Tusiwe wajinga, CHADEMA wana makosa gani iwapo hatujawahi kuwakabidhi uongozi wa nchi?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Nimekuwa natafakari tambo na uongo wa viongozi wajuu wa CCM dhidi ya CHADEMA. Mpaka wachambuzi nguli kama Pascal Mayalla wamediriki kutamka kuwa CDM haijawa tayari kukabidhiwa nchi.

Nimejiuliza kipindi cha kugombea uhuru, TANU ilikuwa na watu wachache mno lakini wasomi ndo walikuwa haba kabisaa. Lakini kupitia uchache huo walifanya juhudi kubwa kudai uhuru na hatimaye tukapewa nchi yetu.

Leo ni wazi, malengo ya uhuru yamefutika kama nyika kavu mbele ya moto kwani,

  1. uhuru umetuzalia wakoloni wapya ndani ya CCM,
  2. uhuru umetuibulia makaburu wapya chini ya CCM
  3. Uhuru umetuletea majizi mapya ya rasilimali zetu chini ya CCM
  4. Uhuru umetupatia wauaji na wakandamizaji wa haki za binadamu chini ya CCM
  5. Uhuru umetuletea demokrasia mpya ya kuiba kura kuisaidia CCM
  6. Uhuru umetuletea wanasiasa waongo kutoka CCM kuliko shetani mwenyewe
  7. Uhuru umedunisha maendeleo ya Watanzania kwa kiwango kikubwa
  8. Uhuru umetuletea elimu isiyoendana na hitaji la taifa kiuchumi, kisayansi na kisekta
Hayo na mengine mengi ndiyo matunda yetu ya uhuru miaka 62 sasa.

Kinachotukwamisha ni ilani ya CCM inayopigiwa chapuo na wachumiatumbo wengi

Kinachotukwamisha ni matumizi maovu ya vyombo vya dola ambapo kwa viapo vyao neno uzalendo ni kuibeba CCM.

Kinachotukwamisha ni katiba mbovu ya chama kimoja (CCM) kutumika katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.

SWALI
Ni jambo gani CHADEMA wamefeli kwenye maongozi ya nchi kiasi kwamba wanashambuliwa sana na dola na CCM kuwa hawawezi kuongoza nchi?

Dhambi hii itatutafuna CCM daima

C: Erythrocyte Gwappo Mwakatobe johnthebaptist GENTAMYCINE GENTAMYCIME zitto junior Lumumbap Kiranga Mzee Mwanakijiji Retired
 
Back
Top Bottom