Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 12,417
- 30,927
Kwakweli katika mambo ambayo naona ni doa kubwa katika Nchi yetu kwa mwaka huu wa 2020 na pengine miaka hii mitano yote ya utawala wa Rais Magufuli ni namna viongozi wa dini walivyoufyata mkia mbele ya dola kandamizi. Ukiwatoa viongozi wachache Kama MWAMAKULA na BAGONZA pengine na wachache wengine ambao labda sijawasikia waliobaki wootee ni machukizo mbele ya altare ya bwana.
Tumeshuhudia kwa uwazi kabisa jinsi serikali ya CCM ilivyowaonea wapinzani kana kwamba wao sio watanzania wa nchi hii. Pamoja na yote mabaya yaliyotendwa na serikali ya CCM ikiwemo mambo ya sintofahamu za kina Lissu, kushambuliwa na Ben kupotezwa viongozi wa dini wamebaki wakiisifu serikali hiyo bila aibu na kuikaribisha kwenye madhabahu za bwana. Haya mambo yamewapotezea heshima kubwa watu wa dini na kufanya waonekane wako kimaslahi zaidi na kwamba dini ni sehemu ya kujifichia ila ni wapigaji tu kama wapigaji wengine.
Waandishi wa Habari
Hawa wao ni woga na hofu yaani Mambo ya Lissu hayatangazwi utadhani Lissu ni muasi wa M23 lakini Mungu alivyo wa ajabu pamoja na kumzima Lissu bado amesikika sawia kwa viwango vilevile vya mgombea wa CCM. Hebu jiulize Lissu angepewa coverage sawa na mgombea wa CCM kwa 50:50 ingekuwaje?
Ukuu wa Mungu haufananishwi na kitu kingine.