Tutalalamika mpaka lini?

Tutalalamika mpaka lini?

Hii cant be applied in our Tanzanian setting

Mkuu hakuna linaloshindikana duniani, I can tell you this thing can happen anytime and anywhere.

Zingatia chuki iliyopo Sasa kati ya

Wananchi dhidi ya watawala.

Wananchi dhidi ya vyombo vya ulinzi.

Utanganyika dhidi ya Uzanzibar

Ikitokea access ya silaha tuu, utaona badamu batakavyomwagika.

Binafsi sipendi na wala siombei tufike huko na ndio maana Bado Imani yangu nimewapa TEETH kwamba kuna jambo wanaweza kulifanya na nchi ikatulia.
 
Ni kweli si rahisi kutekeleza, inahitaji miaka ya miaka kadhaa huku ukiinject pesa na kumonitor watu ulio wapenyeza.
Ikifanikiwa inayo matokeo ya uhakika sana.
Sawa mkuu
Asante kwa maoni
Karibu tena kwenye mijadala mingine
 
Hapa ndipo palipo na mkwamo, na wenye madaraka hawawezi kuwa wajinga kiasi cha kuwaacha raia wajipatie silaha kirahisi rahisi
Mkuu tuishie hapa ila Congo, Burundi na Rwanda ni majirani zetu na hivyo vitu wanavyo vya kutosha tuu.

Mimi natamani CHADEMA waendelee kuwafungua watu akili, sitamani kabisa njia hii ya kumwaga damu.
 
Zamani Mungu alitujibu kwa wakati sisi kama Tanzania...ila kwa sasa dhambi zimezidi....ushoga unaachwa wazi na chukizo kubwa kwenye Taifa...nani atasema na sisi?? Viongozi wa dini wakiongea hawasikilizwi..
Suluhisho ni kuomba sana Mungu atende miujiza...
 
Morning wana JF

Watanzania tumekuwa tukilalamika kila siku kuhusu uongozi na mambo mbalimbali ambayo hatupendezwi nayo

1. Tumeongea sana tukiomba maboresho ya Katiba

2. Tumezungumza sana kuhusu kupitiwa upya kwa suala la Muungano

3. Tumezungumza kuhusu Mahakama na utendaji kazi wake

(Mpaka sasa tunaona mwenendo wa kesi ya mwenyekiti wa chadema TL inavyoenda huku watu wakiwa na mashaka makubwa )

Na mengine mengi sana

Lakini mpaka sasa hakuna matokeo chanya ya kutosha, licha ya kwamba tulipo leo sio tulipokuwa jana
Kuna mambo yamebadilika, lakini bado kuna mengi ambayo tumekuwa tukiyazungumza kwa miaka mingi bila kuona mabadiliko tunayoyatarajia

Tumeona nchi kadhaa zikifanya jitihada za pamoja
Wananchi wameungana, wameandamana na kudai mabadiliko na katika baadhi ya nchi hata jeshi liliishia kuingilia kati baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi

Hii mifano nimeweka hapa nimesoma huko mitandanoni
👇
Mfano, Philippines mwaka 1986, wananchi waliungana katika maandamano makubwa ya amani yaliyokuja kujulikana kama People Power Revolution, na hatimaye utawala wa Ferdinand Marcos ukaondoka

Tunisia mwaka 2011, wananchi waliingia barabarani kudai mabadiliko na maandamano yakawa makubwa kiasi cha kumfanya Rais Zine El Abidine Ben Ali kuondoka madarakani

Sudan mwaka 2019, wananchi waliandamana kwa miezi kadhaa wakidai mabadiliko, mpaka hatimaye Omar al-Bashir akaondolewa madarakani baada ya miaka takribani 30 ya utawala

Hapa kwetu tulijaribu pia
Kupaza sauti zetu tukiwa na madai mbali mbali

Lakini wote tunajua nini kilitokea October 29 💔

Na wote tunajua mtu anayekwenda kinyume na watawala au anayesema mambo fulani hadharani, mara nyingi kinachoweza kumpata

Ukiongea hadharani unatulizwa

Sasa tutaongea chumbani?

Kama hatuwezi kuongea hadharani, kama hatuwezi kuuliza maswali, kama hatuwezi kukosoa na kudai mabadiliko bila kuogopa, basi tutaikomboaje hii nchi?

Na ninaposema kuikomboa, simaanishi kwamba twende kwenye vurugu au kumwaga damu (nisinukuliwe vibaya)

Ninamaanisha taifa ambalo wananchi wawe waamuzi wa mwisho
Taifa ambalo mwananchi awe na uhuru wa kuzungumza, kuuliza, kukosoa, kuchagua na kushiriki katika kuamua mustakabali wa nchi yake

Kwa sababu sasa tumeongea sana

Tumeandika sana

Tumeomba sana

Tumeilalamikia serikali kwa mambo mengi sana

Lakini swali linabaki pale pale

Nini kifanyike ili tutoke kwenye kulalamika?

Kwa sababu sasa tutalalamika mpaka lini?

Je, tunahitaji nini kama wananchi ili sauti yetu iwe na nguvu na iweze kuleta matokeo?

Na kama nchi nyingine zimewahi kufikia hatua wananchi wakaungana na kudai mabadiliko mpaka yakatokea, sisi tatizo letu ni nini?

Tunashindwa kuungana?

Tunaogopa?

Hatuna imani kwamba tunaweza kubadilisha mambo?

Au bado tunasubiri mtu mwingine aje atufanyie?

ShesRise_1 ✋️
Hii nchi ukiongea utapotezwa au kuuwawa.
Ukijidai muongeaji sana unapewa kesi isiyo na dhamana ili unyamaze
Ukikosoa watawala wanaweza kutoa maamuzi juu yako bila kujali sheria

kilichobaki ni wananchi kutumia haki yao kuandamana kwa nguvu maana kuvumilia huku kukifika mwisho ndio mwanzo wa kuzaliwa vikundi vya magaidi kwenye nchi.
 
Zamani Mungu alitujibu kwa wakati sisi kama Tanzania...ila kwa sasa dhambi zimezidi....ushoga unaachwa wazi na chukizo kubwa kwenye Taifa...nani atasema na sisi?? Viongozi wa dini wakiongea hawasikilizwi..
Suluhisho ni kuomba sana Mungu atende miujiza...
Hakuna mungu anakuja kukusaidia kwenye hili, kwani mmeanza kuomba leo mbona hajibu, hao watumishi wenyewe ndio wako meza moja na watawala mtafanya nini sasa. Bila wananchi wenyewe kuamua hamna kitu kitabadilika.
 
Zamani Mungu alitujibu kwa wakati sisi kama Tanzania...ila kwa sasa dhambi zimezidi....ushoga unaachwa wazi na chukizo kubwa kwenye Taifa...nani atasema na sisi?? Viongozi wa dini wakiongea hawasikilizwi..
Suluhisho ni kuomba sana Mungu atende miujiza...
Nchi haitakombolewa kwa maombi pekee my dear
 
Hii nchi ukiongea utapotezwa au kuuwawa.
Ukijidai muongeaji sana unapewa kesi isiyo na dhamana ili unyamaze
Ukikosoa watawala wanaweza kutoa maamuzi juu yako bila kujali sheria

kilichobaki ni wananchi kutumia haki yao kuandamana kwa nguvu maana kuvumilia huku kukifika mwisho ndio mwanzo wa kuzaliwa vikundi vya magaidi kwenye nchi.
Si unakumbuka lakini last year kilichotokea October?
 
Mkuu hakuna linaloshindikana duniani, I can tell you this thing can happen anytime and anywhere.

Zingatia chuki iliyopo Sasa kati ya

Wananchi dhidi ya watawala.

Wananchi dhidi ya vyombo vya ulinzi.

Utanganyika dhidi ya Uzanzibar

Ikitokea access ya silaha tuu, utaona badamu batakavyomwagika.

Binafsi sipendi na wala siombei tufike huko na ndio maana Bado Imani yangu nimewapa TEETH kwamba kuna jambo wanaweza kulifanya na nchi ikatulia.
Tatizo operation za teeth Huwa wanna balance equation kati ya wabaya na wema kwenye jamii!!

Jaribu kufikiri kama huko jikoni wakiandaa operation ondoa msoga,kizimkazi and co lazima ita cost maisha ya Mhaini gerezani,Tata wa katiba mpya alieanguka juzi n.k!!

Hii Huwa inauma sana,coz elimination process ya waovu huenda na wema ili ku balance mambo!!

Lakini wahusika hicho ndio kiapo chao!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom