Moriss Makoy: Mbabe wa CHADEMA na CCM Arusha

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,749
2,437
Nikiwa kama mwandishi huru na mpenda haki, Leo nimeamua katika makala yangu kuandika kuhusiana na mtu huyu maarufu sana kwa wafanyabiashara haswa wadodogo na wamachinga.

Pia ni maarufu kwa vijana wa kike na wa kiume wa Arusha mjini kwani wakati flani alkua anawaajir katika shughuli zake za ushuru wa parking za magari. Kwa wanaomfahamu na wasiomfahamu, bwana huyu amaaruf kama OSAMA ni mfanyabiashara na mwanasiasa.

Wakati wote yeye ni mtu wa kuona mbalii sana na kupangilia mambo yake ya kibiashara na kisiasa Kwa nguvu kubwa lakini hutumia matisho, rushwa na mbinu chafu.

Yeye ni kinara wa nakata linaloendelea hapo Arusha mjini katika vibanda vya stand ndogo ambapo anamiliki vibanda takribani 45 pamoja na choo cha kulipia. Vibanda vyote hivi amevipata kimaabumashi Kwa kusababisha sakata kama la hivi sasa, ingawa la sasa limeskika sana kutokana na mfumo bora wa serikali ya sasa iliyopo madarakani, ambayo inawafanya watu kuwa wazalendo na wanaojiamini Kwa kua Raisi JPM hapendi ufisadi, rushwa na uonevu.

Mnamo mwaka 2007 Kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu wa halmashauri, walianzisha vuguvugu ambalo lilipelekea watu wote walio wajenzi katika gorofa kubwa lilipo katikati ya standi ndogo kupewa notice ya siku 14.

Hapo sasa Kwa kutumia mwanya Huo, Morris alichangisha fedha kutoka Kwa wajenzi wale Kwa Kile alichodai ni gharama za kwenda mahakaman na wale walioshindwa kutoa fedha hizo aliwanyang'anya vibanda kibabe na wale waliopata hofu kwamba jengo litavunjwa walimuuzia vibanda hivyo Kwa bei rahisi sana.(OSAMA NI MWEREVU SANA).

Hakuishia hapo, katika hali isiyofahamika hadi leo, Morris alipewa uwakala wa kukusanya kodi za pango hapo stand ndogo. Kama kawaida yake, nafasi hii hakuifanyia makosa Bali aliitendea Haki.

Kwanza alihakikisha kodi zinapanda na Kwa taarifa yeye ndo muasisi wa kupanda Kwa kodi na kuwa kubwa sana stand ndogo. Nafasi hii pia aliitumia kuwanyang'anya vibanda wajane na mayatima wote walioshindwa Ama kuchelewesha kulipa kodi.

Alipata vibanda vingi sana katika mpango huu, na aliviuza Kwa bei kati ya sh.m20-m25. Na ndo maana hapo stand ndogo wengi wanaojiita wajenzi ni wanunuzi waliopata vibanda hivyo katika mpango wake huu kabambe. Kikubwa sana na kibaya zaidi baada ya kupewa uwakala huu alkua hawakilishi fedha jiji Kwa wakati.

Baada ya masekeseke Haya, Baraza la madiwani lililopita likiongozwa na CCM , liligundua uozo huu na kuanza kufanya upya tathmin ya Mali za halmashauri. Iliamua kutangaza tenda na taratibu zingine ambazo waliona zinafaa.

Kwasababu bwana huyu alijua anavyofaidi na raslimali hizo alitumia nguvu kubwa sana kufadhili madiwani wa upinzani Kwa mashart kwamba wakifanikiwa kuingia madarakani wahakikishe wanauzima kabisa "moto" ambao ulianzishwa na CCM.

Wakati huohuo, Kwa hofu kuwa CCM ni chama Kilichoshika dola na sio rahisi sana kuking'oa madarakani, bwana huyu aliamua kujitumbukiza katika siasa lakini Kwa ticket ya CCM. Alipambana hadi akapata Nafasi ya kukiwakilisha chama huko katika Kata ya Ukaoni moshi vijijini.

Kibabe wapangaj wake wote wakibosho wa huko ukaoni na wale wakibosho waoga walifanyiwa mpango wa kupata kadi ya CCM wao na familia zao na kusafirishwa kwenda ukaoni Kwa ajili ya uchaguzi. Alifanikiwa kupata udiwani na pia alichaguliwa kua mwenyekiti wa halmashauri moshi vijijini.

Kwa ule ubabe wake na tabia zake za matisho, chuki iliyokithiri na uonevu, alisababisha wananchi kuwa na chuki kubwa dhidi ya CCM hivyo kupelekea chama kuanguka sana uchaguzi uliofata. Yeye alibaki Kwani anafahamu alichokifanya hadi akabaki. Enzi hizi za JPM hatatoboa.

Baada tu ya serkali ya awamu ya 5 kuingia madarakani, viongozi waandamizi wa CCM ambao walifahamu vyema mbinu chafu ya huyu bwana Morris Makoy na ambao walikerwa na Tabia mbaya ya huyu bwana kujidai ana mahaba na CCM, kufadhili upande wa pili kwa sababu tu ya maslahi yake binafsi, waliamua kufufua mchakato wa kufatilia Mali za halmashauri ingawa walkua na diwan mmoja tu ambae ni mheshimiwa TOJO.

Madiwani wote baada ya kulipitia Hili swala waliona ni Sawa kabisa na wakati Huo bwana Morris na jopo lake, walikosa nguvu za hoja, sababu kuu zikiwa ni:Watendaji wa halmashauri pamoja na serikali walkua na hofu kubwa sana kufanya faulu zozote kwani waliogopa kutumbuliwa na JPM.

Wapngaji wafanyao biashara katika maeneo yale pia walikua wamechoka na Kodi kubwa walizokua wanatozwa kwa mwaka 450000-800000 (kwa mwezi.) Na walkua wanalipishwa Kwa mkupuo jambo lililokua linawafanya washindwe kulipa kodi za serkali kwa ufanisi.

Morris na jopo lake waliitisha kikao pale stand ndogo mnamo mwezi march mwaka 2016 na walimwalika diwani wa levolosi ili awatulize wapangaji lkn haikuwezekana.

Haikuwezekana kwakua wapangaji walkua na hari na imani kubwa kwa Raisi wao kwamba hatakubali waendelee kuonewa kwenye mali za serkali, lakini wakiwa na imani lazma serkali itafanya kitu ili nao waweze kutoa kodi za TRA kwa ufanisi mkubwa kumuunga Mh Raisi mkono.

Walipoona msimamo wa wafanyabiashara hata mbele ya diwani Nanyaro ambae wao ndo walimweka pale ili awasidie, ndio pale hadharani wakawa wanamwambia diwani akumbuke fadhila walizomfanyia ikiwa ni pamoja na udhamin wa fedha za kampeni, Inasemekana diwani Nanyaro hakuwahi kutumia hata senti yake moja zaidi ya fedha alikua akipewa na Moris na wenzie.

Walienda Kwa mheshimiwa MrishoGambo ambae Kwa wakati ule alikua DC. Na vile Gambo ni smart, very smart, hakutaka kusikiliza upande mmoja, la hasha, bali aliamua kuunda tume chini ya DAS bwana Daudi Mwakiposa.

Tume ile iliskiliza upande wa wajenzi na wapangaj na hatimae mwishoni Tume ile ilishauri kuwe na tenda. Tena tenda hiyo itangazwe kwa wananchi wote wa jiji la Arusha.

Utaratibu ulifanyika na tenda ilifunguliwa, na Bahati nzuri ilifanyika Kwa maeneo yote ya vibanda vinavyomilikiwa na jiji la Arusha. Kwa upande wa stand ndogo ilifanyika na kufunguliwa ingawa liliwekwa zuio la mahakama la duka moja tu.

Morris Makoy alivyo mwerevu, sasa alirudi na gia ya CCM. Aliratibu michango Kwa jina la CCM. Watu walichangishwa fedha kibabe ili apate fedha za kuendesha mashauri mahakamani na kupambana.

Fedha hizo zilichangishwa wananchi waliambiwa CCM ndo wameagiza. Katibu mwenezi wa CCM wilaya ndugu Gasper Kishumbua alikanusha Hilo vikali. Ndipo sasa Moris aliwakusanya mamluki wote eti wao ni CCM Ama wanarudi CCM kutokea CHADEMA.

Hadi shokia aliekua akimtukana JPM Kwa vipaza sauti pale stand kipindi cha kampeni nae alibebwa ni CCM, Dominick Mollel nae ambae ni CHADEMA damu nae eti aligeuka CCM. Fitna ikaanzishwa eti wao ni CCM wanafukuzwa na CHADEMA kwenye vibanda.

Hawa wote wamekuja CCM Kwa maslahi yao binafsi. Hawakipendi chama kabisa bali wanalinda maslah yao, huku wakikandamiza wachache. Ni fitna kubwa sana ilitengenezwa ili kuwarubuni viongozi.

Baada ya sokomoko lote hilo, Mkurugenzi wa jiji ndugu Athumani Kihamia alihamua kuwakutanisha wapangaj na wajenzi ili kutafuta namna nzuri ya wote wabaki, amani iwepo na mapato yapatkane Kwa aehemu zote tatu.

Yalitengenezwa maridhiano na Mkurugenzi wa jiji ambae kimsingi ni mmiliki wa vibanda vya halmashauri alifanya jambo jema sana. Na kupitia vyombo vya habari alitangaza mgogoro ule umemalizika.

MOU ilitengenezwa na kusainiwa na pande zote tatu na Mkurugenzi wa jiji aliagiza utekelezaji uanze haraka iwezekanavyo. Lakini cha kushangaza Moris Makoy ghafla alianzisha vuguvugu la kuyakataa maridhiano Yale ambayo aliyakubali mwanzo. Aliapa kua atayavunja Kwa gharama yoyote ile.

Hadharani amejinadi wapangaj hawawezi kwenda kulalamika popote pale iwe kwa RC, DC, Waziri mwenye dhamana, Waziri Mkuu na hata Raisi. Ya kwamba yeye ana namna ya kupata taarifa zinazoendelea ndani ya serkali na kwamba hata wakijaribu kwenda atawazuia Kwa namna anazozijua yeye na hawatafanikiwa kuwaona viongozi.

Amewashauri wajenzi wasipokee Kodi yoyote Kwa mpangaji, na maduka yaliyofungwa amekataa isipokelewe Kodi yoyote ili viongozi haswa RC DC na Mkurugenzi wawafukuze wapangaj hao Kwa kisingizio kua ni wakorofi.

Ukweli ni kwamba wapangaj sita tu katika stand yote ndo waliopokelewa Kodi.
Kibaya zaidi alichokifanya, ametoa Mali ya mpangaji wake aitwae Stephen na kuvunja kibanda chako yeye akiwa hayupo na haijulikani alipopeleka Mali hiyo. Hivi sasa Anafanya biashara hapo yeye mwenyewe.

Kutokana na mgogoro huu hivi sasa tayari ameshavuna vibanda zaidi ya 25.Wafanyabiashara wa stand wameshikwa na butwaa, wanashangaa ni wapi anapata kiburi na kufanya hayo anayoyafanya, Kwa nini yeye siku zote yupo juu ya sheria. Ni kwann serkali inamwacha mtu huyu inaendelea kuona watu. Kwa maslahi yake maana sheria zinavunjwa na hafanywi chochote, Kwa nini?

Huko Ukaoni kwenyewe sio kwamba hapingwi, Bali hutumia kanuni zake hizo hizo kutisha wanachama wengine wa CCM. Upinzani na kwenyewe Kwa vile huwafadhili wakati wa chaguzi, basi hujitoa kwenye kinyang'anyiro na kumwacha akijinadi amepita bila kupingwa.

Lengo lake ni awe mbunge kupitia CCM. UHAKIKA NI KWAMBA ENZI HIZI ZA JPM NA POLEPOLE HATATOBOA. 40 ZAKO HAKIKA ZIMEFIKA

HITIMISHO
1.Huyu ndie chanzo kikubwa cha migogoro iliyopo stand ndogo.

2.TAKUKURU hebu fanyeni uchunguzi wa Hili swala.

3.Serkali Kuu pia iingilie kati ifanye uchunguzi wa Hili jambo. Rushwa, ufisad na wizi wa kutupwa vimetamalaki hapo stand ndogo.

4.CCM isikubali jina lake na taswira yake kuharibiwa na kutumika vibaya Kwa ajili ya mtu mmoja tu. Pale stand ndogo kuna shina la wakereketwa linaitwa NAMANGA. Morris Makoy pamoja na Very Manjira walikataa kabisa lisiwe pale Kwa madai kwamba lile ni eneo la gorofa lao. Kama Wana mapenzi ya kweli ya CCM basi shina lile liendelee na bendera ipandishwe pale. Kwanini wanajenga shina jipya?? Yani je ndo utaratibu wanachama wapya wakiingia CCM wanafungua shina lao na kufunga lililokuwepo??? Ifahamu tu wale wafanyabiashara pale ni wingi na wanajengewa taswira kwamba wanaonewa na CCM. @HumphreyPolepole.

5.Sio kweli kwamba wale wapangaj eti ni CHADEMA, Bali ni mpango kabambe uliotengenezwa na jabali Hili Morris Makoy.

6.Mimi kama mwandishi habari niliefatilia sakata Hili toka mwanzo, nimefanya utafiti wa kina wa sakata hili pamoja na utafit mkubwa sana wa bwana huyu. Kitabu chake ni kirefu sana Haya ya Leo ni machache ambayo naamin sasa wasioelewa sakata Hili wataanza kupata mwanga.

Kwa Leo wacha niishie hapa. Naamini Kwa kua wale wafanyabiashara wapangaj washatishiwa na Morris kwamba hawataweza kuingia ofisi zozote za serkali, Kwa makala Haya naamini kuna viongozi watasoma tu na watachukua hatua.

Mheshimiwa Mrisho Gambo, Fabian Daqaro na Athuman Kihamia (GDK) naamin Hili halitawashinda. Umefika wakati muafaka wa kuskiliza pia upande wa wapangaj Kwani nao Wana Haki zao.
 
Kama hamuelewi mrudi shule za kata. Ahsante kwa taarifa mtoa Masada. Hata JPM yupo humu MMU subiri action zake. Mrisho Gambo ndo anashinda humuhumu. Very soon atashughulikia
 
Kama hamuelewi mrudi shule za kata. Ahsante kwa taarifa mtoa Masada. Hata JPM yupo humu MMU subiri action zake. Mrisho Gambo ndo anashinda humuhumu. Very soon atashughulikia
 
Hiyo ndio athari ya mali ya umma kuendeshwa kisiasa, yaani kwa namna uchama ulivyotawala hii crisis mtu anaweza kudhani mali zenye mgogoro ni mali za CCM kumbe ni mali ya umma.

Inasikitisha kuweka siasa kwenye maslahi ya taifa kuna mtu anajitapa kwamba maendeleo hayana chama lakini yeye ndio muasisi mkubwa WA huu ubaguzi kwa misingi ya kichama kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kutokea Tanzania.
 
HUYO Fisadi inabidi apewe money laundering case,,,,au uhujumu uchumi kabisa,,,anamshika sharubu Ngosha
 
Kama hamuelewi mrudi shule za kata. Ahsante kwa taarifa mtoa Masada. Hata JPM yupo humu MMU subiri action zake. Mrisho Gambo ndo anashinda humuhumu. Very soon atashughulikia
Litakua jambo la heri sana. Haiwezekani mtu mmoja na kakikundi cha watu wasiozid 30 wawaonee watu zaidi ya 800. Pale stand kuna maduka 396 Kwa haraka haraka ukijumuisha mfanyakazi mmoja tu Kwa kila duka tayari ni watu 792 wanapategemea pale kupata riziki zao za kila siku. Huo ni wastani wa chini. Kuna maduka, migahawa na saloon yana wafanyakazi zaidi ya mmoja, bado wadada wa vibarazan na wakaka wa kucha. Kifupi watafika hata watu 900. Lengo tu wafkuzwe pale. Ni rai kwamba serkali iwalinde.
 
Maccm as usual,uyo makoyi ni bonge la vampire na watu kama hawa ndo wenye ccm yao,ngoja nitawatumia wasifu wa jirani yangu uyu
Sio CCM ya sasa Mkuu. Huyu 40 zake zinafika soon. CCM ya sasa hatutaki mambo ya konakona.
 
Umewakilisha vema ila ni muhimu kufupisha ili tuweze kusoma yote na kuielewa
Mkuu Kelvin Marcus nakushkuru Kwa ushauri. Yani jinsi huyu bwana alivyo na mambo, hapo nimeyafupisha sana. Sijaweka picha wala video clips akiwa anatisha wananchi. Ila ushauri wako nimeupokea na nitaufanyia kazi katika makala zijazo.
 
Back
Top Bottom