tena ujumbe wa maana hasa.
walikurupuka...kkutana na mtu club usiku...kapewa mchezo katangaza ndoa...anataka kutulia mwenzi bado anataka clubKuna watu yatawaliza humu jamvini we subiri tu!
Tangu nianze kujijua kuwa mi ni mwanamke nimeona wameolewa wa kila aina, wazuri, wabaya, malaya, washika dini, washamba, watoto wa mjini wanaojua club, wasomi, wasiosoma, wenye akili, wajinga, wachafu, wasafi na kila aina za wanawake unaowajua.
We chagua wako, wengine watachagua wengine. Kuolewa ni bahati, wasemavyo watu.
Nina rafiki zangu wawili, kama wangekua wanaoa kutokana na hayo mnayoyasema pengine ningeolewa kabla au mwingine asingeolewa kabisa, Ila mashost wako wanalea kwenye miji yao.
Kwa hiyo, msitutishe sababu mnayosema si kweli mnafanya hivyo.
Acha kuumwa roho, ndo maana mtoa uzi kasema hayo yalitokea kwa sababu wanaume walikuwa bado gizani ila baada ya kuzinduka wamegundua siri ya urembo si Makalio, weupe, unene, wala nini bali mwanamke mwenye maono na si maono ya kujua vilabu na majina ya mitaana, saloon na boutiques zote. Bali yule anyejua kesho ipo na hivyo kuna haja ya kujipanga kwa kesho kwa ajili ya kesho. Walioolewa ni bahati tu.