo ilimkosesha pumzi,
Amata alikukuruka aliporusha mguu wake kwa nguvu kwa nyuma alilipiga hilo jitu
kwenye maeneo nyeti, jitu likamuachia Amata na kujishika maeneo,Amata akaanguka
chini akanyayuka haraka na kwa kasi ya ajabu aliruka kitu kama tik tak akalipiga usoni kwa migu miwili, nguvu ile ilimfanya jitu asimame wima bila kujua lakufanya, Amata
kijana aliyejaliwa wepesi na kusaidiwa na michezo ya sarakasi aliyokuwa akicheza
shuleni aliruka hewani na kumpiga mateke ya kifua, jitu lile lilidaka miguu ya Amata
kwa ustadi lakini Amata alijikunja kama samaki na kumpiga kichwa usawa wa pua na
kumvunja mfupa wa pua, Amata alianguka chini baada ya kuachiwa na lile jitu ambalo
wakati huo lilikuwa linavuja damu puani likiwa limeshika pua, Amata alisogea na
kurusha makonde mfululizo yaliyokwenda sawia tumboni ambapo jitu lile liliachia uso
na kujishika tumboni na Amata alibadili mashambulizi kupeleka usoni, alitumia mtindo
huo kama dakika mbili mpaka jitu lile likawa hoi kabisa. Kelele za wafungwa zikazidi
kuufunika uwanja wote askari wakaja kumkamata Amata na kumtoa asije akaleta
madhara zaidi.
Masikini Amata, hakujua kuwa aliyempiga ndiye mbabe wa gereza hilo, hakuna na
haijawahi kutokea mtu akamshinda, wafungwa walimshangilia Amata na tangu hapo
akawa na marafiki wengi na kuogopwa na wafungwa wengine.
[emoji814][emoji814][emoji814]
Maisha yaliendelea gerezani miezi sita ikapita, kazi, mateso, uonevu ndio ilikuwa sera ya
maisha yao na Amata akazoea hali hii, kila kukicha hawaishi kupigana na kuumizana
kunyang’anyana vyakula na kutaka kuwageuza wenzao, japo Amata hakupenda hali hiyo.
Ilikuwa asubuhi tulivu sana jumapili fulani, watu wengi walikuja kuwatembelea ndugu
zao. Amata alikaa kwenye gogo lililopo ndani ya gereza hilo akitafakari hili na lile
akimkumbuka huyu na yule. Mara alihisi gogo lile kutikisika alipogeuka alimuona
mfungwa mwingine amekaa jirani naye, Amata akamtazama jamaa yule kwa makini sura
yake haikuwa ngeni sana lakini hakukumbuka amemuona wapi, alimtazama tena na tena.
“Rafiki!” mfungwa yule alimuita Amata kwa sauti ya chini, Amata akaigeuka tena
kumwangalia vizuri usoni, Amata akaingiwa na hofu kidogo maana mfungwa huyu
hajawahi kukutana naye sura yake ya kawaida tu lakini alipotabasamu aligundua kuwa
hakuwa na meno, Amata alisogea pembeni kidogo akamuuliza
“wewe ni nani, mbona sijawahi kukuona?”
“Umenisahau?! Wewe ni Amata Ga Imba siyo?” Amata alishtuka kuona hata jina lake
analijua.
“Ndiyo! Mimi ni Amata Ga Imba mwana wa Nkhunulaindo! Nikusaidie nini?” Amata
alijibu na kuuliza kishari kwa maana ndiyo hali aliyoizoea sasa.
“Mimi naitwa Golam wa Golam!” alijitambulisha kwa Amata, kisha akatoa lile tabasamu
lake ambalo lilimfurahisha Amata hata alitamani kucheka, kwa sababu kweli alifanana na
Golam ambaye amata aliwahi kumuona katika filam huko kijijini kwao.
“Safari imewadia!” Golam alimnong’oneza Amata
“Safari, safari gani?” Aliuliza kwa mshangao lakini kwa sauti ya chini
“Mimi na wewe tuna safari ya mbali na ngumu sana, safari hii itatugharimu mengi sana
lakini mwisho wake tutaishi kama wafalme he he he! Nilikuwa nakungoja, na sasa
umefika. Wewe ni Mate ya Simba, kila mnyama atakukimbia, mapori yote yatakuinamia
na kukuheshimu, funga mkanda Amata, safari imewadia” Golam aliongea kwa utulivu
mkubwa. Amata hakuelewa anachoambiwa wala anachokisikia, aliduwaa tu akitazama
upande wapili jinsi pilikapilika za wafungwa na askari zilivyoendelea“Unat…” alitaka kumuuliza Golam lakini alipogeuka hakumuona, Golam alishaondoka
pale kitambo na Amata hakuweza kujua ameenda wapi! Amata aliona kama katokewa na
shetani la kiume, ‘safari, safari gani, kwenda wapi? Lini? Mh!’ hakuweza kupata jibu juu
ya maswali hayo, alinyanyuka pale alipoketi na kuvuta hatua chache kuelekea lango kuu
la gereza, alichokiona hakukiamini, ‘Saringo!’ alishaangaa, mara aliitwa kuonana na
mgeni wake, alikataa kwenda akamwambia afande kuwa hana mgeni, afande
akamsisitizia kwa kuwa alishapewa pesa kidogo na Saringo ili afanye makeke, kwa kuwa
wafungwa wa aina ya Amata hawakutakiwa kuonana na ndugu ovyo. Alikwenda lakini
moyoni mwake hakutaka maishani kuonana na kiumbe huyu mwenye uzuri uliofunika
unyama wake.
“Unataka nini tena? Nimeshafungwa! Unataka kuniambia kuwa nitanyongwa, sivyo?”
amata alimwambia Saringo.
“Amata! Nimekuja kukuomba msamaha, maneno yale sikutegemea kama yatakuwa
kweli, wewe hunijui wala mimi sikujui ila nilitumwa kwako na aliyenituma anakuhitaji
sasa!” saringo aliongea kwa uchungu akimwangalia Amata machoni mwake. Kisha
akaingiza mkono kwenye pochi yake akatoa kikaratasi cha rangi ya purple
kimekunjwakunjwa akatazama huku na huku akamkabidhi Amata, Amata akakipokea
akakificha kwenye nguo ya ndani. Saringo akatoa tabasamu la nguvu kwa Amata, kisha
akageuka na kuondoka zake, Amata alibaki anamwangalia akifarijika kuona jinsi mtoto
huyu alivyojaaliwa hata upande wa nyuma ‘mashaallah’ alijisemea moyoni, mara
alijikuta vurugu kubwa inatokea ndani ya suruali yake ya orange akagundua kuwa macho
yamemponza, akarudi ndani.
Jumapili hiyo ilikuwa ni siku ya burudani na michezo huwa mara moja kwa miezi mitatu,
Amata akaketi kwenye nyasi akiangalia wafungwa wenzake wakisakata kabumbu, kila
alipoangalia huku na huku hakumuona Golam, alishindwa kujua kama Golam alikuwa
mzuka au mfungwa mwenzake, mara akaanza kucheka mwenyewe alipokumbuka
tabasamu la Golam. Aliondoka eneo hilo na kusogea pembeni huku akimuangalia kila
anayekutana naye labda atamuona lakini hakufanikiwa, aliendelea kuvuta hatua taratibu
akiwa bado na mawazo lukuki na maswali yasiyo na majibu.
Golam wa Golam, mfungwa asiyependa kuongea sana na anayependa kufanya kazi muda
wote, alikuwa amepangwa kufanya kazi jikoni kama mpishi na kwa miaka miwili sasa.
Golam alifungwa katika gereza la Sogera yapata miaka saba sasa kwa kosa la mauaji,
alikuwa hapo akisubiri hukumu yake ya kunyongwa kwa kosa hilo. Alipokuwa gerezani
humo hakupenda kujichanganya na wafungwa wengine hakuwa na rafiki na daima
alionekana mtu mwenye kupanga kitu fulani, kwa kipindi cha miaka saba hii hata ndugu
zake walishajua kuwa amenyongwa, hawakuja kumtazama wala kumtaka hali. Alipata
kufahamu njia zote za gereza hilo na ratiba zote za askari za ulinzi wa gereza hilo.
Aliwahi kuwa na rafiki mmoja tu ambaye yeye alishanyongwa pale tu alipojaribu
kutoroka kwenye ngome hii isiyopenyeka.
Akiwa bize na kazi ya kuandaa chakula cha jioni cha siku hiyo Golam alionekana
mtulivu sana hata alikuwa anafanya kazi dakika chache na chache anapumzika lakini
akizama katika fikra zingine.
Amata alirudi kwenye kichumba chake na kujilaza kwenye kigodoro chake kidogo, baridi
ilikuwa kali sana siku hiyo, akiwa amejilaza hapo alipitiwa na usingizi
 
Bado asubuhi sana,ngoja pasogee kidogo then nitafumbua macho kutazama yaliyomo.
 
Mzee Kulubule asanteh sana kwa kuinogesha wikend!
 
MSITU WA SOLONDO

Mtunzi: Richard Mwambe

Sehemu 3

Watu warefu walikuja wakamkamata Amata, wakambeba juu juu, watu hao Amata
hakuweza kuwaona miguu yao wala sura zao, walimpitisha kwenye bonde kubwa lenye
manyoka makubwa mengine yana vichwa viwili, manyoka yale yalijaribu kumrukia
lakini kutokana na urefu wa hao viumbe waliombeba hawakuweza kumfikia kabisa. Mara
walifika eneo kubwa la wazi, pale aliona viumbe wenye vichwa vibaya na vipembe
vilivyojinyonga kama vya kondoo, katikati yao kulikuwa na chungu kikubwa kinachotoa
mvuke wa ajabu. Mara wale viumbe waliombeba walianza kuwa wafupi mpaka kufikia
urefu wa wale wengine, walimpomshusha, Amata ndio aligundua kuwa wale viumbe
wana miguu kama ya kuku na mikia pia walikuwa na jicho moja, wakamnyanyua ili
kumtumbukiza ndani ya chungu, kumbe hawa viumbe wanakula watu baada tu ya
kuwachemsha, Amata alipiga kelele za ajabu….’
Mara alikurupuka kutoka usingizini kumbe alipitiwa na ndoto ya ajabu na mbaya. Jasho
lilimvuja kama kamwagikiwa na maji, akitweta kama mtu aliyekimbia mbio fupi za mita
mia moja. Alipotulia na kurudi katika hali ya kawaida huku akijiuliza maana ya ndoto
hiyo aliona kipande cha karatasi chakavu chini ya mlango, alijinyanyua taratibu na
kuokota kikaratasi kile, akakifungua kwa woga, kikaratasi kile kilikuwa kichafu lakini
kwa taabu aliweza ona kilichoandikwa kwa muandiko ambao herufi zake ziko
mbalimbali, alijaribu kuziangalia vizuri lakini ilimuia ngumu kuelewa ni nini
kimeandikwa, alikiweka pembeni, alipoangalia nje kupitia kidirisha kidogo aliona bado
ni usiku kwani ni mbala mwezi na nyota ndizo zilizong’aza nje, na mizunguko ya askari
walio zamu kwa muda huo. Aliketi tena juu ya kigodolo chake akakunjua tena
kijikaratasi kile, alipokigeuza kwa nyuma aliona mchoro wa ajabu, hakuweza kuuelewa
mchoro huo, kitu chenye umbo la mraba, ndani yake kuna duara kubwa ambalo
lililochorwa X, katikati ya x ile pamewekwa namba tano na mshale uliongalia juu, kabla
ya kuishia mshale ule kamstari kengine kalikatisha na kufanya kitu kama mchoro wa dira
katika kamstari kale kuliwekwa herufi A upande wa kulia na kuliandikwa lugha
isiyoeleweka, Amata aliangalia mchoro ule akaona hamna anachokielewa akakunja kile
kikaratasi tena akakiweka chini ya tandiko akajilaza.
Kulipopambazuka siku hiyo Amata aligubikwa na mawazo mengi alikuwa mpole sana
kama mtu anayeumwa, siku hiyo alitakiwa kwenda na wafungwa wenzake kukata miti
kwa ajili ya kuongeza idadi ya kuni kwa matumizi ya gereza. Wakiwa msituni na kazi
imepamba moto, waliendelea na kuimba nyimbo mbalimbali za kuhamasishana huku
wengine wakipakia magogo lorini, askari mmoja bwana mdogo alisogea karibu na Amata
“Mfungwa! Chagua wengine watatu tukashushe mzigo wengine endelea…”alimwambia
Amata. Wafungwa wanne wakapanda pamoja na Amata, akiwa amekaa juu kabisa ya lori
lile pamoja na askari wawili wenye SMG wakiwa makini na kazi yao, lori lile aina ya
Leyland lilikwenda kwa mwendo wa pole likiwa linapanda mlima mkubwa sana.
Lilipofika juu yam lima kabla alijaanza kuteremkia upande wa pili, Amata aligutushwa
na mfungwa mwingine
“Amata! Cheki nyumba yako kule bondeni ilivyo…” alimwambia. Amata akaangalia
kwa makini akaweza kuliona gereza ambalo wenyewe huliita nyumba, akaangalia vizuri,
lilikuwa linaonekana bondeni hivyo aliweza kuliona vizuri sana. Mara akaona kitu cha
ajabu kidogo aliweza kuiona vizuri picha ya gereza lile… aliliona katika mraba na
alipokaza macho aliona kwa ndani kuna kama kitu cha duara kilichozunguka, Amata
alishangaa sana akaingiza mkono kwenye nguo yake ya ndani akatoa kile kikaratasi mara
akakumbuka kuwa alipo hapafai kufanya hivyo Mfungwa! Telemka huko kaa chini na wenzio!” aling’aka kwa hasira akimnyooshea
kiboko chake. Amata alishuka na kujichanganya na wengine.
Safari ilitimu wakashuka na kuanza kutelemsha kuni kupeleka jikoni, alipoingia jikoni
alimuona Golam kwa mbali akiwa ametingwa na kazi. Golam nae akamuona Amata,
akatoa lile tabasamu lake, Amata akamsogelea Golam
“Umeona mzigo wako?” Golan alimuuliza Amata kwa sauti ya chini huku wakipanga
kuni
“Mzigo gani?”Amata akauliza
“Karatasi ndogo” Golam akajibu
“Ndio! Ni nini kile? Sijaelewa” Amata alimuuliza
“Mimi sijui! Nimepewa nikuletee” alijibu Golam
“Oooh nani alikupa?” Akauliza Amata
“Amesema utamkuta, muonane” Golam alimueleza
“Nitamkuta wapi? Nani?” Amata alizidi kuchanganyikiwa kabla hajauliza aliitwa na
askari na wakaondoka.
