Tusipende kupiga watoto wetu

Tusipende kupiga watoto wetu

Drone Camera

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2017
Posts
14,121
Reaction score
14,032
Mtoto ni zawadi.Ndiyo alama yako utakayoacha hapa duniani. Hizo mali utakazoacha zitagombaniwa zitaisha.Ila jina lako atabaki nalo wewe na atalitumia kwa mjukuu wako kama jina lake la tatu. Tusitelekeze wala kuwapiga piga watoto.

Huwa najisikia vibaya pale mzazi au yoyote yule anamposhushia kipigo mtoto tena kilichozidi umri wake.Huku kitaa kuna mama huwa anampiga sana mwanae.Mwanae yupo la pili ni wa kike.Yule mtoto anafanya kazi nyingi jamani.Siku dogo alichelewa kurudi akarudi saa 9 badala ya saa 7 basi kaingia ndani tu hivi ndani kamsalimia mama kakutana na kipigo.Hapo hata hajauliza shida nn ya kuchelewa.

Kumbe dogo alikutana na wahuni wa shule huko yale madarasa ya juu wakampora baadhi ya vitu basi dogo akaenda kushitaki kwa ticha sasa hiyo process hadi ya kupata vitu vyake ndo muda ukapotea hapo.Sisi tumetulia hatuna habari tukashtushwa na kelele hiyo nyumba.Kelele yenyewe si ya kawaida! Ikabidi twende yawezekana shida ni kubwa.

Kumbe bhana sijui alikosa cha kumpigia humo ndani basi akatumia mwamvuli ile ncha iliyochongoka! Kampiga usoni! Mungu mkubwa alimiss jicho! La sivyo alikuwa analiondoa! Ilo usoni alimpompiga palianza kubreed! Sasa mtu wa hivi usipomuita mzazi ukamuita shetani utakuwa na kosa?

Jioni mzee wa nyumba aliporudi ikabidi amuulize kulikoni mwanae! Mtoto akajieleza vizuri huku baba anasikiliza kwa makini! Kilichofuata yule mama alitwangwa,alipigwa,alinyooshwa sana.Mimi huwa sipendi kuona au kusikia mwanamke anapigwa na mwanaume ila hiyo siku nilifurahi sana! Alipata dawa yake.Mtoto kama vile sio wake wa kuzaa.

Wengine hadi vitoto vidogo wakiwa wanaviogesha basi wanavichapa humo humo kwenye beseni.Vinalia hadi vinahuzunisha.Sio vizuri hivyo.
Wakati wa kutaka mwanao akuelewe kwa vipigo ushaisha huko! Mengine tuwaachie mababu zetu waliopenda waogopeke ili wakiingia nyumbani kutoka shamba basi watoto wajifiche.Huu muda ni wa kutengeneza urafiki na watoto wetu ili wawe huru kueleza changamoto zao kisha tuzitatue.

Watoto wa zamani waliwapenda bibi na babu zao sababu waliwasikiliza tofauti na wazazi waliopenda kutumia silaha ya mkono.
Mimi sitapiga mwanangu yoyote kabisakabisa.
 
Kwahiyo unapinga kipigo kilichozidi mtoto tu au unapinga kipigo kwa ujumla?...
kwamba wapigwe kwa kiwango chake au wasipigwe kabisa?

Kama jibu ni la pili nakupa pole sana kwani huna tofauti na aliyeenda kupambania suluba ziondolewe gerezani na jeshini matokeo yake... niishie hapo kwanza
 
Kwahiyo unapinga kipigo kilichozidi mtoto tu au unapinga kipigo kwa ujumla?...
kwamba wapigwe kwa kiwango chake au wasipigwe kabisa?

Kama jibu ni la pili nakupa pole sana kwani huna tofauti na aliyeenda kupambania suluba ziondolewe gerezani na jeshini matokeo yake... niishie hapo kwanza
Isizidi kiasi.Ila mimi najisemea upande wangu sitafanya hivyo.Hata baba yangu hakuwahi kunipiga.Mama mwenyewe kafanya hivyo mara chache sana!
 
Umenikumbusha, jana nilikuwa sehemu sasa kuna mtoto anamwambia mama yake nasikia njaa huku analia, yule mama alichukua fimbo akaanza kuchapa jamani, yule niliyekuwa nae akakosa uvumilivu alimsema sana yule mama.... Unakuta mzazi ana stress zake binafsi anamalizia kwa mtoto
 
Hakuna wazazi wanaopiga siku hizi,kipigo kilikuwa 1990s kurudi nyuma.
Shuleni moto Nyumbani moto.
Dingi akikumata hata mama hasogei,akikuachia unakaa mahali unajiuliza huyu ni baba yangu kweli?
 
Umenikumbusha, jana nilikuwa sehemu sasa kuna mtoto anamwambia mama yake nasikia njaa huku analia, yule mama alichukua fimbo akaanza kuchapa jamani, yule niliyekuwa nae akakosa uvumilivu alimsema sana yule mama.... Unakuta mzazi ana stress zake binafsi anamalizia kwa mtoto
Haya ya namna hii ndo yanafanya sisi wa pembeni tuumie na kukosa uvumilivu.Utafikir ni kosa la mtoto! Hapo ukimnunulia mtoto chochote cha kula unasolve kesi.
 
Back
Top Bottom