Tupike Pilau Nazi

Tupike Pilau Nazi

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,425
Reaction score
61,320
Hi guys,. Habari za siku nyingi
Bila kupoteza mda tupike pamoja pilau nazi

Kwenye sufuria yako ya kupikia utaweka mafuta, yakipata moto utaweka vitunguu na ( hoho ni optional)
IMG_3340.jpeg

Utakaanga kwa muda utaweka kitunguu saumu na tangawizi utaendelea kukaanga kwa mda kidogo
IMG_3341.jpeg

Utakaanga kwa mda tena kidogo utaweka pilau masala kijiko kimoja na garam masala nusu kijiko
IMG_3342.jpeg


Utakaanga tena kidogo utaweka nyama yako ambayo imeshachemshwa
IMG_3343.jpeg


Utakaanga kidogo then utaweka viazi na nyanya kidogo,. (Hadi hapa harufu iliwafanya waliochelewa kunywa chai waache watunze njaa kwajili ya pilau😹 )
IMG_3345.jpeg


Utakaanga tena hadi nyanya zilainike kidogo,. Utaweka chumvi halafu utaweka mchele ( mie nimetumia basmati) ila wakawaida ingekua poa sana😍
IMG_3347.jpeg


Utakaanga kwa mda kidogo ili viungo vishikane vizuri,. Then utaweka supu ya nyama utaweka na tui la nazi vikombe viwili au vitatu,.
IMG_3348.jpeg


Utakoroga taratibu taratibu then Utafunika utapunguza moto uache upikike kwa moto mdogo mdogo kwa dakika 25 au hadi nusu saa.
Then utafunua ugeuze na pilau yetu itakua tayari kama hivi
IMG_3356.jpeg


Utatengeneza na kachumbari kidogo,. ( mie niliweka carrot 🥕 hoho kitunguu nyanya na ndimu )
IMG_3357.jpeg


Tukala tukashushia na mirinda nyeusi ya baridi ( pepsi ziliisha )
IMG_3359.jpeg


Hope you enjoyed 😋😍😘
 
Dada mzuri naomba upakue uje tule wote , tujifungie ndani huku tunaangalia movie.....

Kuja kwako hapana, sijawahi kwenda kwa mwanamke na hautokuja kutokea ....

Nb...hongera upo vizuri jikoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom