Tupo Wenyewe Ulimwenguni?

Sisi RC tuna amini Mungu aliumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyo onekana(ref. Kanuni ya imani ya kanisa Katoliki la mitume)
Unazungumzia vitu vinavyoonekana na visivyoonekana au viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana, kama ni vitu unajuaje Mungu alimaanisha Upepo, Pumzi au giza?🤣
 
Unazungumzia vitu vinavyoonekana na visivyoonekana au viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana, kama ni vitu unajuaje Mungu alimaanisha Upepo, Pumzi au giza?🤣
Imeandikwa"...Muumba wa mbingu na dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana...." inaonekana imekusanya vyote hata Upepo,Pumzi,Giza,Mwanga n.k. ndo mana inaitwa Kanuni ya Imani
 
Hapana hatuko wenyewe Kuna Alien pia marekani walionekana Lakini trump alikanusha ili kuzuia taharuki
 
Kwa mtazamo wa Kiislamu, si sahihi kusema kwa uhakika kwamba tupo wenyewe katika ulimwengu. Qur’an inasema: “Miongoni mwa ishara Zake ni kuumba mbingu na ardhi na viumbe hai alivyovieneza ndani yake.” (Qur’an 42:29). Hii inaacha uwezekano wa kuwepo kwa viumbe wengine ambao sisi hatujui.

Kwa upande wa sayansi, mpaka sasa hakuna ushahidi uliothibitishwa wa uhai nje ya Dunia. Lakini pia sayansi haijasema kwamba Dunia ndiyo sehemu pekee yenye uhai. Ulimwengu ni mkubwa sana, hivyo uwezekano wa kuwepo maisha mahali pengine hauwezi kufutwa.

Kwa hiyo, Uislamu haukulazimishi kusema tupo peke yetu, na sayansi bado haijathibitisha kama tupo peke yetu au la. Cha muhimu ni kutofanya uwezekano kuwa ukweli kabla ya ushahidi. Allah ndiye Mjuzi zaidi.
 
Kwanini umatumia AI kujibu maswali yetu, wewe huna uwezo wa kujibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…