Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,969
- 30,314
kopites said:
''Watu wanacheza bao,kunywa kahawa cku nzima,wanawaza simba na yanga tu kwa nini wasizidiwe ujanja.''🤣🤣
JIBU LANGU KWA KAPITES
Mathalan nikikuomba ushahidi kuwa wazee wangu walikuwa wanacheza bao na kunywa kahawa siku nzima na wanawaza Simba na Yanga unaweza kuuweka hapa?
Kahawa na kucheza bao ni katika mila za watu wa Pwani kama wengine wanavyokunywa pombe za kienyeji katika vilabu vya pombe zinazouza dengerua, mbege, kimpumu nk.
Hawa unaowakejeli wewe kuwa ni ''wanywa kahawa na kucheza bao'' ndiyo waliounda chama cha TANU na kupiogania uhuru wa Tanganyika.
Soma majina ya ''wanywa kahawa na wacheza bao'' waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo August 1954:
Rajab Diwani, Abdul na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Julius Nyerere, Mshume Kiyate, Max Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Rashid Ali Meli, Clement Mohamed Mtamila, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafungo, Schneider Abdillah Plantan, Iddi Tulio, Marsha Bilal na Denis Phombeah aliyekuwa Meneja wa Arnautoglo.
Soma pia hapo chini majina ya ''wanywa kahawa na wacheza bao'' walioasisi African Association mwaka wa 1929 na kujenga ofisi ambapo leo ndipo lilipo jengo la CCM Lumumba Avenue:
Kleist Abdallah Sykes, Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.
Naomba nami nikuulize wakati hawa ''wanywa kahawa'' wanawatayarisha Watanganyika kupigania uhuru wazee wako wewe wanywa pombe za kienyeji siyo siku nzima bali kwa nyakati maalium walikuwa wanafanya nini?
Mwangalie Mwalimu Nyerere hapo chini na ''wacheza bao kutwa nzima na wanywa kahawa'':