Mvua kubwa ilinyesha jioni ile radi kali zenye ngurumo za ajabu zilendelea. Amata na
wenzake walikuwa bado wapo kazini, sasa walikuwa wakirekebisha mitaro ya maji
machafu , viatu walivyovaa vilikuwa vimelowa alkadhalika nguo zao zilikuwa
chapachapa huku baridi kali ikiwapiga walifanya kazi chini ya uangalizi mkali tena
wakati kama huu walifungwa minyororo miguuni. Baada ya kazi hiyo ilipigwa filimbi na
wote walitakiwa kusimama katikati ya uwanja ule. Amata akiwa katikati kabisa ambapo
nyuma yao kidogo kulikuwa ni sehemu ya kunyongea, mara akasikia sauti ya kitu kama
jiwe liliodondokea batini upande wa kushoto akageuka upande ule, kulikuwa na kibanda
kidogo kilichotumika kama choo kwa ajili ya askari, akufuatilia sana akageuka kuangalia
mbele lakini kuna kitu kilimrudisha macho upande ule, katika mlango wa choo kile
kulikuwa na mchoro wa pembetatu iliyojazwa rangi na katikati kulikuwa na duara
ambalo halikupakwa rangi, mchoro ule ulimvutia Amata akakumbuka katika kile
kijikaratasi upande wa nyuma kuna ule mchoro hapo akagundua lazima kuna siri ndani
yake kwa nini michoro hii ifanane, hapo akavuta taswira akakumbuka jinsi alivyoona
gereza lile kwa juu wakiwa juu ya mlima akaoanisha hivi vitu vitatu akagundua kuna siri
ndani yake ‘labda Golam anafahamu siri hii’ alifikiria moyoni. Mvua kubwa iliendelea
kunyesha
“Kutokana na hali ilivyo hatuwezi kuendelea na kazi” aliwaambia askari mmoja, kasha
akaendelea
“mtapanga foleni mtachukua chakula na kwenda kupumzika, hatakiwi mtu kuonekana
nje!”
Wakiwa katika foleni ya chakula, Amata alikazia macho sana upande ule, alikuwa bado
anatafiti kichwani mwake ni kwa nini michoro ile ilifanana na ile ya kwenye kijikaratsi
kile kinachoonekana kuchakaa sana pia ni kipande tu je kingine chake kikowapi, alikosa
jibu.
[emoji814][emoji814][emoji814]
Usiku ule tafrija ya maafande iliendelea, pombe za kufa mtu zilikuwa huko, Amata
alikuwa ni mmoja wanaosaidia katika tafrija hiyo, lakini akili yake yote ilikuwa ni kuingia ndani ya choo kile aone tu kuna nini, kwa mbali alimuona Golam nae yuko bize
kuhudumia katika meza ya wakubwa, brassband iliendelea kupiga mziki wa taratibu.
Amata alijaribu kuangalia ulinzi uliopo muda huo aliona hakuna mabadiliko kabisa lakini
alijaribu kutafuta nafasi japo aonane na Golam.
Alipokuwa stoo akipanga vinywaji kwenye chano mara Golam aliingia moja kwa moja
akamfuata Amata
“Tutafute muda tukajisaidie!” alimnong’oneza Amata. Amata akapokea kwa mshangao
kauli hiyo lakini baadae akaona kuwa lazima Golam anafahamu chochote juu ya choo
kile.
“Wakianza kuchangamka tu tuonane ili tujue tunaingiaje pale chooni, maana kwa nyuma
kuna mlinzi na juu kabisa yupo mwingi na taa kubwa inamulika ule mlango” Golam
aliendelea kumdokezea Amata. Akili ya amata ilianza kufanya kazi kwa kasi na shauku
ya kuingia pale ilimjaa, lakini aliwaza ‘vipi wasipokuta chochote mle ndani na
wakasthukiwa na askari, itakuwaje’ alikumbuka yule jamaa jinsi alivyonyongwa
akaingiwa na woga. Lakini alijipa moyo na kuamua kutoa dozi ya pombe ili hawa jamaa
wachangamke mapema.
Punde si punde, sherehe ilichangamka, watu waliimba na kucheza, Golam akazunguka
upande wa Amata akampigia mbinja, Amata alipogeuka akamuona Golam, Golam
akampa ishara ya mkono kuwa azunguke upande wa pili wa jingo hilo, alipofika upande
huo alikuta miili miwili ya askari ikiwa chini, Golam akamwambia Amata avae uniform
ya mmoja wao, akafanya hivyo japo nguo ile haikumkaa sawia lakini alionekana kama
mmoja wa maafande, Golam naye akatwaa za yule mwingine halafu wakawavalisha nguo
zile za ufungwa, amata hakujivunga akabeba SMG na magazine mbili za akiba
akamuoneshea alama ya dole gumba
“Naingia vitani!” Amata alinong’ona kwa Golam. Golam aliondokea upande wa pili na
Amata upande mwingine, kazi ikaanza.
Hadi kufika katika choo kile kutoka walipo akina Amata ni kama mita mia nne hivi na
katikati hapo kuna mataa makubwa yanayoangaza hata akipita panya taa zile
huzungushwa kufuatilia kinapoelekea kitu hiko, jinsi walinzi walivyo makini. Amata
akajiweka tayari na kwa mwendo wa taratibu akiwa amejifunika koti lile la magereza,
alivyojipapasa mfukoni alikuta kuna sigara alipoitoa aligundua kuwa ni msokoto wa
bangi, Amata akatabasamu kwa sababu ana muda mrefu sana bila kupata hiyo kitu.
Aliendelea kupita na kiambaza cha ukuta chini ya vibanda vya walinzi, alipofika upande
ule ambako ndiko choo kile kilipo alitulia kidogo kwenye kona moja kwa kuwa aliona
mtu akija upande ule aliokuwepo. Amata alisimama kikakamavu akiwa kampa mgongo
mara alihisi kashikwa begani alipogeuka taratibu aligundua alimgundua kuwa alikuwa
Golam
“Shhhhhh!!!” Golam alimuashiria Amata kutulia kisha akampita na kumpa ishara ya
kumfuata, Amata alimfuata kwa nyuma wakazunguka nyuma ya jengo ambalo hutumika
kama stoo ya kuni wakalipita na kuendelea mbele kisha Golam akasimama juu ya kitu
kama tank kubwa liliochimbiwa ardhini, akatoa katochi kadogo kama peni ambako
alikakuta ndani yan nguo zile akamulika juu ya mfuniko wa taki lile, kulikuwa na
matenki kama matano. Amata hakuelewa Golam anaangalia nini juu ya matank hayo,
tank la tatu akamwita Amata kasha akampa ishara ya mkono kumuonesha kwamba ‘ni
hapa’, Amata na Golam wakasaidiana kufungua mfuniko hule na walipofanikiwa Golam
aliingia wa kwanza na Amata akafuatia kasha wakafunga mfuniko ule kwa ndani.Ndani ya shimo lile kulikuwa na giza nene sana hata huwezi kuona kitu kilicho mita moja
mbele yako, Amata alijaribu kukanyaga taratibu na Golam akafuatia, Golam akatoa
katochi kake mfukoni na kuangaza kidogo, ni mwanga hafifu sana uliotoka katika tochi
ile haikuweza kuangaza mbali, taratibu Amata alimfuata Golam alikoelekea kwa mwendo
wa kunyata, ukimya uliokuwa ndani ya shimo lile ulitisha, kawa mwendo ule ule
wakiangaziwa na mwanga hafifu, Amata aliogopa sana kutokana na giza lile alitamani
kumwambia kitu Golam lakini alishindwa pia aliona labda akifanya hivyo ataaribu
utaratibu asioujua, mara ghafla wakasikia kelele kama za mbawa za njiwa arukae kabla
Amata hajajiweka tayari Popo mkubwa alipita usoni kwake na mbawa zake zikampiga
usoni, Amata alitoa mguno wa sikitiko lakini hakuthubutu kupiga kelele alivumilia tu,
bado waliendelea kupiga hatua ndogondogo. Baada ya kutembea kwa mwendo huo kama
dakika kumi na tano hivi Golam akasimama ghafla kisha akamzuia Amata kwa mkono
wake walisimama katika ukimya wa hali ya juu kama sekunde hamsini hivi. Amata
alitamani kumuuliza kitu Golam lakini bado alishindwa ila alihisi kitu fulani kumkaba
kooni kutaka kusema lakini aliona sio wakati muafaka japo alipenda kujua hata ni wapi
wanaelekea.Walitembea taratibu mwendo kama wa lisaa limoja, masikio ya Amata
yalikuwa kama yanataka kuziba kwa ukimya ule ambao hajawahi kuuhisi katika maisha
yake, mara akaanza kusikia sauti kama za njiwa dume na jike wakiwa katika harakati za
mapenzi na punde tu zikapotea akaanza kusikia sauti za mbu wengi sana wakitaka
kuingia masikioni lakini alipopunga mkono wake upande wa sikio hakuhisi kugusa
chochote akasikia kama wanamfuata kwa nyuma akageuka hakuona kitu huku akivuta
hatua ndogondogo mara akahisi kugonga kitu alipotazama mbele alijikuta amegonga
ukuta... hakuna njia... Golam haonekani! Matatizo.
Amata alipapasa ukuta ule akona ulikuwa wa mawe makubwa ambayo si ya kujengwa na
binadamu bali ni mwamba mkubwa, mkono wa mtu ukamshika begani Amata akashtuka
na kupiga ukelele wa nguvu alipogeuka alimuona Golam,
“Usipige kelele !!” Golam akamsisitiza Amata
“Utawaamsha mapema!” aliongeza
Amata hakuelewa alichoambiwa na Golam ‘nani wataamka mapema?’ alijiuliza bila jibu
Mbele kidogo walikuta kuna milango milango ipatayo kama nane hivi, Golam
akasimama akatoa kipande cha karatasi kutoka kwenye nguo yake ya ndani akakimulika
kwa mwanga hafifu wa kale katochi ambako tayari betri zake zilishaanza kupoteza
nguvu. Golam akawa kama anahesabu kitu fulani katika ile milango kisha akampa ishara
ya kumfuata Amata akafanya hivyo, walipita kwenye moja ya hiyo milango huko
wakatembea kwa mwendo wa haraka kidogo, Amata aliendelea kusikia sauti za vitu
mbalimbali mara watu wanacheka mara wanalia, kwake ilikuwa ni uoga mtupu. Mbele
kidogo baada ya mwendo wa kama saa moja ingine Amata alianza kusikia kelele za maji
mengi kama mto upitao, akamtazama Golam ambaye alikuwa amesimama kimya kama
gogo, akamsogelea akamuona Golam kafumba macho katulia sana hakumshtua akasubiri
aone nini kinafuata.
“Maji !” Golam alinong’ona na Amata akasikia mnong’ono huo
“Sasa tufanyeje?...”Amata naye alijibu kwa swali kwa kunong’ona
“Lazima tuvuke, tufuate huu mto... mto Solondo” Golam alimjibu Amata
“Mto Solondo!?” Amata alishangaa na kumuuliza GolamNdiyo. Huu ni mto wa Solondo, lazima tuvuke kwa kuogelea kuna watu wanatusubiri
nje, ila tahadhali mto huu una Mamba na maajabu mengi uwe makini, unajua kuogelea?”
Golam akamwambia Amata
“Najua kidogo sijawahi kuogelea kwenye maji mengi kama haya, hakika nitakufa.”
Amata alijibu kwa kuhuzunika
“Acha ujinga Amata! Ukisema utakufa, utakufa kweli” Golam alimwambia Amata kwa
ukali kidogo na kumtupia swali
“haya unajua haya maji yanaelekea upande gani?”
Amata kwa uoga akajibu
“Sijui mbona hata maji yenyewe siyaoni nasikia mvumo tu”
“Ukipiga hatua mbili utatumbukia mtoni. Niambie haya maji yanaelekea upande gani?
