Tutaendelea KUOA vituko kwa sababu vinaakili

Tutaendelea KUOA vituko kwa sababu vinaakili

Hii ni mada pana sana zaidi ya Kibo10 anavyofikiri. Binadamu huenda wakabadilika tabia, mitazamo, na kimaamuzi kutegemeana na tofauti ya mazingira ya awali na ya sasa. Ikiwa tu kuna tofauti basi tegemea lazima binadamu atabadilika. Nakumbuka classmate wangu mmoja aliolewa na daktari na kwa kipindi kile binti alikuwa katika mazingira fulani ya kijijini, akaletwa mjini akasomeshwa clinical officer huko Mtwara na mmewe akimgharimia. Alipokuwa Mtwara kwa kuwa sasa aling'aa, akapendeza na mazingira yakawa mazuri akawa na mahusiano na DC wa huko. Alipomaliza chuo mmewe kama kawaida katuma nauli ya ndege na akawa anamsubiri airport Dar pale. Hadi siku nyingine inafika mke hajaonekana na ndege zote zimetua na hata ile ya Mtwara siku hiyo imetua. Kumbe binti zake na DC huko wameruka hadi Nairobi kula maraha na binti kajisahau kabisa. Of course binti alikuwa mzuri. Kwa hiyo mimi naweza kusema hili jambo ni pana na kila mtu ana tafsiri yake. Hata ukioa wanawake 10 wote watakuwa tofauti, kimtizamo, kiakili, kimaumbile, kibusara, ila kwa maana ya kwamba utapata perfect siyo kwa hata nyie wanaume hamko perfect. Binadamu yeyote hayuko perfect. Kiasi kile unachoweza kuvumilia tabia ya mwingine ndio allowance ya furaha kwa mwingine. Nawasilisha.
 
Nikutane Na mdada, tuwe marafiki, tufikie uchumba, nitoe mahari(tena nyingi), nimue alafu nimuite "kituko"?..sasa hapo kituko atakuwa nani??
 
Tangu nianze kujijua kuwa mi ni mwanamke nimeona wameolewa wa kila aina, wazuri, wabaya, malaya, washika dini, washamba, watoto wa mjini wanaojua club, wasomi, wasiosoma, wenye akili, wajinga, wachafu, wasafi na kila aina za wanawake unaowajua.
We chagua wako, wengine watachagua wengine. Kuolewa ni bahati, wasemavyo watu.
Nina rafiki zangu wawili, kama wangekua wanaoa kutokana na hayo mnayoyasema pengine ningeolewa kabla au mwingine asingeolewa kabisa, Ila mashost wako wanalea kwenye miji yao.
Kwa hiyo, msitutishe sababu mnayosema si kweli mnafanya hivyo.
Wanaishi maisha ya aina gani hao watu...au ni kuweka alama tu wameolewa..?!
 
Tena siku hizi wanavyojiuza fb na instagramu kwa kurundika picha unaweza ukasema Mungu akupe nini. Usijaribu utajuta, achana na hawa mademu wanaouza sura mitandaoni. Tena ukitaka kama unakutana na demu kwa mara ya kwanza wewe msachi facebook na insta ukiona karundika picha kimbia kabisa. Sisi hatuangalii ------ ama kuacha matiti nje tunaka mwanamke wa kuishi maisha bia bugudha, kuasidiana maisha. Si unaoa mwanamke killa week mara send off mara kitchen part mara sijui wapi aaaah
 
cc: Masogange, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, na wasanii wanawake wote wa bongo fleva na movie.
 
kama ipo ipo tu....................

kuna magube gube yalioshindikana na mitume lakin yameolewa

Mmmh...sasa kama ata mtume kayashindwa sasa huyo mme aliyeyaoa atayawezaje?si kujitafutia balaa huko....
 
Back
Top Bottom