Tusijisahaulishe, masikini ni matokeo ya dhambi. Kabla ya hapo Mungu alipanga tuishi kifalme

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,603
15,404
Hii ni kweli. Mungu ni Tajiri mkubwa anayemiliki vyote. Na sisi ni watoto wake, na sifa ya mtoto ni kurithi vya baba. Hivyo kila anachomiliki Mungu ni cha kwetu.

Kabla ya udanganyifu wa Adam na Eva kula tunda tulikusudiwa binadamu wote kuwa matajiri sana na kuishi kifalme. Tukio la kuacha matunda zaidi ya mamilioni na vyakula vya asili zaidi ya milioni na kwenda kufakamia katunda kamoja kalikozuiwa ndio chanzo cha mitazamo ya kimasikini kwa mwanadamu (poverty mentality).

Ndio maana hadi leo hii dhana shetani anaoendeleza kutishia watu.

Wakati maji ni asilimia kubwa ya dunia lakini tunatangaziwa uhaba mkubwa wa maji.

Wakati ardhi ya chakula ni kubwa tunatangaziwa uhaba mkubwa wa chakula.

Wakati hali ya hewa ni nzuri oxygen ya kutosha, anatangazia watu kuna uharibifu mkubwa wa mazingira.

Wakati kuna aina malaki za nafaka, matunda, mboga za majani anakufanya upende tunda,nafaka au mboga za majani aina moja na mengine unaona kama ni makosa.

Haya yote ni matokeo ya fikra za umasikini (poverty mentality) ambazo ziliingizwa wakati wa dhambi. Mungu wetu ni mungu wa vingi (plenty mentality).
 
Jidanganye. Mungu ni kitu gani? Yuko wapi? Jinsia gani? Anakusaidia nini? Mmekalilishwa,mkalishwa mkameza ujinga,mnaanza kuwapumbaza watu. Hiyo mitabia pelekeni huko uzunguni mlipojaziwa matope
 
Jidanganye. Mungu ni kitu gani? Yuko wapi? Jinsia gani? Anakusaidia nini? Mmekalilishwa,mkalishwa mkameza ujinga,mnaanza kuwapumbaza watu. Hiyo mitabia pelekeni huko uzunguni mlipojaziwa matope
Huu ujinga umeanza hivi karibuni na watu ambao wanamisongo ya mawazo na lgbtqi wa ulaya. Naona unakua kwa kasi na tutatafuta namna ya kuwasaidia na nyie pia mkichoka huu ujinga.
 
Back
Top Bottom