Tujifunze kwa Uturuki tusiwe mazombi jamani

george aloyce

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Posts
1,302
Reaction score
2,035
Ziara ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Uturuki tarehe 17-20 April: Tunaangazia machache:

Mambo 11 muhimu ziara ya Mh. Rais kuangazia kila nchi tunayohusiana nayo kujua tunavuna au tunavunwa au sote tunavunana. Kwa hio inatufanya kuiangazia hii nchi na kulinganisha mambo kadhaa ili tuone tunajifunza nini kwao:

Hili linapaswa kufanyika kabla ya ziara ili kuongeza tija kwenye DIPLOMASIA YA UCHUMI:

1. Uturuki ina watu milioni 85 yaani ni zaidi ya watu milioni 23 kwa wa Tanzania....wakati Tanzania ina watu 62 Milioni kwa takwimu za 2022

2. Pato la mtu mmoja yaani Per capita kwa Uturuki ni 37,090 USD yaani mara 37 ya Tanzania maana Tanzania wastani wa pato kwa mtu ni 1,100 USD tuu

3. Ukubwa wa uchumi wa Uturuki kwa pato ghafi ni GDP bilioni 907 USD yaani ni mara 12 ya Tanzania..wakati Tanzania ni 75 bilioni USD tuu kwa takwimu za 2022

4. Ukuaji wa uchumi wa Uturuki ni wastani wa 5.5% unaofanana kwa karibu na Tanzania maana hata Tanzania wastani kwa sasa ni 5.1% japo wametuzidi kidogo

5.Tanzania inaagiza toka kwao yaani Import from Turkey 347 Milioni USDs na kuagiza kunaongezeka kwa 17%y, hasa tunaagiza mbolea, vyuma na nafaka...TUNAAGIZA BIDHAA SIO MALIGHAFI GHAFI

6.Tanzania inasafirisha mazao kwenda Uturuki yaani Export ya 40 Milioni USD yaani pungufu ya chini ya mara 9 hivi ya tunachoagiza toka kwao.. ongezeko 14% tumbaku ghafi, kopa, plastic scrap.....yaani mazao GHAFI

7. Ukubwa wa nchi ya Uturuki ni 783,562 Sq.km wakati Tanzania ni 945,087 sq.km yaani Tanzania ni kubwa zaidi ya km za mraba 161,525

8. Kuhusu Maendeleo ya WATU, Uturuki wametuzidi mbali maana ni nchi ya 45 hivi kati ya nchi 190 wakati Tanzania ni nchi ya 167/190 kwa takwimu za 2024

9. Mazingira ya ufanyaji biashara Uturuki ni bora zaidi kuliko Tanzania maana ni nchi ya 33 kati ya nchi 190 wakati Tanzania ni nchi ya 141/190

10. Uturuki ni nchi inayofuuata mfumo wa uchumi mchanganyiko lakini udhibiti wa serikali ni mkubwa zaidi pengine tofauti na Tanzania wakati wa Mzee Ruksa, JK na Samia na kufanana na wakati wa Awamu ya kwanza na wakati wa Magufuli

11. Mshahara kima cha chini ni zaidi ya TZS 1,000,000 wakati sisi tunaongelea 370,000
Tunajifunza na Tunaona haya ili wakati tuasikiliza hotuba za Wakuu wetu wa Nchi Tunaona wapi tunavuna na wapi wao wanavuna na lengo TUPATE NA KUINUA TIJA YA DIPLOMASIA YA UCHUMI yaani ECONOMIC DIPLOMACY:

1.Nchi hizi mbili zinatofautiana sana kwenye ufanyaji biashara kati yao hasa kwa thamani ya biashara...Tanzania inaonekana kusafirisha malighafi tena ya thamani ndogo ukilinganisha na tunachoagiza toka Uturuki...Maana yake tunavunwa

2. Nafaka na Mbolea toka UturuKi sio biashara ya kuendekeza. Ni wakati sasa wa kuzalisha Nafaka sisi maana ardhi ipo na watu tunao pengine tuanze sasa PIVOT FARMING tuajiri vijana wetu ili kuzalisha ngano, alizeti, mchele nknk na kuondoa kabisa uagizaji toka nje. Mbolea pia tuzalishe wenyewe maana soko lipo ndani ya nchi na nje ya nchi

3. Hapa tunapaswa kuachana na kusafirisha mazao ghafi, tuongeze thamani ili tuvune zaidi na kuongeza ajira kwa watu wetu.

4. Tuzalishe zaidi tuuze nje zaidi ikibidi tuwazidi

5. Watu wengi zaidi washiriki kwenye uchumi ili kuongeza pato la taifa na mtu mmoja mmoja na hapa mfumo wetu wa uchumi uachane na fikra za kijamaa na kuwa na mfumo mpya ambao ni JUMUISHI

6. Naamini kabla ya ziara huwa tunachakata taarifa hizi ili kuvuna zaidi na kunufaika kimkakati na ziara hizi hasa kufikia malengo ya diplomasia ya uchumi

7. Kila Balozi anapaswa kuwa na takwimu hizi kwenye nchi anayosimamia ili kupimwa kwa kupunguza pengo na kunufaika na mkakati maalum wa kusawazisha tofauti tulizonanzo kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya Tanzania zaidi....

8. Mazingira ya ufanyaji biashara ndio msingi wa ukuaji wa uchumi...tujifunze toka Uturuki

9. Maendeleo ya watu ni maendeleo ya nchi...Tanzania kuwa nchi ya 16 kati ya nchi 190 haina afya na pia kwa mujibu wa sera yetu ya elimu na mafunzo 84% ya wafanyakazi wake wana maarifa ya chini....Tujifunze Uturuki

10. Tuwaze zaidi ili kuanza kusafirisha HUDUMA badala ya biashara hii iliyozoeleka ya vitu na malighafi...Tujifunze Uturuki

11. Kima cha chini cha mshahara kitufikirishe na tuone cha kufanya hasa kukuza uchumi uweze kubeba kima cha chini cha juu zaidi ya sasa. Tuna mengi kujifunza toka Utuuruki

1707163784076.jpg
 
Mada nzuri sana hii..yani umeielezea vzr mnoo mpk unatamani mtu ukimbie shambani ukalime...unawaza hizi hekari maelfu kwa maelfu ziko tuu wazi hakuna lolote linaendelea..hakuna kilimo hakuna ufugaji hakuna viwanda...tutapata lini kiongozi mwenye maono?? Zaidi ya hawa corrupted leaders?..
 
Viongozi wanawaza uchaguzi ujao. Wapo wanawaza kampeni na jinsi ya kuiba kura. Bila kusahau kuiba hela 🤣
 
Ni Tusi kubwa kufananisha Tz na uturuki..

Inabidi uchukuliwe Sheria Kwa kuichafua uturuki🤒

Karne ya 21 bdo tunakimbiza mwenge tena Kwa budget kubwa ambayo ingesaidia hata kuwakopesha vijana na kurudisha Kwa riba nafuu ili kutengeneza walipa Kodi wengi. So sad😥
 
Kitu kinachohtajika Tanzania ni elimu displin na Oder basi. Mengine story mzee. Hiz elimu zetu za kuwafanya vijana maboss badala ya wataalamu ni hatar. Vijana wapewe elim ya ufundi Zaid sio kuvaa tai na perfume
 
Kwa uchumi huu wa viongozi na wanasiasa kujinufaisha wao kwanza na kuacha wananchi wakiwa hakuna pa kwenda tusahau suala la maendeleo kabisa au hata kuwafikia nchi zilizoendelea.
 
Wazo la kulima kwa kumwagilia kutumia pivot ni zuri. Kama serikali ingejenga mabwawa ya kukusanya maji ya mafuriko kisha wakafunga hayo mapivot tungekuwa mbali mno. Ila sasa maji yazagaa bure tu na kuleta mafuriko.
 
Uturuki ni ya 19 kiuchumi duniani,Tanzania ni ya 78,ni jambo zuri kama changamoto lakini uuwiano haupo.

Sisi hapa bado CAG anasema pesa zilizotengwa kwa ajili ya madawa zilitoka hazina lakini hazikufika MSD.
😂😂.
 
Edogan kaipaisha sana Uturuki kwenye utawala wake.
pamoja na mazuri yake yoye hayo lakini bado washirika wa Nato walipanga njama za kumpindua wananchi wakamlinda na mapinduzi.
 
Ahsante sana mleta mada. Kwa kweli umedadavua vizuri sana. Raisi na viongozi wote wanapaswa waisome hii.
Ziara ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan nchini Uturuki tarehe 17-20 April: Tunaangazia machache:

Mambo 11 muhimu ziara ya Mh. Rais kuangazia kila nchi tunayohusiana nayo kujua tunavuna au tunavunwa au sote tunavunana. Kwa hio inatufanya kuiangazia hii nchi na kulinganisha mambo kadhaa ili tuone tunajifunza nini kwao:

Hili linapaswa kufanyika kabla ya ziara ili kuongeza tija kwenye DIPLOMASIA YA UCHUMI:

1. Uturuki ina watu milioni 85 yaani ni zaidi ya watu milioni 23 kwa wa Tanzania....wakati Tanzania ina watu 62 Milioni kwa takwimu za 2022

2. Pato la mtu mmoja yaani Per capita kwa Uturuki ni 37,090 USD yaani mara 37 ya Tanzania maana Tanzania wastani wa pato kwa mtu ni 1,100 USD tuu

3. Ukubwa wa uchumi wa Uturuki kwa pato ghafi ni GDP bilioni 907 USD yaani ni mara 12 ya Tanzania..wakati Tanzania ni 75 bilioni USD tuu kwa takwimu za 2022

4. Ukuaji wa uchumi wa Uturuki ni wastani wa 5.5% unaofanana kwa karibu na Tanzania maana hata Tanzania wastani kwa sasa ni 5.1% japo wametuzidi kidogo

5.Tanzania inaagiza toka kwao yaani Import from Turkey 347 Milioni USDs na kuagiza kunaongezeka kwa 17%y, hasa tunaagiza mbolea, vyuma na nafaka...TUNAAGIZA BIDHAA SIO MALIGHAFI GHAFI

6.Tanzania inasafirisha mazao kwenda Uturuki yaani Export ya 40 Milioni USD yaani pungufu ya chini ya mara 9 hivi ya tunachoagiza toka kwao.. ongezeko 14% tumbaku ghafi, kopa, plastic scrap.....yaani mazao GHAFI

7. Ukubwa wa nchi ya Uturuki ni 783,562 Sq.km wakati Tanzania ni 945,087 sq.km yaani Tanzania ni kubwa zaidi ya km za mraba 161,525

8. Kuhusu Maendeleo ya WATU, Uturuki wametuzidi mbali maana ni nchi ya 45 hivi kati ya nchi 190 wakati Tanzania ni nchi ya 167/190 kwa takwimu za 2024

9. Mazingira ya ufanyaji biashara Uturuki ni bora zaidi kuliko Tanzania maana ni nchi ya 33 kati ya nchi 190 wakati Tanzania ni nchi ya 141/190

10. Uturuki ni nchi inayofuuata mfumo wa uchumi mchanganyiko lakini udhibiti wa serikali ni mkubwa zaidi pengine tofauti na Tanzania wakati wa Mzee Ruksa, JK na Samia na kufanana na wakati wa Awamu ya kwanza na wakati wa Magufuli

11. Mshahara kima cha chini ni zaidi ya TZS 1,000,000 wakati sisi tunaongelea 370,000
Tunajifunza na Tunaona haya ili wakati tuasikiliza hotuba za Wakuu wetu wa Nchi Tunaona wapi tunavuna na wapi wao wanavuna na lengo TUPATE NA KUINUA TIJA YA DIPLOMASIA YA UCHUMI yaani ECONOMIC DIPLOMACY:

1.Nchi hizi mbili zinatofautiana sana kwenye ufanyaji biashara kati yao hasa kwa thamani ya biashara...Tanzania inaonekana kusafirisha malighafi tena ya thamani ndogo ukilinganisha na tunachoagiza toka Uturuki...Maana yake tunavunwa

2. Nafaka na Mbolea toka UturuKi sio biashara ya kuendekeza. Ni wakati sasa wa kuzalisha Nafaka sisi maana ardhi ipo na watu tunao pengine tuanze sasa PIVOT FARMING tuajiri vijana wetu ili kuzalisha ngano, alizeti, mchele nknk na kuondoa kabisa uagizaji toka nje. Mbolea pia tuzalishe wenyewe maana soko lipo ndani ya nchi na nje ya nchi

3. Hapa tunapaswa kuachana na kusafirisha mazao ghafi, tuongeze thamani ili tuvune zaidi na kuongeza ajira kwa watu wetu.

4. Tuzalishe zaidi tuuze nje zaidi ikibidi tuwazidi

5. Watu wengi zaidi washiriki kwenye uchumi ili kuongeza pato la taifa na mtu mmoja mmoja na hapa mfumo wetu wa uchumi uachane na fikra za kijamaa na kuwa na mfumo mpya ambao ni JUMUISHI

6. Naamini kabla ya ziara huwa tunachakata taarifa hizi ili kuvuna zaidi na kunufaika kimkakati na ziara hizi hasa kufikia malengo ya diplomasia ya uchumi

7. Kila Balozi anapaswa kuwa na takwimu hizi kwenye nchi anayosimamia ili kupimwa kwa kupunguza pengo na kunufaika na mkakati maalum wa kusawazisha tofauti tulizonanzo kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya Tanzania zaidi....

8. Mazingira ya ufanyaji biashara ndio msingi wa ukuaji wa uchumi...tujifunze toka Uturuki

9. Maendeleo ya watu ni maendeleo ya nchi...Tanzania kuwa nchi ya 16 kati ya nchi 190 haina afya na pia kwa mujibu wa sera yetu ya elimu na mafunzo 84% ya wafanyakazi wake wana maarifa ya chini....Tujifunze Uturuki

10. Tuwaze zaidi ili kuanza kusafirisha HUDUMA badala ya biashara hii iliyozoeleka ya vitu na malighafi...Tujifunze Uturuki

11. Kima cha chini cha mshahara kitufikirishe na tuone cha kufanya hasa kukuza uchumi uweze kubeba kima cha chini cha juu zaidi ya sasa. Tuna mengi kujifunza toka Utuuruki

View attachment 2966019
 
Uturuki ni ya 19 kiuchumi duniani,Tanzania ni ya 78,ni jambo zuri kama changamoto lakini uuwiano haupo.

Sisi hapa bado CAG anasema pesa zilizotengwa kwa ajili ya madawa zilitoka hazina lakini hazikufika MSD.
[emoji23][emoji23].
Hizi ripot za cag hua zinaumiza masikio yg
 
Kitu kinachohtajika Tanzania ni elimu displin na Oder basi. Mengine story mzee. Hiz elimu zetu za kuwafanya vijana maboss badala ya wataalamu ni hatar. Vijana wapewe elim ya ufundi Zaid sio kuvaa tai na perfume
Kila kijana anawaza ajira
 
Back
Top Bottom