Mradi wa Usalama Barabarani SMART TRAFFIC MANAGEMENT

Mradi wa Usalama Barabarani SMART TRAFFIC MANAGEMENT

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,133
Reaction score
166,018
Kuna mradi wa Usalama Barabarani unaitwa SMART TRAFFIC MANAGEMENT ambao unahusu kufunga Camera za usalama kwenye barabara kuu zote za Tanzania. Lengo ni kupunguza ajali na makosa yote ya usalama Barabarani.

Mradi huu utatekelezwa kupitia mfumo wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP) kwa ushirikiano kati ya:
  • Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Tanzania Police Force Corporation Sole
  • Kampuni ya Rom Solution Ltd

Lengo kuu ni:
  • Kupunguza na kuzuia ajali za barabarani.
  • Kuongeza utii wa sheria za usalama barabarani.
  • Kuboresha uwezo wa askari wa usalama barabarani katika kufuatilia makosa.
  • Kuimarisha ulinzi na usalama kwenye barabara kuu nchini.

Mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili
1786110324290.png


Taarifa zinasema, huu mradi unakwenda kutumia pesa nyingi mara karibia mara tatu ya uhalisia wake na namna pekee ya kulizilipa ni kuongeza faini kwa kila kosa watakalolifanya watumia vyombo vya moto.

"Wewe kula kwa urefu wa kamba yako"
Alisikika mlevi mmoja kwenye vilabu vya Ulanzi huko kijijini kwetu Ngalanga...
 
Back
Top Bottom