Tutegemee CHADEMA kuanza kutetea wamachinga?

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,045
2,000
Baada ya jiji kuajiri wanamgambo wa kupiga wamachinga na Mama Ntilie ifikapo tarehe 18/5, angalau jiji la Dar litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.

Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua.

Kumbuka bodaboda, Mama Ntilie, machinga walikataa kushiriki maandamano ya Chadema kwa miaka 5 kwa sababu walikuwa na kazi za kufanya na walilipa kodi kupitia kitambulisho maalum.

Hao wamachinga watakaokuwa wanapigwa barabarani si watakimbilia Chadema? Watapokewa?

Bila shaka sasa baada ya kuanza kuwapiga CCM na maisha bora kwa kila mtanzania vitaimarika sana na huenda uchaguzi mkuu 2025 CCM wakazoa kura 99%
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
41,586
2,000
Yaani nyie ni vichaa sijapata kuona, yaani mnajua tulivyopinga upuuzi wenu wa kuruhusu huu ujinga wa biashara holela mkamsikiliza yule mwendazake.

Leo mnaanza kutusumbua hapa, mnatengeneza tatizo, mnakuja na suluhisho fake then mnashangilia. Mna akili kweli nyie? Naona kama vile mnastahili kwenda mirembe.
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,432
2,000
Bavicha mna roho mbaya sana. Hata wanyonge mnawaonea wivu! Kisa hawakushiriki maandamano yenu na hawakuwapa kura basi wamekua maadui zenu. Mnatete shamba la Mbowe huku mnashabikiwa masikini waharibiwe hata wanachokitegemea pekee.
 
Iboya2021

JF-Expert Member
Dec 1, 2020
465
500
Yaani nyie ni vichaa sijapata kuona, yaani mnajua tulivyopinga upuuzi wenu wa kuruhusu huu ujinga wa biashara holela mkamsikiliza yule mwendazake.

Leo mnaanza kutusumbua hapa, mnatengeneza tatizo, mnakuja na suluhisho fake then mnashangilia. Mna akili kweli nyie? Naona kama vile mnastahili kwenda mirembe
Chadema vichaa tu kama walivyo vichaa wa Milembe
 
Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,045
2,000
Yaani nyie ni vichaa sijapata kuona, yaani mnajua tulivyopinga upuuzi wenu wa kuruhusu huu ujinga wa biashara holela mkamsikiliza yule mwendazake.

Leo mnaanza kutusumbua hapa, mnatengeneza tatizo, mnakuja na suluhisho fake then mnashangilia. Mna akili kweli nyie? Naona kama vile mnastahili kwenda mirembe
Je utawatetea mama ntilie watakavyoanza kupigwa?
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
504
1,000
Wengi wamekaa kimya sio kwamba hizi taarifa hawana lahasha. Ila wanachosubiri ni kusikia Robart Amsterdam na M'beleji (Lisu) wanasema nini kuhusu hii ishu, afu na wao ndo waanze kufuata upepo utaotokea Ulaya.
 
  • Thanks
Reactions: mmh

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
12,149
2,000
Magufuli ndo aliyewaruhusu kufanya kazi..pro-magu kazi kwenu.

Miji na majiji wamegeuka vituko..maturubai kila sehemu.
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
41,586
2,000
Je utawatetea mama ntilie watakavyoanza kupigwa?
Kwahio mmetengeneza Tatizo, na sasa mnataka muwapige, sio? Wakupigwa na kulaaniwa ni Nyie mliowaruhusu wafanye biashara holela eti Rais wa Wanyonge
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
41,586
2,000
WABUNGE WA CCM WANAKIAIBISHA CHAMA.

Na Thadei Ole Mushi.

Jana Waziri mkuu kakosa maswali ya kuulizwa kwenye session yake ya nusu saa alhamisi.

Huu ni umbumbumbu mkubwa kwa wabunge wetu wa CCM. Yaani Waziri mkuu anakosa maswali Bungeni wakati:-

Bei ya Sukari ipo juu.

Bei ya mafuta haishikiki.

Baadhi ya Mitandao haijashusha Bei ya Vifurushi.

Vijana wanapambana kutafuta ajira na hazipo.

Yapo mengi Sana ya kuuliza.

Mtu wa kuyatolea ufafanuzi na mwenye mamlaka yupo lakini hakuna wa kumuuliza.

Bunge la Chama kimoja na Akili za wabunge Nazo zimeungana na kuwa Moja.

Tuna Kazi kubwa Sana 2025 ya ku screen vijana wenye maarifa na weledi wagombee Ubunge. Hawa walio screeniwa na Bashiru na Polepole wanatia aibu.

Shame!!!

Ole Mushi
0712702602
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,321
2,000
CDM wanachosema ni kwamba " Weka misingi mizuri ya mambo haya" - miaka nenda rudi tatizo la wamachinga dar es salaam halijawahi kutatuliwa na kuisha kwa nini? CCM mmeshindwa kutatua tatizo hili badala yake huwa mnaliahirisha then mnaibuka tena kulitatua wakati limeshakuwa si tatizo tena bali ni zigo.

Hawa sasa hao wamachinga waliojazana hapo mitaa ya posta na mwingineko kote kwa maelfu unawapekeka wapi, kwa utaratibu upi?
 
Hao wamachinga aatakuwa wanapigwa barabarani si watakimbilia chadema?
Mtawapokea?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom