Lema spidi 120

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
SIASA
ico_plus.png

Na Peter Saramba na Musa Juma

Posted Jumapili,Decemba23 2012 saa 8:37 AM

KWA UFUPI

AFUNIKA MOSHI,ARUSHA,BARABARA ZAFUNGWA KWA SAA TANO,SHUGHULI ZASIMAMA,ASEMA AMEREJEA KUTETEA HAKI"LEMA, jembeee, jembe limerudi, wamebana wameachia." Ni baadhi ya maneno yaliyosikika kutoka kwa maelfu ya wafuasi wa Chadema, kumsifia Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, wakati wa mapokezi makubwa ya mbunge huyo mjini Arusha jana.

Aidha, Chadema kimetangaza kuwadai Sh250 milioni, wanachama watatu wa CCM waliomfungulia kesi Lema, ikiwa ni gharama za kesi hiyo.

Mapokezi hayo yalifunika na kusababisha shughuli mbalimbali kusimama kwa takriban saa 5, huku barabara nyingi na mitaa ikifungwa.

Lema alikuwa akirejea Arusha kutoka jijini Dar es Salaam, baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kumrejeshea ubunge wake, aliovuliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Jaji Gabriel Rwakibarila alimvua Lema ubunge, baada ya kuridhika na ushahidi wa wanachama watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo na mashahidi wao kuwa mbunge huyo alitoa kauli za kashfa dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Burian.

Mbali na nyimbo za kumsifu Lema, wafuasi hao wa Chadema walikuwa wakikiponda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Msafara wa mapokezi ya Lema aliyevaa fulana nyeupe iliyokuwa na maandishi kifuani yaliyosomeka; ‘Usiogope, Mungu yupo kazini G. Lema', ulianzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ukiwa na magari na pikipiki zaidi ya 100 za wanachama na wapenzi wa Chadema, waliojitolea kuzijaza mafuta na kupakia abiria bila kulipwa.

Shughuli zote za kijamii, zikiwamo safari za magari na biashara katika barabara zote ulipopitia msafara wa Lema, zilisimama kwa muda kupisha msururu huo wa magari na watu kupita, huku waliolazimika kuegesha magari yao pembeni kupisha msafara wakionyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema.

Msafara kuelekea KIA ulianzia eneo la Phillips jijini Arusha, ukiongozwa na viongozi wa Chadema wilaya na mkoa wa Arusha.

Waliokosa nafasi katika magari ya wanachama na wafuasi wa chama hicho waliamua kusimamisha magari aina ya Coaster, yanayofanya safari kati ya Arusha-Moshi na kuyakodi kwa kujilipia Sh5,000 kama nauli ya kwenda na kurudi KIA.

Baada ya kufika KIA, msafara kutoka Arusha uliungana na uliotoka mkoani Kilimanjaro na kuanza safari ya kurejea Arusha Saa 4:00 asubuhi, safari iliyochukua zaidi saa tano, ambao uliwasili Uwanja wa Soko la Kilombero jijini Arusha saa 9:30 alasiri.

Kwa kawaida, safari kutoka KIA hadi Arusha mjini huchukua dakika 40 hadi 45, lakini jana, safari hiyo ilichukua muda mrefu kutokana na msururu mrefu wa magari, pikipiki na watu waliokuwa wakijitokeza njiani kuusimamisha wakishinikiza kusalimiana na Lema.

Kutokana na hali hiyo, Lema, alilazimika kusimama katika vituo zaidi ya 20 ili kusalimiana na wananchi, ambao wengi wao walishika matawi ya miti mikononi kuashiria amani.

Vituo ambavyo Lema alilazimika kusimama baada ya wananchi kufunga barabara ni pamoja na Njia Panda ya KIA, King'ori, Kikatiti, Maji ya Chai, USA-River, Tengeru, Chama, Kwa Pole, Shangarai, Kambi ya Chokaa, Kwa Mrefu, Ngulelo, Kimandolu, Phillips, Mount Meru Hotel na Sanawari.

Mbunge huyo aliyepanda gari la wazi ili kukata kiu ya wananchi waliokuwa na hamu ya kumwona tangu KIA hadi Arusha mjini pia alisimama katika maeneo ya Clock Tower, Metro Pole, Friends Conner, Kilombero Sokoni kabla ya kuingia kwenye uwanja wa Kilombero National Housing, alikohutubia mkutano mkubwa wa hadhara.

Mapokezi hayo yalihudhuriwa na viongozi kadhaa wa kitaifa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Heche na wabunge Israel Natse wa Karatu, Joshua Nassari wa Arumeru Mashariki, Cecilia Paresso na Grace Kiwelu wa Viti Maalumu.

Katika hatua nyingine, Chadema, kimetangaza kudai fidia ya zaidi ya Sh250 milioni kwa wanachama watatu wa CCM, waliofungua kesi dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Akihutubia mkutano wa hadhara baada ya mapokezi ya Lema jana, Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alisema kuwa Chadema kimewasamehe wote waliohusika kutunga na kufungua kesi hiyo, lakini, hakitawasamehe kulipa gharama za shauri hilo kuanzia Mahakama Kuu hadi Mahakama ya Rufani.

"Chadema tumewasamehe bure, wote waliomhangaisha mbunge wetu kwa kipindi chote cha miaka mitatu, tangu uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu tunajua walitumika kwa tamaa na ushawishi wa fedha. Lakini, gharama zetu lazima walipe," alisema Golugwa.

Akizungumza jana, Lema alisema kuwa kiasi cha Sh250 milioni kilichotajwa na Golugwa ni hesabu za haraka haraka na kwamba kiasi hicho kinaweza kuongezeka, baada ya mawakili wake na wataalamu wa hesabu kukokotoa hesabu.

Lema aliuchekesha umati uliohudhuria mkutano huo aliposema kuwa mnunuzi wa nyumba za mmoja wa waliomfungulia kesi, aliyemtaja kwa jina la Mussa Mkanga tayari amepatikana na yuko tayari kutoa malipo ya awali.

Mkanga ni mdai namba moja katika shauri la kupinga ushindi wa Lema lililokubaliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kabla ya kubatilishwa na Mahakama ya Rufani iliyomrejeshea Lema ubunge wake.

Pamoja na Mkanga, wadai wengine katika shauri hilo walikuwa ni Agnes Mollel na Happy Kivuyo ambao Mahakama ya Rufani imewaamuru kulipa gharama za shauri hilo tangu hatua za awali.

Lema aliyekuwa amesindikizwa pia na baba yake mzazi alisema kuwa amerudi kuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha, kutetea watu wake na siyo masilahi yake, wala ya familia yake kwani kurejea kwake kumetokana na mshikamano wa wananchi.

"Kuna watu waliwahi kumfuata baba yangu na kumshauri eti aniambie, mimi sasa nimechaguliwa kuwa mbunge, nikae na kujenga familia yangu, lakini nilimwambia hapana, mimi sikuchaguliwa kwa manufaa ya familia,"alisema Lema.

Lema aliwataka wakazi wa Arusha, kuwa na mshikamano na kupinga unyanyasaji wa aina yoyote, kwa kuwa chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa hukumu ni mahakama.

"Kuanzia sasa nimerudi, ni marufuku mgambo kuwakamata ovyo na kuwapiga vijana mitaani, maarufu wamachinga na akina mama ntilie kupigwa kama ambavyo imekuwa ikitokea, cha msingi muwe kitu kimoja, mjikinge na wasaliti kutetea haki zenu,"alisema Lema.

Lema alisema anarudi bungeni ambapo atahakikisha anashirikiana na wabunge na viongozi wengine wa chama hicho kufa na kupona katika kuwatetea Watanzania ili kunufaika na rasilimali zao.

Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche, alitangaza kuwa Chadema kimejipanga kumpeleka Ikulu Katibu wake Mkuu, Dk Willbrod Slaa katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015, kutokana na wananchi kuchoshwa na uongozi wa CCM.

"Dk Slaa amewashinda CCM katika kiti cha ubunge Jimbo la Karatu kwa miaka 15 na alipojitokeza kuwania urais uchaguzi wa 2010 alitoa ushindani mkubwa, ambao bado unawatia hofu CCM uchaguzi ujao wa 2015. Ndiyo maana wanawatumia wasaliti wachache kujaribu kumdhoofisha," alisema Heche.

Mwenyekiti huyo aliikumbusha CCM kuwa Dk Slaa wala Chadema siyo adui yao wala siyo sababu ya chama hicho kukosa haiba machoni pa umma, bali adui wa CCM ni CCM yenyewe iliyoshindwa kutimiza mahitaji ya umma.

Heche aliwataka Watanzania kupuuza kampeni za kumchafua Dk Slaa alizosema zimeanzishwa na kuratibiwa kwa mamilioni ya fedha na watu kutoka ndani ya CCM wanaowatumia baadhi ya vijana wasaliti ndani ya Chadema.

Hata hivyo, Chadema hakijatangaza rasmi iwapo Dk Slaa ndiye atakuwa mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015.

ANGALIA HUO UMATI; SIO MIKUTANO ya NDANI kama ya MCHEMBA... Hauoni Wananchi Wanaosikiliza...

lema.jpg

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Imetulia.

CHADEMA mwendo mdundo tu. Hawa wasaliti tumeshawajua na watashughulikiwa hivyo hatuna muda wa kupoteza na wachumia tumbo wachache.

Naomba Lema aunganishe madiwani na viongozi wa CHADEMA mkoani hapo ili kupambana na CCM. Nimekuwa Arusha kwa wiki moja hivi, lakini malalamiko ya wananchi kuhusu Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi na Meya ni mengi. Kuna namna serikali inawakomoa watu wa Arusha (a sort of collective punishment) na ni ukandamizaji unaostahili kupingwa na kushindwa kwa nguvu zote.
 
VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,094
2,000
Pamoja Kamanda Lema. 2015 uje Kibaha Mjini kunisupport. Habibu Mchange tumeshamshtukia ni muongo,kilaza na msaliti
 
Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Initially Lema was not my bread and butter. But he has earned and now he's won my admiration.

What stands out most is his attitude. Lema is very daring, he's also aggressive (which suits the current war) and of coz he loves his voters. It seems there's a bond with his people which defies the political norms.

CCM wana kila sababu ya kumwogopa Lema, maana hakuna jambo baya ambalo hawajajaribu kumtendea:-

1) Walijaribu kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa ubunge 2010 (hali iliyopelekea kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na kusababisha taharuki ambayo kama RPC Basilio Matei hakuingilia huenda maafa makubwa yangetokea)
2) Mchakato mzima wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na mauaji yaliyofutia
3) Vurugu, dhuluma na hujuma ili kumsababisha asitekeleze majukumu yake ya kibunge jimboni kwake
4) Katika kupinga dhuluma na uonevu dhidi yake na hasa kwa wapiga kura wake Lema "alijotlea" kukaa magereza kwa siku 14. Juhudi za kumsihi atoke gerezani zilfanikiwa kabla ya kipindi hicho kutimia.
5) Lema alibaini na kusimama kidete kupinga hila na njama za madiwani watano walioisaliti CHADEMA na wananchi wao.
6) CCM kupitia Jaji mchumia tumbo wakamvua ubunge ktk mazingira tata na ya aibu
7) Alitumia muda na fursa hiyo kukitumikia chama na hasa vuguvugu la M4C. Kila alikokwenda ameisambratisha CCM na hivyo kumwongezea kujiamini na mbinu zaidi za kisiasa na kiutendaji.
8) Ingawa Lema hakutaka kukata rufaa, alishauriwa na kukubali ushauri wa kukata rufaa na hatimaye tarehe 21 Disemba 2012 alitangazwa kuwa Mbunge halali wa Arusha na Mahakama ya Rufaa.

Hivyo kwa hayo machache Lema haihofii wala kutishwa na CCM kwa lolote, ila kinyume chake ni CCM wanaomhofia Lema. Afanye kazi kwa kipindi kilichobaki maana mchango na uongozi wake unahitajika sana jimboni kwake kwa sasa.

May G-D bless Godbless J. Lema
 
Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Ritz yupo wapi na staili yake ya kuzima ubongo na kuchangia JF?Aje atueleze kama watu wanaojaza magari na pikipiki zao mafuta kwa hela yao na kupiga kilometer kadhaa na kurudi wanaweza kuwa wapiga viroba ya bure.
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,231
2,000
Pamoja Kamanda Lema. 2015 uje Kibaha Mjini kunisupport. Habibu Mchange tumeshamshtukia ni muongo,kilaza na msaliti
usisubiri mwaka 2015 kama unania anza kujenga chama na kujijenga sasa na kama unataka sapoti yake ni sasa ili mwaka 2015 kazi iwe rahisi....
 
ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,211
0
Kiukweli Lema ametuonyesha vijana wengi namna ya kuwa majasiri na kutumikia chama na umma kwa unyenyekevu mkubwa. Lema muda wote amekuwa mtumishi mbele ya chama chake kwa operation mbalimbali kama m4c.
 
notradamme

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,009
1,195
Initially Lema was not my bread and butter. But he has earned and now he's won my admiration.

What stands out most is his attitude. Lema is very daring, he's also aggressive (which suits the current war) and of coz he loves his voters. It seems there's a bond with his people which defies the political norms.

CCM wana kila sababu ya kumwogopa Lema, maana hakuna jambo baya ambalo hawajajaribu kumtendea:-

1) Walijaribu kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa ubunge 2010 (hali iliyopelekea kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo na kusababisha taharuki ambayo kama RPC Basilio Matei hakuingilia huenda maafa makubwa yangetokea)
2) Mchakato mzima wa uchaguzi wa Meya wa Arusha na mauaji yaliyofutia
3) Vurugu, dhuluma na hujuma ili kumsababisha asitekeleze majukumu yake ya kibunge jimboni kwake
4) Katika kupinga dhuluma na uonevu dhidi yake na hasa kwa wapiga kura wake Lema "alijotlea" kukaa magereza kwa siku 14. Juhudi za kumsihi atoke gerezani zilfanikiwa kabla ya kipindi hicho kutimia.
5) Lema alibaini na kusimama kidete kupinga hila na njama za madiwani watano walioisaliti CHADEMA na wananchi wao.
6) CCM kupitia Jaji mchumia tumbo wakamvua ubunge ktk mazingira tata na ya aibu
7) Alitumia muda na fursa hiyo kukitumikia chama na hasa vuguvugu la M4C. Kila alikokwenda ameisambratisha CCM na hivyo kumwongezea kujiamini na mbinu zaidi za kisiasa na kiutendaji.
8) Ingawa Lema hakutaka kukata rufaa, alishauriwa na kukubali ushauri wa kukata rufaa na hatimaye tarehe 21 Disemba 2012 alitangazwa kuwa Mbunge halali wa Arusha na Mahakama ya Rufaa.

Hivyo kwa hayo machache Lema haihofii wala kutishwa na CCM kwa lolote, ila kinyume chake ni CCM wanaomhofia Lema. Afanye kazi kwa kipindi kilichobaki maana mchango na uongozi wake unahitajika sana jimboni kwake kwa sasa.

May G-D bless Godbless J. Lema
...

anastahili hongera......
na asiyetaka kumpongeza LEMA ana lake jambo!!!!!!! ni adui wa democrasia
CCM wanajua toka zamani kuwa jimbo la ARUSHA wameshalipoteza milele na ushindi wa mahakamani wala usigewasaidi

ila kuna machache tunatakiwa tujiulize!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
1.Lema alisema mwenendo wa kesi yake na hukumu ya kwanza iliingiliwa na IKULU(RAISI)
2. Je na hii hukumu ya pili hakuna mkono wa raisi???????
3. mahakama ya rufaa ina ukubwa gani kimamlaka mpaka ipuuze amri ya ikulu(raisi)??????????????
4. kama hukumu hii ya sasa ni ya haki(kwa mujibu wa sheria) kwa nini hukumu ya mwanzo isiwe ya haki(kwa mujibu wa sheria)?????????
5. au haki inamaanisha ni ushindi kwa Lema tu na anaposhindwa basi ni nguvu za dola (ikulu) zimetumika??????

kwa ujumla kuna mambo mengi yanayotosha kabisa kuandika kitabu kuhusu mwisho wa kesi hii na hapo ndipo panapotudhihirishia kuwa huenda tukawa tunashabikia watu tusiowajua vizuri. LEMA kipenzi cha watu hususan wana wa ARUSHA lakini hana busara ya kiuongozi hata kidogo.. sijui atauficha wapi uso wake pale atakapokumbushwa kauli yake kua eti IKULU ILMEINGILIA MWENENDO NA HUKUMU YA KESI YANGU..
Mi naona vichekesho tuuuuuuu.
HALAFU KWA MACHO YANGU NIMEMUONA freeman mbowe kwenye mkutano waRAILA ODINGA.. najua ni haki yake kama kiongozi wa kisiasa... Mnasemaje wadau maana mlishamuandama sana MAGUFULI
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
7,003
2,000
Ritz yupo wapi na staili yake ya kuzima ubongo na kuchangia JF?Aje atueleze kama watu wanaojaza magari na pikipiki zao mafuta kwa hela yao na kupiga kilometer kadhaa na kurudi wanaweza kuwa wapiga viroba ya bure.

Nakubaliana na wewe mkuu, naomba niende mbali zaidi, Mchungaji Msigwa aliwahi kusema, tusiruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa, hivi kama CDM wanauwezi wa kuwanywesha viloba watu wote hawa basi CDM wana hela nyingi sana, tena sana, hiyo moja lakini kitu cha pili, kama wote hao wamenunuliwa pombe (bila kujali ni viroba au Bia) mbona hiyo ineeonekana tu impact yake kwenye mapato ya serikali, serikali huchukua pesa kwenye kila kinywaji kinachonunuliwa, sasa umati huu ungekua umetengeneza pesa ya kutosha sana, issue ya tatu, wamiliki wa Bar wangekua matajiri sana kila CDM inapokua na harakati eneo husika, hivyo ni baadi tu ya viashiria ambavyo vyaweza onekena kama kweli CDM huwanunulia watu viroba! Kwa vile akili zao fupi ndo maana wanaweza kudanganya tena uongo wa kitoto kabisa, kama wa mtoto wa shule.
 
Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
7,003
2,000
...

anastahili hongera......
na asiyetaka kumpongeza LEMA ana lake jambo!!!!!!! ni adui wa democrasia
CCM wanajua toka zamani kuwa jimbo la ARUSHA wameshalipoteza milele na ushindi wa mahakamani wala usigewasaidi

ila kuna machache tunatakiwa tujiulize!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
1.Lema alisema mwenendo wa kesi yake na hukumu ya kwanza iliingiliwa na IKULU(RAISI)
2. Je na hii hukumu ya pili hakuna mkono wa raisi???????
3. mahakama ya rufaa ina ukubwa gani kimamlaka mpaka ipuuze amri ya ikulu(raisi)??????????????
4. kama hukumu hii ya sasa ni ya haki(kwa mujibu wa sheria) kwa nini hukumu ya mwanzo isiwe ya haki(kwa mujibu wa sheria)?????????
5. au haki inamaanisha ni ushindi kwa Lema tu na anaposhindwa basi ni nguvu za dola (ikulu) zimetumika??????

kwa ujumla kuna mambo mengi yanayotosha kabisa kuandika kitabu kuhusu mwisho wa kesi hii na hapo ndipo panapotudhihirishia kuwa huenda tukawa tunashabikia watu tusiowajua vizuri. LEMA kipenzi cha watu hususan wana wa ARUSHA lakini hana busara ya kiuongozi hata kidogo.. sijui atauficha wapi uso wake pale atakapokumbushwa kauli yake kua eti IKULU ILMEINGILIA MWENENDO NA HUKUMU YA KESI YANGU..
Mi naona vichekesho tuuuuuuu.
HALAFU KWA MACHO YANGU NIMEMUONA freeman mbowe kwenye mkutano waRAILA ODINGA.. najua ni haki yake kama kiongozi wa kisiasa... Mnasemaje wadau maana mlishamuandama sana MAGUFULI

Nimependa tu namna yako mpya ya kufikiri basi, hilo tu, ungeruhusu kichwa kifanye kazi yake walau kwa dakika 5 tu kwenye hili wala usingeuliza maswali ya kitoto kama haya, ushauri wangu, fanya hivi, "Ruhusu kila kiuongo kifanye kazi kilichowekewa, tumbo liwe tu container la chakula na sio sehemu ya Ubongo"
 
EL MAGNIFICAL

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
938
195
Habarini wana jf !
Kwanza nianze kwa kusema kuleta mada hii haimaanishi nina chuki binafsi na mhusika tajwa hapo juu, Ukihisi nimekosea jua sijui ila nahitaji kueleweshwa zaidi.
Mh. Lema ni mwana siasa machachari sana hapa Tz lakini umaarufu wake mpaka sasa binafsi sijaelewa unatokana na nini !
Mwenye majibu anaweza kunisaidia na nitamshukulu inapobidi !
Je ni mchango gani mkubwa aliowahi kuutoa ktk Taifa hili ?
Je ni uwezo mzuri alionao ktk ujenzi wa hoja kama walivyo wenzie mfano Tundu lissu, Zzk nk. ?
Je ni mwenendo wa siasa anazokwenda nazo ndio zinampa umaarufu ?
Je kuna ukweli kuwa anafuata nyayo za Nelson Mandela ?
Je siasa anazozifanya ni siasa za kuigwa na vizazi vijavyo ?
Je anafaa kukabidhiwa madaraka makubwa zaidi ya ubunge ktk nchi ?
Naomba kuwasilisha...!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom