SoC01 Tusiwageuze traffic polisi mafisadi

Stories of Change - 2021 Competition

Mulokozi GG

Member
Jul 14, 2021
34
44
Tamaduni na matendo yetu kama binaadamu ni muunganiko na matokeo ya tabia ndogo ndogo tuzifanyazo kila siku. Hivyo mtu anaye ishi maisha yake kama jambazi, mwizi au fisadi hakuzaliwa hivyo bali alilelewa hivyo. Kwa maneno mengine fisadi au jambazi sugu analelewa na kufundishwa tabia hiyo na watu wake wakaribu na jamii inayo mzunguka kwa ujumla, iwe kwa kujua au kwa kuto kujua. Kwani ni uhalisia mbuyu huanza kama mchicha na chatu huanzia kwenye yai dogo tu.

Ilianza kwa kufichwa fichwa ikiwa ni tabia inayo kemewa vikali hadhalani, baadae ikachukuliwa kama njia ya kuwapoza kwenye majukumu yao. Sahivi umegeuka utaratibu traffic akilisimamisha gari barabarani, hasa hasa magari ya abiri(daladala) na magari ya mizigo, njia nyepesi ya kuafikiana naye ni kumpa pesa kidogo tu.

Maalumu nikizungumzia mkoa wa Dar es salaam kama kitovu cha Tanzania kwenye biashara. Dereva au kondakita gari lake likipewa ishala ya kusimama na traffic moja kwa moja anakuwa anajua kuwa anapaswa ampatie pesa kiasi kadhaa. Sababu traffic wanakuwa katika vituo tofauti tofauti ikitokea kondakita ametoa pesa mara kadhaa na amechoka akionesha dalili ya kutotaka kutoa pesa tena, huyo ataonekana ana kiburi, jeuri, mbishi na bila hata kujua ndiye anaye geuka na kuonekana kama anavunja sheria kwa kukataa kutoa hongo. Bahati mbaya ni kiasi kidogo sana kinacho walidhisha wakasahau kuutimiza wajibu wao ndani ya Taifa na kulijengea Taifa tabia ya kibadhilifu.

Traffic wanapeana zamu na kushindana kusimamisha magari siyo kwa lengo la kukagua ushuru ambao haujalipwa au mapungufu kwenye hayo magari bali kwa lengo la kupewa pesa kidogo na makondakita. Wanakuwa wapole kama maji kwenye mtungi wakiisha pewa pesa hiyo, wanasahau majukumu na thamani ya vazi wanalo livaa katika Taifa.

Mfano kulingana na taarifa tofauti tofauti kwa siku moja traffic wanaweza kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi 15,000 hadi 30,000 kutoka kwenye kila gari(daladala) moja kwa siku. Kwa mjibu wa mamlaka ya udhibiti usafari aridhini(LATRA), mkoa wa Dar es salaam una takiribani daladala 600 zilizo sajiliwa. Kwahiyo pesa hii ni sawa na shilingi 3,240,000,000 hadi 6,480,000,000 kwa mwaka, hizi ni bilioni za kitanzania zinazo potea kwa mwaka mmoja tu.

Tabia hii ni dalili mbaya sana na inaumiza kuanzia wanao endesha magari hayo(dereva na kondakita), wanao miliki hayo magari, wanao simamia hayo magari (serikali) hadi wanachi na Taifa zima kwa ujumla. Hapa kiasi cha pesa wanacho kabidhi wanao endesha gari (dereva na kondakita) kinapungua na malipo yao vile vile yanapungua, anaye miliki gari hapati faida kama ilivyo kusudiwa, serikali haipati kodi kulingana na mapato halisi ya gari hivyo inakosa pesa za kuendeshea shughuli zake za kila siku na matokeo yake ni kupandisha au kuanzisha kodi mpya zinazo kuwa mzigo usio himilika kwa wananchi.

Hamna tatizo lolote juu ya pesa wanayo lipwa au kupewa traffic kwani ni wazi kazi wanayo fanya ni kubwa na ya muhimu sana, kuhakikisha na kuendeleza usalama barabarani. Changamoto ni jinsi wanavyo pewa hiyo pesa. Traffic anaye omba na kupokea rushwa ya shilingi 2,000 au 3,000 hadi 5,000 leo barabarani, huyu huyu ndiye anaweza kuwa mkuu wa idara yoyote hapa nchini miaka michache mbele. Je akiwa na ili tabia yake aliyo ijengea barabarani ya kuomba na kupokea rushwa, ni nini atakifanya kama matokeo ya tabia hii ikisha komaa na akiwa mkuu wa idara? Kama siyo wizi, ubadhilifu na ufisadi ulio kubuhu.

Kama mishahara wanayo pewa traffic haitoshi kukidhi mahitaji yao kiasi cha kuwasababishia kuomba na kupokea rushwa Viongozi wa ngazi za juu serikalini wakiendelea kukaa kimya, TAKUKURU wakiwa wanaendeleza kampeini za kukataza rushwa lakini hawawachukulii hatua yoyote traffic hawa.

Kinacho weza kufanyika, badala ya kuacha traffic kuendelea kuchukua rushwa hii, kila gari liwekewe ushuru angalau shilingi 100 au 200 kwa siku au wiki, kwa ajiri ya nyongeza ya mishahara au posho ya mauzulio/utendaji kwa traffic. Baada ya hapo traffic atakaye onekana akiomba au kupokea rushwa siyo tu aachishwe kazi bali awe na mda wa kutumikia gerezani kadiri sheria itakavyo ona inafaa.

Hii itaepusha na kuiondoa tabia hatari iliyo changa na inayo lelewa na kuendelezwa ndani ya jamii yetu ya traffic kukusanya pesa kiasi na kwa njia wanazo zitaka, pia italeta usawa kwa traffic wote kupewa malipo au posho sawa kulingana na utendaji wao na kuwafanya wawe na utumishi unaofuata usawa, haki na sheria kwa wote na kuondoa visasi, upendeleo na rushwa kwenye jamii yetu.
 
Back
Top Bottom