Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,662
Imenibidi nielezee masimago tunayopata/niliyopata katika kipindi chote ambacho nimekuwa na sijawahi kuonja pombe. Mwanzoni nilifikili hii tabia ya kudharauliwa kwa sababu ya kutotumia pombe iko nchini mwangu tu!!!, hali hii imenikumba hata ugenini na naomba nielezee tukio la jana.
Muda wa saa 11 jioni kulikuwa na kikao cha kugawana asilimia/ shares za kampuni baina ya mwenyeji wangu na baadhi ya jamaa wengine. Baada ya kumaliza tukachukuana kwenda Hotel, Nilipofika pale mtu wa kwanza akaagiza vinywaji ajabu hapakuwa na kinywaji hata kimoja baridi. Nikiwa namwangalia mwenyeji wangu kwa vile anafahamu Situmii tungi lkn ni kama alikuwa amepanga kunikomoa, baadae akaniangizia juice hivi nikawa nakunywa taratibu huku macho nikiyageuza kama kinyonga kuangalia wahudumu na mashuga mummy wakiingia kwenye hotel na vitu vya ukweli muda mwingine yameogozana na mabinti zao.
Baadae saa tatu kuelekea saa nne usiku likaanza disco hapo ndipo nilitaka kulia kwani hata kucheza disco nilikuwa naogopa huku wezangu wakikita ngoma kwa msaada wa tungi!! Sasa likaja li mama shombeshombe la kizungu likaninyongea mauno likiniomba nikacheze nalo!! Baadae lilipoona nakunywa juice, likashangaa likisema... Lol!! What a f..ck is this guy doing here!!!
Ilibidi nikakae kwenye gari na baada ya muda mfupi mwenyeji wangu alikuja tukaondoka na akiniambia pole sana na kama kawaida ya walevi siku zote huwa wanakupongeza kinafiki kuwa; hata mimi natamani niache pombe hivyo usijaribu kuiga, pombe ni mbaya sana!!!!