Vimbwanga na vituko vya boss wetu

Sela Son

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,620
6,079
WanaJF bila shaka mu wazima kama mimi. Mwaka mpya ndio huoo waja. Mola atufikishe. Amina.

Maisha ni safari ndefu sana tena sana. Watoto wa kisasa wakisikia kuwa uyaone wao hudhani ni maparachichi na machungwa watayaona.

Lakini duh utu uzima ni mzigo. Na hili lazima niliseme wazi. Nina miaka 42 sasa. Historia yangu si nzuri sana hadi leo ninaishi. Ni Mungu tu muokozi wetu anisaidia.

Ni miaka nane sasa toka nipate kazi katika ofisi fulani hapa mkoani. Hawanilipi fedha nyingi but zinanisaidia kusogeza siku katika kipindi hiki kigumu cha kiuchumi mi na mwanangu. Lakini bwana wee boss wetu ni shabiki kindakindaki wa club ya Simba.

Huwezi amini hao Simba wakifungwa humu kazini ni vimbwanga na vituko. Siku moja Simba kafungwa basi kadamkia kazini saa 11:00 alfajiri kapaki gari. Bwana we mbona tulikoma hivyo vitimbi. Kwa kawaida muda wa kazi ni sa 1:30 uwe umefika.

Haya Sasa hiyo siku aliyowahi hivyo wote tuliochelewa akatuita ofisini kwake na kutuambia kwanzia leo nyie ndo maboss na mimi ni mfanyakazi wenu. Akaniita Selason (Mimi huyo)we ndo meneja, huyu sijui not utakuwa hivi na vile. Mara hivi na vile.

Mi coz ndo mkubwa kiumri nikaomba msamaha basi akatusamehe kwa sharti Kwamba tusirudie Tena . Sasa basi hiyo hiyo siku akaingia jikoni kuna mpishi wake maalum katika eneo hili la kazi. Hakumkuta sijui kaenda wapi kuchukua sijui tangawizi sijui nini huko mtaani.

Basi akaingia jikoni hajamkuta. Cha ajabu kwa hasira akaanza kuosha vyombo na kugusa hiki na kile cha jikoni humo. Oya nyie anakera kichizi basi tu.

Mpishi anarudi anamkuta boss asuuza vyombo. "Hivi we mpumbavu kwanini vyombo ni vichafu hivi. Unakuwaga wapi nakulipa hela ya bure kupika yenyewe hujui" akapayuka. Basi kamfukuza yule dogo. Siku hizi pakula hana humwagiza bodaboda mmoja alete chakula coz tuko nje kidogo ya mji.

Juzi Kati Simba walidraw na Yanga wakashinda . Asubuhi kapaki ndinga anakagua ofisi zake uso umefura kwa hasira. Anakagua akute kosa tu apayuke makelele. Kaingia ofisi ya sekratari mtoto mwenyewe mpole hana muda hapa kazini basi kaanza makelele.

Yule mtoto kumbe hanaga uvumilivu kaanza kumchana boss kwamba asimzoee kumpigia kelele Mungu ndo mtoa riziki. Usinitishe we mzee halafu nakusikiaga mimi sio kama hao uliowafanya miskule ( eti ndo sisi) . Unajua akamjibuje . Hunijui utanifahamu. Dogo kamwambia eti kwendraaaa nikacheka ka chizi kuona hivyo.

We bwana wakati nacheka (ofisi zinatizamana) kumbe kaniona akanifata. Akaniambiaje eti we mzee kwenu hamna wakubwa. Mtoto ananidhalilisha we unacheka. Tutaonana mwisho wa mwezi utaondoka. Ndo hivyo mi nasubiri liwalo na liwe.

Ukitaka awe rafiki yake ukimuona asubuhi uanze kumchekeachekea na kumsifia Kwamba ye ndo kidume Yanga hamna kitu Simba ndo baba lao.

Humu ndani ana wambeya wake yaani chawas mmoja huitwa mchina (si jina lake halisi) na mwingine Yeremia. Basi hao uongelee wapi usiyaskie kikaoni? Hawana dogo washapeleka.

Juzi Kati mwanae kapata ajali ya gari kwa kugonga gari nyingine. Basi kaombwa laki nne amlipe aliyegongwa. Hasira za mwanae akahamishia kwetu.

Kiufupi boss wetu ni mswahili originally.Asikuone unaongea na simu utaskia ulikua unaongea na nani muda wote huu kilugha? Mnataka kuniroga ehh! Basi niwaambieni tu sirogeki mi ndo ....(Anataja jina lake). Na kufa sifi mpaka Mungu apende. Kenge nyie.

Duh ndo hivyo bwana vimbwanga vya boss wetu. Tuhadithiane vimbwanga vya maboss wenu huko tuskie wote au sio wana jf?
NB.
Boss wetu Hana mke. Wameachana toka 2007. Labda ndo maana ana stress.

Kwaheri.
 
Boss wangu wa zamani alikuwa anafanya nalia kila siku kikaoni asubuhi maana nina machozi ya jirani. Hasira zangu mimi mpaka nilie so akituchamba naishia kulia kazi zinaendelea.

Kikao ni kila siku asubuhi 8:30 - 9:00 ila siku akiamua kutusema mtatoka kikaoni saa 12. Hapo akija mteja kupata huduma anainuka mmoja anahudumia akimaliza anarudi kwenye kuchambwa.

Ila i miss him pamoja ya yote ana roho nzuri sana na huruma.
 
Kuna siku niliandika msg huyu Boss wangu ni khanithi mshahara mpaka leo hajatoa, sasa wakat nasend nikajikuta nimemtumia Boss badala ya Wife, halafu tulikuwa kwenye kikao pale sub scania, najitahid kuizuia waapi naskia imefika kwake nae akaifungua akaisoma akashusha miwani kisha akatabasamu.

Kikao kikaendelea lakini wakati huo mimi jasho linatoka na ndani unyunyu upo wa kutosha tu. Baada ya kikao kwisha ndio Boss akaniuliza kwa hiyo nishakuwa Khanith* sio? Ikabidi tu nimjibu ndio.
 
Mbona anafanana na boss wangu alikuwa ana vituko nyie siku akufurahi mtapata raha siku akinuna uwiii atachokonoa vitu ,atachunguza hadi maisha yako binafsi halaf anaanza kukupangia maisha yako binafsi uishu anavyopenda yeye alikuwa na vituko msomali yule
Kipindi cha magufuli anatulazimisha tumpigie kura maguful 😂😂😂
 
Boss wangu alikuwa na chawa wake yaani mkiwa mnafanya kazi si kuna ile mood inakata ya kufanya kazi unapumzika basi chawa anapiga simu kwa boss then boss anapiga kwa hr kuwa huyo alie pumzika mwambie haludi nyumbani akapumzike

Akija sasa unaaza kuchambwa mpaka mda wa kazi unaisha ndio unaachiwa huru
 
Back
Top Bottom