Tusiotumia pombe njoni tupeane pole

Tusiotumia pombe njoni tupeane pole

Dah...Pombe bana🙂🙂
Kazi kubwa ya pombe mwilini ni kutia uchizi..
Unapokunywa pombe...kimelea cha pombe(Ethanol) huingia kwenye damu na huenda kupenya katikati ya seli za ubongo na kukata/kuharibu mawasiliano na sehemu nyingine za mwili..ndiyo maana mlevi huwa anashindwa kujidhibiti...kujiona yeye ndiyo bora kuliuko binadam mwingine..kuongea/kucheka kwa sauti ya juu...kutukana...kupigana...kulia bila sababu....kuwa mzembe kwa kutovaa viatu.....na majuto yote huja baada ya pombe kuisha...na hiyo ndiyo huwa salama yake...kwani unywaji wa pombe uliokithiri huishia kwenye koma au kifo....Uamuzi ni wako.😀😀😀😀😀

Kazi ni kwao sasa mkuu.
 
watu wanafiki sana ;

wanajifanya pombe hawanywi ila kuvunja amri kumi za Mungu wanaona sawa.

katika zile amri kumi Mungu alizompa Musa hakuna mahali wamesema usinywe pombe.

wanafiki hao hao hawajui kusema uongo ni dhambi ila sio kunywa mvinyo.
 
Mnaokunywa pombe mnatupa shida sana
Sema wewe mdogo wangu.

Nimekumbuka mbali miaka ya nyuma tukiwa wadogo kulikuwa na jirani yetu huyo kila akirudi nyumbani amelewa hatari basi kazi yake ni kulia tu sa nikawa najiuliza faida ya pombe iko wapi hapo.
 
Kuepuka pombe kuna mitihani mingi sana! Ila acha niwe mshamba! Pombe sinywi!
Wala sio ushamba kaka ake. Nionavyo wale wanywaji ndio wanakuwaga washamba.

Sasa kama umekunywa kazi yako ni kupiga kelele njia nzima huo si ndio ushamba.
 
Back
Top Bottom