WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Hii nii siku njema ya furaha na kwa kweli ya kufurahia.. ila sijui kama imesherehekewa na maadhimisho yameenda yalivyopaswa..
Kweli kabisa.Maisha yanafinya sana.Sherehe kama hii inakuwa siyo kipaumbele kwa mwananchi wa kawaida.Je, ni sahihi kusema ni sherehe ya serikali zaidi, na siyo ya wananchi?Watu wengi hatujasherehekea kwa furaha sana, maana kibano cha maisha kipo pale pale. bidhaa zipo juu, umeme nao wameshaomba kupandisha pei ya unit kwa 150%, mavazi, na nauri za kwenda mikoani zinazidi kupanda kwa kipindi hiki cha mwezi 12.
kama saa moja hivi ilopita nilizungumza na mdogo wangu akiwa 'kwa mama' na kumuuliza 'vipi sikukuu ya uhuru' akanijibu hakuna lolote la maana, hali ni ngumu. ni kama hakuna sikukuu tu.
Hatuwezi kusherehekea sawa kwa maana kuna wanaoshereheka wakiwa wanapiga mihayo huku wengine wakigonga glasi za wine,mvinyo na champagne,Sina maana mbaya ila kikubwa ni kutengeneza kwanza vitu vinavyoonesha UHURU kabla ya kukimbilia kushereheka kinafiki
Nyerere aliwahi kuandika na kusema 'Freedom&Development' na akasema hivi vitu ni sawa na kuku na yai ...kusherehekea Uhuru ni kusherehekea matunda na maendeleo ya Uhuru wenu,sasa leo,reli ni ileile,maradhi,umaskini na ujinga vimekithiri na kibaya zaidi urithi wa nchi yetu umeporwa huku shilingi ikishuka...tunashereheka nini?ardhi kuuzwa?mgao wa umeme?kufeli kwa wahitimu wa kidato cha 4?kuwa na serikali ya mashemeji,maswahiba na nyumba dogo ama labda kuwa na serikali isiyokuwa na uzalendo kwa wafanyakazi wake na wastaafu?
Niwatakie sherehe njema wale wote wanaoona kuna la kushereheka na niwape pole wenzangu kama mie tusiojua nini hatma yetu masaa kumi yajayo.
Mimi nimechinja mbuzi kufurahi uhuru wa Tanzania, nawahadithia wanangu maana ya uhuru ..
Uhuru ni continues struglle ..uhuru kiuchumi, kuwa huru kimawazo etc..
Pasipo kwanza kuziba pakacha habari zingine zote ni ndoto.. Ufisadi ni adui wa kwanza wa uchumi wa nchi yetu na hata kuleta maisha magumu iwe umeme hadi dawati la mwanafunzi shuleni. Huoni sasbabu ya kusherehekea kwa sababu ya uongozi mbovu ambao umeleta adha hizi zote..Bila kurudisha Miiko na maadili ya viongozi kwanza na kuhakikisha yanafanya kazi hakuna kitu tunachoweza kubadilisha - Good Governance inasimama mbele ya kila kitu...Leo ni siku muhimu sana kwa watanzania.Tunajivunia kufikisha miaka 50 ya kuwa nchi huru.
Tukiachilia mbali siasa, nadhani leo ni siku ya kila mmoja wetu kufurahi apendavyo.
Ukiweza jumuika na wenzio mcheze, muimbe, mrukeruke. Ukiweza fanya tafrija ule
na kunywa na wenzio.Bahati mbaya sana, uchumi mifukoni hauruhusu.Labda tuwezeshwe!
Nimefuatlia sherehe zinavyokwenda, na nimefarijika angalau
kushiriki kwa macho ( kupitia TV).Waliostahili wamepokea nishani zao kwa michango
yao katika kuleta uhuru na pia kwa utumishi uliotukuka.Aidha baada ya kupokea
nishani hizo, basi ni raha tu.Watu wanajumuika pamoja kwenye cocktail,
na huenda labda kutakua na maakuli badae.Sijui.Mradi ni raha tu, watu wanatabasamu
kuashiria furaha wanajichanganya na kushiriki mazungumzo na kupongezana.
Katika yote haya, nimejikuta nawafikiria wananchi walio wengi na kujaribu kujiuliiza. Hivi miaka
50 hii, ni kwa vipi labda wangeweza nao kujisikia wanasherehekea? Je ni kwa kuangalia TV,
kusikiliza redio au ni kusubiri simulizi?Huenda wengine walibahatika kushiriki maonyesho yaliyokuwa
yanafanywa na wizara mbalimbali kwa zaidi ya mwezi mmoja, kuanzia viwanja vya Mnazi MMoja
na hatimaye kilele leo kule Viwanja vya saba saba. Huenda pia walishiriki kwenye mkesha
na kujionea fataki.Lakini sina uhakika ni vipi wananchi hata 50% wamefikiwa
na sherehe hizi ukizingatia hali ngumu ya maisha yanayozikumba familia nyingi.
Huenda ingepokelewa kwa wema sana kama serikali ingefanya matendo ya huruma kwa wanachi
katika kipindi hiki cha sherehe kama:
1. Kuwapunguzia angalau adha ya umeme,nauli nk
2. Kuwapa huduma mbalimbali bure kwa kipindi maalum
3.Kuziwajibisha taasis zile zenye usugu wa kero za wananchi mf. rushwa za matrafiki barabarani.
4.Kuteua shule kadhaa za mfano na kuziewekea huduma kama vile madawati ya kutosha,
kuwapa wanafunzi madaftari na huduma nyingine, kuwajengea waalimu nyumba za bei nafuu
5.Kujenga angalau barabara mbili kila kata za kiwango cha lami na kuzipa majina ya waasis wa uhuru
6. Kuweka mabomba na visima vyenye kutoa maji hasa maeneo yenye usugu wa maji n.k.
Hii ni kwa uchache tu.
Nadhani haya matendo yangekuwa alama ya kudumu katika vichwa na fikra za wananchi kila wakikumbuka
miaka 50 ya uhuru kuliko shughuli nilizoziona zikifanywa kuashiria miaka 50 - kwangu nahisi kama vile
kumbukumbu haitakuwepo.Khanga, tshirt, vipeperushi, siyo vitu vya kudumu.
Viongozi wangu wasikivu, hamjachelewa sana.Bado mnaweza kufanya haya matendo mkawagusa wananchi.
Pesa sidhani ni tatizo.Inahitaji nia na dhamira tu.Nia ikiwepo, njia itapatikana .
Pasipo kwanza kuziba pakacha habari zingine zote ni ndoto.. Ufisadi ni adui wa kwanza wa uchumi wa nchi yetu na hata kuleta maisha magumu iwe umeme hadi dawati la mwanafunzi shuleni. Huoni sasbabu ya kusherehekea kwa sababu ya uongozi mbovu ambao umeleta adha hizi zote..Bila kurudisha Miiko na maadili ya viongozi kwanza na kuhakikisha yanafanya kazi hakuna kitu tunachoweza kubadilisha - Good Governance inasimama mbele ya kila kitu...
katika hili nadhani asilimia kubwa ya Watanzania tumepitia maisha haya. na hakika kwa kila uloyasema nimeyaona ktk maisha yangu sijui wewe. lakini Je, mafanikio yangu yametoka wapi? kwanza sikutaka kutazama nyuma wazazi wangu walifanya niniili niwalaumu isipokuwa kuyajua makosa waloyafanya na mimi nisiyarudie. Pili nimesoma kwa taabu sana wala sina haja ya kuyaweka hapa lakini siwezi kuwalaumu wazazi wangu kwa sababu hawakuwa na uwezo. Na kidogo walichokuwa nacho walinunua nyumba ya nyumba sita tukajirundika familia nzima ya watoto tisa..Kweli kabisa.
Lakini huoni kuwa tukisema tusafishe kila kitu kibaya ndipo mengine yafate, hakuna kitakachofanyika?
Naweza kulinganisha tatizo la taifa letu na Mzazi - baba/mama aliyewakosea watoto wake vibaya sana kiasi ambacho
watoto wamekuwa wajasiri wakapiga kelele, wakaibua uozo wa wazazi wale, wakawachambua barabara.Wazazi wale wakaona aibu wee, mwisho wakazoea. Watoto wakaenda kushtaki kwa babu na bibi, babu na bibi kumbe nao walikuwa na madhambi yao.Matokeo wakaamua nao kukaa kimya.Wazazi hata hivyo wakaanza kufikiria, wakaona kweli watoto wana point.Lakini watoto wale wakaweka demands kubwa mno kiasi wazazi wale wakajiskia kukata tamaa.Wasifanye lolote.Unadhani kwa mfano watoto wale wangesema - 1.baba, mama, tunachohitaji ni mtulipie ada tu tuendelee na shule au
2. Baba,mama mmefanya makosa mengi sana maishani, mmekuwa hamna msaada wowote hadi sasa hivi, tunaona aibu hata kuwaita nyie wazazi wetu. Mkitaka tuwaheshimu, basi acheni ulevi, jengeni nyumba bora, tulipieni ada, tuisheni, na mtununulie kila tunachohitaji.
Katika 1 NA 2 kipi rahisi kufanyika?
Samahani nimetoa mfano too simplistic kwa tatizo kubwa lakini ni
kwa ajali ya kuchagiza majadiliano tu, in line with my thread.
I like this. Uhuru ni continuous struggle ... Sio kitu cha dakika moja. Ni kitu we people have to fight for continuously... Na kwa maana hii naona tunaweza kusema kua jana (in the 70's and 80's) tulikua huru kuliko leo (late 90's to date)...Mimi nimechinja mbuzi kufurahi uhuru wa Tanzania, nawahadithia wanangu maana ya uhuru ..
Uhuru ni continuous struggle ..uhuru kiuchumi, kuwa huru kimawazo etc..
Nimeipenda hii Mkuu!Watoto wengi waliozaliwa kuanzia miaka ya 80 hadi sasa,
hawaijui historia ya nchi yetu.Umefanya jambo jema sana la kuigwa.
Niependa ulivyotumia siku ya leo kukaa hususan na watoto.
Je ulijaaliwa kupanua wigo na kujumuika na walio nje ya familia yako?
Duh! Waliozaliwa kuanzia 80 ni watoto! Kiasi Kikwete ajiite kijana