Tunatakiwa kuelekea upande yanakotoka siyo yanakokwenda...” Golam aliendelea
kumuambia Amata.
Golam akachuchumaa na Amata akafanya vivyo hivyo,
“Papasa kwa mkono polepole mpaka ufike ukingo wa mto kisha tumbukiza japo kidole
uone maji yanaelekea wapi!” Golam alimwambia Amata. Amata akafany hivyo
akapapasa na mara akahisi kafika mwisho wa kajia kale na kelele za maji ziliongezeka,
akaingiwa na woga mkuu, moyo wake ulikuwa unadunda kwa kasi na kijasho
kumtiririka. Akayagusa yale maji yalikuwa ya moto kama yako jikoni akahisi mkono
wake unavutwa upande wa kulia, akajaribu kuutoa alihisi kama kitu kimemshika mkono
kinamvuta majini, nguvu zikamuishia akapiga kelele
“Golaaaaaaaammmmmmmmm!!!”
Kishindo kikubwa kikasikika cha kitu kutumbukia majini, Golam akapiga hatua mbili
mbele akaita
“Amataaaaaa!!!”
Alipoona kimya akajirusha majini akapiga mbizi maridadi, ndani yamaji yake palikuwa
na mimea iliyotambaa akamuona Amata amenasa kwenye mimea hiyo akaogelea na
kuanza kumsaidia aktoa kisu chake kidogo na kuanza kukata mimea hile, kila alipokata
ilitoa kitu kama damu, alipofanikiwa kumto Amata wakaanza kuogelea kinyume na maji
haikuwa kazi ndogo. Amata hakuwa mzuri kuogelea kama Golam kila mara Golam
alijikuta kamuacha Amata nyuma, Golama akamshika Amata huku upande mmoja
kashika kwenye ncha ya jiwe akamvuta Amata kwa nguvu zote na kumuweka mbele
yake, wakaendelea kuogelea sasa Amata akiwa mbele na Golam nyuma. Amata akiwa
mbele aliendele a kuogelea kwa shida kwa kuwa maji yalikuwa yanasukuma nyuma,
Golam alijitahidi kumlinda Amata asije kubebwa na maji. Baada ya kuogelea kama
masaa mawili hivi Amata alianza kuona maji yale yanang’aa kwa mwanga wa nje,
alikuwa amechoka hata kujisogeza haikuwa rahisi, Golama alimvuta Amata na taratibu
walijikuta wanafika nje ya lile pango kubwa lakini bado kasi ya maji haikuwa ndogo,
Amata akahisi kitu kimemshika mguu akahangaika kujinasua akashindwa, Golam
akajitahidi kumvuta lakini haikuwa rahisi wote walikuwa wamechoka sana, Amata
akaponyoka kutoka katika mikono ya Golam, akahisi kuvutwa tena majini mara hii ni
kwa nguvu zaidi, alihisi kama mikono ya watu imemshika miguu, alikunya maji
akajaribu kujizuia lakini ikashindikana alilegea na kukosa nguvu kabisa. Golam aliibuka
nje ya mto, akarushiwa kamba na kuishika barabara akavutiwa nje
“Amata yuko wapi?” aliulizwa, akajibu kwa ishara tu kuoneshea kuwa yuko ndani ya
maji. Jiwe kubwa lililosukumwa na maji lilimgonga Amata kwenye paji la usoakachanika ngozi ya usoni damu zikaanza kumvuja kwa nguvu, mara akajikuta ameibuka
nje na kunaswa kwenye miti midogo iliyo jirani na hapo, Golam akamuona Amata,
wakafanya juu chini na kumnasua na kumleta nchi kavu. Wakakoka moto mkubwa ili
kuwapa joto Golam na Amata, wakamsaidia Amata kutapika maji yale na kuzuia damu
iliyokuwa inatoka katika jeraha lake. Amata akapoteza faham
 
Ya Solondo yanatisha!

Shukran mkuu Kulubule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom