Tutawapata akina Musa au akina Joshua kwenye Uchaguzi Mkuu 2020; Rais sina shaka ila kwa Wabunge

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Tumebakiza muda mfupi sana bunge kuvunjwa na kwenda kwenye ungwe nyingine ya hiena hiena.

Wengi tunajua Musa aliwavuja Israel bahari ya Shamu, na baadae Joshua akawavusha mto Jordan ili kuingia nchi ya ahadi. Sina shaka na ushindi wa Rais; ila kwa wabunge ambao baadhi yao ndiyo wanakuja kuwa mabosi wa wizara.

Safari hii sina hoja zenye maneno mengi sana, bado natafakari mambo kadhaa na kuna siku ntaandika na kuweka rejea kadhaa ili tunapochangua, tuwe na aina ya viongozi wenye vision na mission za kutufanya ku-enjoy kuwa nchi ya ahadi kwa kudhibiti rasimali kwa kuzigeuza kuwa fedha za kumudu mahitaji ya bidhaa na huduma na huku Kaisari akichukua kodi yake.

Ila natoa angalizo kwa viongozi wa dini zote kubwa hapa nchini. Pamoja na mahudiri ya habari njema ya kwenda mbinguni; na pamoja na juhudi njema za kutanguluza sala na maombi kwa watawala ili tuwe na amani katika nchi yetu ya Tanzania.

Ifike wakati pia tutafakari kwa kina na kuchukua maamuzi ya kina namna gani ya kudhibiti mazingira ya "nchi hii ya asali na maziwa" ili tunapoidhibiti kwa kutumia rasimali zilizopo; tuone mrejesho wa manufaa ya kuwa na uchumi jumuishi.

Tujifunze kule dini ilikotokea kwa maelezo hapa chini...



Either, wanasiasa. Tunawashukuru kwa jihudi kubwa sana mnazofanya chini ya Mkulu na walau tumeona mengi yakifanyika kujenga uchumi mkubwa (Macro Economics).

Ila uchumi mzuri pia lazima uchumi mdogo (micro-econimics) iwe jumuishi kwenye utekelezaji wake. Kuna model ya micro-economics iko hapa chini, tunaweza kupitia hapa chini.

Rais atavunja Bunge la JMT mwezi Juni. Tuko wapi na tunafika lini nchi ya asali na maziwa?

Kwenye muktadha wa leo, naomba pia tu-extract madini toka kwenye falsafa ya mzungumzaji hapa chini.
Nanachopenda miners huwa wanachimbua kupata madini katikati ya matope na vumbi. Tuna la kujifunza kwa huyu mzungumzaji na kila la kheri wale ambao mtapata nafasi ya kutuongoza; natamani tuige model ya mzungumzaji sio kwa ku-copy na ku-paste; sio vibaya, ku-copy, ku-paste the tuka-customize kwa manufaa mapana ya Watazania wengi kuwa kwenye mnyororo wa thamani ya uzalishaji.

Kuna siku ntakuja na nini mimi nimeona.

Wasalaam

Happy Friday kuelekea June juma lijalo
 

Attachments

  • Wealth of Africa Vs Investment.mp4
    3.9 MB
Magufuli apashwi kuendelea kuwa Rais JMT lazima akae pembeni apishe watu wasomi na wenye nia njema na Taifa hili..
 
Back
Top Bottom