Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
MAMA NA MWANA WAZALENDO WAPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Huenda historia ya Bi. Mwamtoro bint Chuma na mwanae Haydar Mwinyimvua ikawa ndiyo historia ya pekee ya mama na mwana wote wawili na kwa pamoja walikuwa katika TANU mstari wa mbele wakipigania uhuru wa Tanganyika.
Nyumba ya Bi. Mwamtoro ilikuwa nyuma ya ofisi ya TANU ikawa Mwalimu Nyerere alipokuwa anataka kufanya mkutano wa ndani alikuwa akimuomba Bi. Mwamtoro avunje ua wake waunganishe na ua wa TANU ipatikane nafasi kubwa kwa wanachama kukusanyika mahali pamoja.
Hili lilikuwa likifanyika na kufanya nyumba ya Bi. Mwamtoro kuwa moja ya viwanja na ngome ya TANU katika kupambana na wakoloni.
Rashid Mfaume Kawawa alipata kusema kuwa endapo nyumba hii inataka kuuzwa basi asiuziwe yeyote ila chama cha TANU kwa kuwa TANU ina historia kubwa na nyumba hiyo.
Nyumba iko nyuma ya Ofisi Ndogo ya CCM.
Inasikitisha kuwa ni watu wachache sana hivi sasa wanajua historia ya nyumba hii na historia hii ya mama na mwana.